Mabondia Thomas Mashali kushoto na Fransic Cheka wakitunishiana misuli wakati wa kutambulisha mpambono wao utakaofanyika katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Desemba 25 Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Mabondia Thomas Mashali kushoto na Fransic Cheka wakitambiana mbele ya wandishi wa habari wakati wa kutambulisha mpambano wao wa desemba 25 utakaofanyika katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Bondia Thomas Mashali kulia akizungumza na waandishi wa habari awapo pichani wakati alipokuwa akitambulisha mpambano wake na Fransic Cheka kushoto utakaofanyika katika uwanja wa jamuhuri Morogoro siku ya Desemba 25 Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Mabondia Fransic Cheka kushoto na Thomas Mashali wakiangaliana kwa usongo wakati wa kutambulisha mpambano wao wa desemba 25 utakaofanyika katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS |
KOCHA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI RAMADHANI UHADI KULIA AKIWA NA PROMOTA KAIKE SIRAJU PAMOJA NA BONDIA THOMAS MASHALI |
Mabondia
Thomas Mashali kushoto na Fransic Cheka wakitambiana mbele ya wandishi
wa habari wakati wa kutambulisha mpambano wao wa desemba 25
utakaofanyika katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS Na Mwandishi Wetu MABONDIA Thomas Mashali wa Dar es salaam na Fransic Cheka wa Morogoro wamendelea kutambiana kuelekea mpambano wao wa desemba 25 utakaofanyika katika uwanja wa jamuhuri Morogoro uzito wa kg 76 akiongea na waandishi wa habari Mashali amesema kuwa hii ni vita ya Dar na Moro hivyo kawaomba wapenzi wa mchezo wa masumbwi wa Dar es salaam waweze kuhamia morogoro kwa muda kwa ajili ya kumsapoti siku hiyo ambayo kwake atakuwa na kibaruwa kigumu ambapo atapigana na Cheka pamoja na wakazi wa Morogoro nae Chaka alijibu mapigo hayo kwa kusema siku zote anamweshimu bondia anaetaka mpambano wa marudiano hata hivyo dozi ya mashali ipo pale pale na nitampiga katika raundi za awali tu kwa kuwa nipo vizuri na naendelea na mazoezi nae kocha wa Mashali Ramadhani Uhadi amesema kuwa cheka ni bondia wa kawaida sana hivyo wapenzi waje waone mchezo mzuri utakaochezwa na Mashali atakavyo msambalatisha Cheka siku hiyo mjini Morogoro na kocha wa bondia Cheka Abdallah Salehe amesema Cheka yupo vizuri sana kwa sasa nimempika ameshaiva ata kama mpambano utakuwa leo Mashali atapigwa mapema sana katika mpambano huo kutakuwa na mipambano mingine ya bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' atapambana na Twaha Kassimu kg 63 na Vicent Mbilinyi kg 63 atakumbana na Deo Njiku wakati Pius Kazaula kg 66 atamenyana na Seba Temba mpambano mwingine utawakutanisha mabondia Epson John kg 57 na Sadiq Momba na wana dada Lulu Kayage kg 51 atapambana na Mwanne Haji kugombania ubingwa wa taifa
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa
na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua
sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengipia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha |
No comments :
Post a Comment