Meneja Rasilimali watu wa Airtel, Bi, Gabriella
Kaisi (kulia) akiwapongeza James Kwayu (katikati) na Abubakar Nassor ambao ni
wanafunzi wa vyuo waliofaidika na aiira katika kampuni ya Airtel kupitia
ushirikiano kati ya Airtel na chama cha wanafunzi vyuoni Tanzania AIESEC
wenye lengo la kuwawezesha vijana walioko vyuoni kupata ajira katika
makampuni mbalimbali kila mwaka.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
· Airtel yatoa
ajira kwa wanafunzi wenye vipaji katika vyuo vikuu
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imedhamini
kongamano la ajira kwa vijana wa chuo kikuu linaloandaliwa na AIESEC
Tanzania lenye lengo la kuwaweka pamoja waajiri (makapuni) na waajiriwa
watarajiwa (wanafunzi) kwa lengo la kuwapatia Fursa zitakazowasaidia
katika kuendesha shughuli za kiuchumi.
Kila Mwaka AIESEC huandaa kongamano la ajira kwa
vijana linaloshirikisha wanafunzi zaidi ya 1500 kutoka katika vyuo vikuu
mbalimbali nchini. Kuanzia mwaka jana Airtel imejikita na kushiriki
katika kongamano hilo ikiwa ni sehemu ya kuendeleza dhamira yake ya kuwawezesha
vijana wanaohitimu vyuoni kupata ajira.
Akiongea kuhusu mpango huo, Meneja Rasilimali watu
wa Airtel , Gabriella Kaisi alisema”Tunayofuraha kuwa sehemu ya mpango huu kwa
kushirikiana AIESEC Tanzania lengo likiwa ni kuwafikia na kuwaajiri vijana
wenye vipaji kutoka katika vyuo vikuu mbalimbali nchini. Tunaamini kila kijana
ana nafasi ya kufikia ndoto zake na ndio mana tunatoa fursa kwa
vijana kufanya kazi pamoja nasi.
Mwaka jana tuliwawezesha vijana watatu wahitimu
kutoka vyuo vikuu vya IFM pamoja na chuo kikuu cha Dar es salaam kupata ajira katika
ofisi zetu za Airtel. Vijana hao ni pamoja na Abubakar Nassor ambaye anafanya
kazi katika kitengo cha masoko James Kwayu yuko katika kitengo cha Huduma kwa
wateja na Gerald Msafiri anafanya kazi katika kitengo cha mauzo.
Vijana hawa watapata nafasi ya kwenda kufanya kazi nje ya nchi katika
makao makuu ya Airtel nchini Kenya na India kwa muda wa mienzi
miwili kuanzia mwezi wa Mei hadi Julai 2016. Watakaporudi watapangia kufanya
katika vitengo tofauti ili kupata uzoefu na mwanga zaidi aliongeza Kaisi
Akiongea kuhusu program hiyo, moja kati ya
waliofaidika na mpango katika kitengo cha masoko, Abubakar Nassor alisema”
najisikia furaha kuwa mwanachama wa AIESEC Tanzania kwani kumeniwezesha kupata
fursa hii adimu ya ajira, uzoefu katika kazi na nafasi ya kujifunza katika
kampuni kubwa ya simu duniani. Nimejipanga vyema kujifunza zaidi katika miezi 2
nitakayokuwa nchini India na Nairobi, nahaidi kuitumia fursa
hii vyema ili kuweza kuzifikia ndoto zangu
Mwaka huu Airtel imejipanga kuendelea kuwafikia
vijana wengi zaidi kwa kutoa ajira kwa vijana wengine watano ambao watafanya
vizuri na kufaulu mitihani mbalimbali inayoendelea kwa sasa.
No comments :
Post a Comment