Mkurugenzi wa Utalii na Masoko TANAPA Ibrahim Mussa.
Akizungumza leo kwenye Mkutano wa mwaka wa hifadhi za taifa Tanzania TANAPA, wa mwaka wa Hifadhi za taifa Tanzania na Wahariri na waaandishi waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari unaoendelea kwenye ukumbi wa VETA ,Mkoani Morogoro Mkurugenzi wa Utalii na Masoko TANAPA Ibrahim Mussa alisema kuwa matangazo hayo ya bure ya mlima Kilimanjaro yamekuwa yakiwekwa kwenye ndege zingine alizozitaja na kuonesha picha ambazo ni Shirika la KLM na Shirika la ndege la Ethiopia.
"Hakuna ubaya wowote kwa KQ kutangaza mlima Kilimanjaro, pia huwezi kuwa na haki miliki ya mlima kutokana na sheria za kimataifa, tunaweka nguvu sana kuilaumu kenya jambo ambalo siyo sahihi" alisema Mussa.
Aidha aliongeza kwa kusema "tuseme ukweli ukiwa Amboseri nchini Kenya ni eneo la mbuga tu hivyo mlima Kilimanjaro unaonekana vuzuri zaidi hata ukipiga picha ndiyo maana wakenya husema 'Come Amboseri to see mount Kilimanjaro' wako sahihi alisema.
"Tuwaache wafanye matangazo sababu wanatuletea fedha huku wao wakibeba hao watalii kupitia ndege zao" alisema Mussa. Akifafanua kuhusu kuyeyuka kwa barafu ya mlima Kilimanjaro alisema kuna utafiti mkubwa unaendelea na kufanywa na wataalam, pia akihusisha kuwa inawezekana ikawa ni mabadiliko ya tabianchi na pia huu ni mjadala mrefu linalohusu Sayansi zaid huku akiwatoa hofu watu kama mlima huo unaweza kuyeyuka.
No comments :
Post a Comment