Profesa Winiester Andersonkutoka( UDSM).
Watanzania na jamii nzima wametakiwa kujenga tabia ya kuwa watalii wa
ndani ikiwa ni katika kukuza utalii na uchumi wa ndani. Endapo
watanzania watawajengea watoto wao utamaduni wa kutangaza vivutio
tulivyonavyo kwenye hifadhi za taifa, wanyama pori, maziwa , mapango ,
milima.
Hayo yamesemwa leo asubuhi na Profesa Winiester Anderson kutoka Chuo
Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), kwenye mkutano wa mwaka wa hifadhi za
taifa Tanzania na Wahariri na wanahabari waandamizi kutoka vyombo
mbalimbali vya habari nchini unaendelea kwenye Ukumbi wa VETA mkoani
Morogoro.
"Utalii wa ndani hasa barani Afrika unakua kwa kasi hivi sasa, na ina
sadikika kuwa utalii wa ndani ni mara kumi zaidi ya watalii wanaotoka
nje ya nje" alisema Profesa Anderson.
"Utalii wa ndani unakua zaidi ya asilimia kumi tofauti na ule wa
kimataifa ambao unakua kwa asilimia tatu tu na ni wa msimu ambapo
watalii wa nje ratiba yao ya utalii inafahamika huja nchini kati ya June
na Oktoba kila mwaka, dunia nzima ndivyo ilivyo utalii wa kimataifa
ukiwa chini unahitaji utalii wa ndani".
"Lengo la kutengeneza utalii wa ndani ni kuziba mapengo ya watalii na
ukitangaza utalii wa ndani unabakisha fedha katika uchumi wa ndani ya
nchi" alisema Profesa Andason Profesa.
Anderson ametoa wito kwa Watanzania kuanza kufundisha namna bora ya
kumjali mteja, alisema hivyo kwa sababu hivi sasa changamoto ya watoaji
huduma ni mbovu na wengi wao wanatakiwa kufundishwa thamani ya mteja ili
kuweza kuongeza pato na kutoa sifa nzuri ya utalii ndani na nje ya
nchi.
Utalii ni pato siyo idadi kubwa ya watalii tunawaambia watanzania
wajiandae ili kuweza kukabiliana na changamoto ya kupqmbana na soko la
utalii barani Afrika. Wakati huohuo amezungumzia umuhimu wa ukosefu wa
taarifa kwa watalii kwani wengi wamekuwa waking'anywa taarifa za kibali
za kununua vinyago ambavyo hunyang'anywa Uwanja wa Ndege na nchi
kuonekana ni wezi.
"Inabidi itungwe sheria ambayo itaweka wazi haki ya mtalii kununua
kinyago na haki yake ya kusafiri nacho tofauti na ilivyo hivi sasa kwani
wengi bada ya kununua siku wanapoondoka huishia kulia baada ya
kulazimika kuacha vinyago vyao hivyo inabidi hili jambo liangaliwe
sababu halileti sifa nzuri kwa taifa letu" alisema Profesa Andason.
No comments :
Post a Comment