Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, August 10, 2016

HASSAN ABBAS ATEULIWA KUWA MKURUGENI MPYA WA HABARI MAELEZO NA MSEMAJI WA SERIKALI






Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye amemtangaza Bw.Hassan Abbas kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali kuanzia Agosti 5 Mwaka huu.

Uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria za Utumishi wa Umma Namba 8 ya mwaka 2002 kifungu Namba 6(1)(b) kufuatia uhamisho wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara hiyo Bw. Assah Mwambene uliofanyika tarehe 7 Machi 2016 kwenda Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mhe.Nape Moses Nnauye ametoa wito kwa Wanahabari na Wananchi kwa ujumla kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Bw Abbas atakapokuwa anatekeleza majukumu yake.

“Ninawaomba Wanahabari na Watanzania kwa ujumla mumtambue Bw Abbas na mtoe ushirikiano unaostahili katika utendaji wa kazi zake”.Alisema Mhe. Waziri.

Aidha Mhe. Waziri Nape alimpongeza Bibi Zamaradi Kawawa aliyekuwa anakaimu nafasi hiyo kwa kujituma na kusimamia majukumu yote ya Idara kwa ukamilifu na uadilifu.

Kwa upande wake Mkurugenzi huyo mpya amekubali uteuzi huo na ameahidi kuitumikia nafasi hiyo kwa uadilifu mkubwa na ameomba ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wafanyakazi wa Idara ya Habari Maelezo na Watanzania kwa ujumla.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Hassan Abbas alikuwa ni Meneja Habari na Mawasiliano katika Ofisi ya Rais inayosimamia Utekelezaji wa Program ya Matokeo Makubwa sasa (President`s Delivery Bureau).

No comments :

Post a Comment