
Mshindi wa jumla wa mashindano ya kuwania kombe la Johnnie
Walker Waitara 2012 Sudson Manatsa akinyanyua juu vikombe vyake viwili alivyoshinda
wakati wa Mashindano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya
Gofu Lugalo jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yalidhaminiwa na Kampuni ya
Bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake kikali cha Johnnie Walker.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL)
Stephen Gannon akimkabidhi zawadi Mshindi wa pili wa daraja A, Aidan
Nziku kikombe na zawadi nyingine baada
ya kuibuka mshindi wa kundi hilo katika mashindano ya kuwania kombe la Johnnie
Walker Waitara 2012. Kampuni
ya Bia ya Serengeti imedhamini mashindano hayo kupitia kinywaji chake cha
Johnnie Walker.
No comments :
Post a Comment