BAADA ya
kutamba na wimbo wake wa ‘Apate Raha’, msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini,
Ismail Sadick ‘Suma Lee’, anajipanga kuachia wimbo wake mmoja kati ya nyimbo
tano ambazo ameziandaa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Suma Lee alisema katika stoo yake ana
nyimbo zaidi ya nne, ambazo ameziandaa na hajui aanze kuitoa ipi kutokana na
ubora zilizonazo.
Alisema baadhi
ya nyimbo ambazo tayari amezirekodi ni ‘UK Dubai’, ‘Moyo Safi’, ‘Nimekaa’,
‘Hesabu za Mapenzi’ na ‘Ndoa’, hivyo bado yupo kwenye wakati mgumu, aanze na
upi.
“Baadhi ya
mashabiki wanasema nimeishiwa mistari, wengine wanasema sitaki ‘Hakunaga’
ichuje ndiyo maana sitoi wimbo mwingine, naomba mkae mkao wa kula, vitu vizuri
vinakuja,” alisema Suma Lee.
Mbali na vibao
hivyo, Suma Lee alishawahi kutamba na nyimbo zake kama ‘Hakunaga’,
‘Utanikumbuka’, ‘Chungwa’ na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya
vizuri katika tasnia ya muziki wa bongo fleva.
No comments :
Post a Comment