Na Elizabeth John
TIMU za Tanzania zimejitoa kushiriki
mashindano ya klabu bingwa ya Afrika Mashariki katika mchezo wa Netiboli.
Timu hizo ni ambazo zilitakiwa
kushiriki mashindano hayo ni Filbert Bayi, JKT Mbweni na Jeshi Stars.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana,
Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA), Annie Kibira alisema kila
timu imejitoa kushiriki mashindano hayo kwa sababu mbalimbali.
“Kila timu imejitoa kwa sababu yake, ni vigumu
kuelezea sababu, hivyo hatutashiriki mashindano hayo kwasasa tunajiandaa na
mashindano ya klabu bingwa ya taifa,” alisema Kibira.
Alisema klabu zote ambazo zinatarajia kushiriki mashindano ya klabu
bingwa ya taifa, zinatakiwa kujiandaa na mashindano hayo ambayo yanatarajia
kuanza kutimua vumbi Agosti 24 jijini Mbeya.
“Klabu 20 zinatarajia kushiriki mashindano hayo, timu zinatakiwa
zianze maandalizi mapema ili kuweka mashindano hayo kuwa ya kishindani zaidi,”
alisema.
No comments :
Post a Comment