Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Monday, March 17, 2014

AIRTEL yakabidhi shilingi million Tano kwa wanawake kwa ajili ya Tuzo ya Mwanamakuka 2014


 

Afisa uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde (kushoto) akimkabithi mfano wa hundimwenyekiti na Mratibu wa Mradi wa The Unity of Women friends Maryam Shamo wakati wa halfa ya Tuzo za Mwanamakuka 2014 ambapo Airtel Tanzania ni moja kati ya Wadhamini wa tuzo hizo,  Bi Leil Mwambungu aliibuka na kutangazwa mshindi wa mwanamakuka 2014. Akishuhudia ni Mkurugenzi  Mkuu wa Bank ya Wanawake  Tanzania Bi Margreth Chacha (wakwanza kulia), Hafla ya mwanamakuka ilifanyika jana katika ukumbi wa Escape 1 mikocheni Dar es salaam. 

 Afisa uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde (kulia) akimpongeza mshindi wa mwanamakuka 2014 bi Leila Mwambungu mara baada ya kutangazwa katika halfa ya Tuzo za mwanamakuka iliyofanyika Escape 1 jijini Dar esaalam
mshindi wa mwanamakuka 2014 bi Leila Mwambungu mara baada ya kutangazwa katika hafla ya Tuzo za mwanamakuka iliyofanyika Escape 1 jijini Dar esaalam, pichani kushoto ni Mkurugenzi  Mkuu wa Bank ya Wanawake  Tanzania Bi Margreth Chacha

========  ========  =========
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel  imekabithi waandaaji wa Tuzo za mwanamakuka The Unity of Women Friends kiasi cha million tano pesa taslimu wakati wa halfa ya  tuzo za mwanamakuka 2014 zilizofanyika jijini Dar es saalam mwisho wa wiki
Tuzo hizi za mwanamakuka 2014 ziliwashirikiasha washindi 10 wa mwaka 2012 na mwaka 2013 ambapo washindi hawa walifatiliwa biashara zao na kuchaguliwa mshindi mmoja aliyefanya vizuri na kutumia vyema zawadi aliyoshinda katika kuendeleza biashara zao ambapo bi Leila Mwambungu aliyekuwa mshindi wa pili mwaka Jana kuibuka kuwa mshindi wa mwanamakuka 2014
Akiongea wakati wa kukabithi zawadi hiyo, Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde alisema”  Tunayofuraha kuwa  wadhamini  wa tuzo hizi za mwanamakuka kwa miaka mitatu mfululizo kwa sasa na kuwa sehemu ya kuleta mabadiliko kwa wanawake kupitia tuzo hizi. tunafurahi kuona jinsi kina mama hawa wajasiriamali walioshinda miaka iliyopita wakifanya vizuri katika biashara zao.
Na sisi Airtel leo tunakabithi kiasi cha kiasi cha shilingi milioni tano kama mchango wetu kwa tuzo hizi za mwanamakuka kwa mwaka 2014. Tunaamini kiasi hichi cha fedha kitaweza kuwawezesha waaandawaji wa tuzo hizi kufanikisha halfa hii na kuwafikia wanawake na kuwawezesha  kutanua mitaji yao na hatimae kuongeza kipato na faida zaidi na kujikwamua kiuchumi”.
“Tutaendelea kushirikiana na The unity of Women Friends ili kuhakikisha tunaweza kuwafikia wanawake wengi zaidi nchini” aliongeza Matinde.
Kwa upande wake mshindi wa mwanamakuka 2014 bi Leila Mwambungu Alisema “naona fahari na furaha kuwa mshindi wa tuzo hizi za mwanamakuka kwa mwaka huu, napenda kuwashukuru sana waandaaji wa tuzo hizi kwa kuniona kupitia juhudi ninazoziweka katika kazi zangu na biashara zangu. Mpaka sasa nimeweza kuajiri watanzania kupitia biashara zangu na  Kiasi hii nilichozawadiwa leo kitanisaidia sana kukuza mtaji. 

Cha msingi wanawake tupendane na kushirikiana napenda kuwahasa wanawake wenzangu kutokata tamaa na kuongeza  katika biashara zao,  haijalishi kama mtaji mdogo bali wajipange na kujikita katika uzalishaji na hatimae kuinua mtaji na kuweza kufanya biasha kwa mtaji mkubwa, hakuna siri nyingine ya mafanikio zaidi ya jitihada , hari na kujiwekea malengo na kuhakikisha yanafikiwa kwa wakati uliopagwa.
Naye mwenyekiti na Mratibu wa Mradi wa The Unity of Women friends Maryam Shamo alisema Tuzo hizi za Mwanamakuka zinaendelea kukua na kuziboresha zaidi,   kwa mwaka huu lengo letu lilikuwa ni kuwawezesha wachache kwa kuwafatilia washindi wetu 10 wamiaka iliyopita na kuona jinsi gani biashara zao zinavyoenda na kumzawadia anayefanya vizuri zaidi. Lengo ni kuendelea kuwahamasisha na kufatilia mafanikio yao kwa karibu.
vilevule tukiangalia miaka iliyopita tuliweza kuwashirikisha wanawake tu katika sherehe za tuzo hizi lakini kwa mwaka huu tumeamua kushirikisha familia kwa kuandaa bonanza ambapo wakinababa na watoto kwa pamoja tunasherehekea mafanikio haya, na kusherehekea siku ya wanawake duaniani huku tukienzi juhudi za wanawake jasiri nchini na kuwazawadia
Tunashukuru sana Airtel kwa kushirikiana nasi miaka mitatu kwa sasa na tunaamini kuwa bado wataendelea kutoa mchango wao na kushirikiana nasi na kutuunga mkono kwa miaka mengine ijayo na kuhakikisha lengo letu la kumwinua mwanamke wa kitanzania linafikiwa. Alisema Shamo

Kwa mwaka huu Tuzo hizi zilishirikisha washindi waliopatikana miaka iliyopita ambapo kati yao pamoja na Tatu  Ngao, Mwananne Msekalile, Sikudhani Daudi, Nasra, Aziz, Khalid, Leila Mwambungu, Selestina Renatus, Maajab Yusufu na Agnes Daudi  ambapo Bi Leila Mwambungu Ameibuka kuwa mshindi wa mwanamakuka 2014

No comments :

Post a Comment