Mabondia
wanaotegemea kupigana jumamosi kugombea ubingwa wa UBO international katika
ukumbi wa Karume zamani PTA hall, wakiongozwa na Thomas Mashali na Japhet
kaseba wanategemea kupima uzito siku ya
ijumaa katika hotel ya National hotel
iliyopo maeneo ya keko kuanzia saa tatu asubuhi. Akizungumza na wanahabari hizi
bw Ibrahim kamwe amesema kuwa mabondia wote wanaocheza mapambano ya utangulizi
wapo katika hali nzuri na wale mabondia wa mikoani wanategemea kuingia kesho alhamis
wakiongozwa na alan kamote atakaecheza pambano la ubingwa wa Africa dhidi ya
karage suba ambae amekuwa mbadala wa bondia fadhili awadh aliyefariki kwa ugonjwa
wa malaria kali iliyomkuta kipindi akijiandaa na mapambano haya ya ubingwa,
mapambano mengine yatakayopigwa siku hiyo yatakuwa kama ifuatavyo fredy sayuni motto
wa keko atazipiga na Rajab mahoja wa tanga kugombe ubingwa wa taifa wa PST
mabondia hawa walishawahi kuzipiga mkwakwani tanga na sayuni kuchezea kichapo
kikali, safari hii Fredy sayuni anakutana nae tena kwao akitaka kulipa kisasi. Baina
Mazola wa mzazi atapambana na Bakari dunda, huku dogo anayekuja juu kwa kasi na
wengi humpenda kwa staili ya uchezaji wake Issa omar Nampepeche au “peche boy”
atapimana ubavu na bondia mkongwe bingwa wa bantam Zuberi kitandula pia
kutakuwepo na mapambano mengine mengi tu pamoja na lile la juma fundi na haji
juma, shaban mtengela na jumanne Mohamed, jocky hamis na said chaku pambano la
wakongwe hili .nao watakuja kupima afya zao na uzito kwa mara ya mwisho
wakisubiri hukumu ya ulingoni
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment