Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, April 13, 2014

MATAYARISHO YA MATENGENEZO YA KUREJESHA MAWASILIANO YA BARABARA KATI YA DAR – BAGAMOYO YAENDELEA



Sehemu ya barabara iliyobomolewa katika Daraja la Mpiji kwenye barabara ya Dar es Salaam - Bagamoyo.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akipokea maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Alhaj Mussa Iyombe (aliyenyoosha mkono). Kulia ni Mbunge Mteule wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (mbele mwenye kofia) akiongozana na viongozi wengine wakati walipotembelea kukagua sehemu ya barabara iliyobomoka katika barabara ya Dar – Bagamoyo. Wengine kutoka kushoto ni; Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Said Mick Saddik na Mbunge Mteule wa Chalinze, Mhe. Ridhiwan Kikwete.Sehemu ya barabara na daraja.
Mawasiliano ya barabara kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo yamejifunga kutokana na barabara hiyo kubomolewa na maji katika Daraja la Mpiji mpakani mwa mikoa wa Dar es Salaam na Pwani.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alifanikiwa kufika katika eneo hilo mara tu baada ya kupokea taarifa za kukatika kwa barabara hiyo.
Akiwa ameongozana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Alhaj Mussa Iyombe pamoja na watendaji wengine kutoka TANROADS, Waziri Magufuli amewaagiza watendaji hao kuhakikisha kuwa wanafanyakazi mchana na usiku ili barabara hiyo muhimu na yeye kupitisha magari mengi ifunguliwe mapema iwezekanavyo.
Zaidi ya maelekezo hayo, Mhe. Magufuli pia ameagiza kuahirishwa hadi itakapopangwa baadaye kwa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa TANROADS ambalo lilikuwa limepangwa kufanyika kuanzia siku ya Jumanne ya tarehe 15 Aprili 2014 huko mkoani Tanga. Hatua hiyo imechukuliwa ili watendaji hao wabaki katika vituo vyao vya kazi hadi hali ya mvua zinazoendelea kutulia na taarifa nyingine kutolewa.
Akizungumzia hali katika eneo hilo la Mpiji, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Alhaj Mussa Iyombe kwa upande mwingine alibainisha kuwa kilichozolewa na maji ni sehemu ya barabara na siyo daraja lenyewe la Mpiji.
Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali hapa nchini zimesababisha madhara kadhaa kwa upande wa miundombinu ya barabara. Waziri Magufuli ameendelea kutahadharisha kuhusu shughuli za uchimbaji wa mchanga zinazofanywa karibu au chini ya madaraja, kwamba kwa maeneo mengi ndicho chanzo cha mito kuhama kutoka katika njia yake ya asili na kubomoa barabara. “Kama manavyoona daraja lenyewe ni zima na linauwezo mkubwa wa kupitisha maji lakini mto umehama kutokana na uharibifu wa mazingira” alisistiza Mhe. Magufuli.
Daraja la Mpiji lilifunguliwa rasmi mwezi Julai 2005 na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete wakati huo akiwa ni Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
TANROADS kwa kushirikiana na kampuni za ujenzi za SKOL na Estim Construction Company Limited zote za Dar es Salaam tayari wameanza kazi za kurekebisha sehemu hiyo.(PICHA / HABARI: MICHUZI BLOG)

No comments :

Post a Comment