Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, April 24, 2014

Mhe Temba, Chegge Waueni sasa!



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjx3tBUXPISt5ol2OyKCzpUBVIrXy-WZU3Gg2Urt_U2Z9mFmxnh4TW86aQ-fQQGjU9wOwRz4cjwWrtV4UZKaOJGyqCyxvMUmsNx7gZnw7KCi8yc6RZNe8LQWvz_vn5sC8bjGdAA0uQw/s1600/Temba+and+Chege.jpgNYOTA wa muziki wa kizazi kipya wanaotoka kundi la TMK Wanaume Family, Chegge na Mhe Temba wanatarajia kuachia hewani wimbo wao mpya uitwao 'Waue' waliowashirikisha 'membaz' wa Mkubwa wa Wanawe.
Wasanii walioshirikishwa na wakali hao ni Maromboso na YP ambao nao wanatokea 'ukoo' wa TMK Wanaume Family na Mkubwa na Wanae.
Mkurugenzi wa Mkubwa na Wanawe na Meneja wa wasanii hao, Said Fella 'Mkubwa' aliiambia MICHARAZO kuwa, wimbo huo utaachiwa 'audio' na video wiki mbili zijazo baada ya kukamilisha baadhi ya mambo.
Mkubwa, alisema wimbo huo umerekodiwa katika studio zao za Mkubwa na Wanae chini na mtayarishaji, Shirko na video imefanywa na Adam Juma kupitia kampuni yake ya Visual Lab.
"Wasanii Temba na Chegge wamekamilisha kurekodi 'audio' na video ya wimbo wao uitwao 'Waue' wallioimba na Maromboso na YP, na tunapanga kuachia kazi hizo kwa pamoja wiki ijayo," alisema.
Chegge na Mhe Temba wamekuwa wakitoa kazi za pamoja mbali na zile za binafsi za kila mmoja nje ya nyimbo za kundi lao la TMK Wanaume Family.

No comments :

Post a Comment