Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, May 29, 2014

BUJINGA TRADERS WATENGENEZAJI WA FLIERS,POSTERS,CARDS & CARENDER



BUJINGA TRADERS WATENGENEZAJI WA  FLIERS,POSTERS,CARDS & CARENDER WAPO MACHINGA COMPLEX  4TH FLOOR E4, EAST WING
Email; johnson@bujingatradere.com,info@bujingatraders.com
www.bujingatraders.com
P.O. BOX 43064
Dar es Salaam Tanzania 
Cell+255765224522 Tel;+255773623320
Tanzania East Africa


BUJINGA TRADERS WATENGENEZAJI WA  FLIERS,POSTERS,CARDS & CARENDER WAPO MACHINGA COMPLEX  4TH FLOOR E4, EAST WING
Email; johnson@bujingatradere.com,info@bujingatraders.com
www.bujingatraders.com
P.O. BOX 43064
Dar es Salaam Tanzania 
Cell+255765224522 Tel;+255773623320
Tanzania East Africa

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA MKUTANO WA MASHAURIANO WA BODI YA USAJILI WA MAKANDARASI KWA MWAKA 2014 JIJINI DAR LEO.




 Makamu wa Rais Dkt Bilal, akipokea zawadi baada ya kufungua rasmo mkutano huo kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi. 
 Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Mkutano wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa mwaka 2014, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam leo mchana. Mbali na ufunguzi wa mkutano huo pia Makamu, alishuhudia hafla ya kuapishwa kwa Wakandarasi.

SUGU AMLIPUA ZITTO




Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe sio tu ni Mbunge anayebanwa na masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, bali pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Fedha za Serikali (PAC). Kwa mujibu wa kipengele cha 12 cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge lako tukufu, mojawapo ya majukumu ya PAC ni kushughulikia maeneo yenye matatizo sugu ya matumizi mabaya ya fedha za umma katika Wizara na Mashirika ya Umma yaliyoainishwa katika taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. NSSF na TANAPA ni baadhi tu ya Mashirika ya Umma yaliyo chini ya usimamizi wa kibunge wa PAC. 

Kwa maana hiyo, Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Zitto Kabwe, kwa kutumia makampuni yake ya Leka Dutigite Ltd. na Gombe Advisors Ltd., amefanya biashara na TANAPA, shirika la umma analolisimamia kama Mbunge na Mwenyekiti wa PAC. Mheshimiwa Zitto Kabwe na wanamuziki washirika wake, kwa kutumia makampuni ya Gombe Advisors Ltd. na Leka Dutigite Ltd., wamelipwa fedha za umma za TANAPA na NSSF. 

Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kutoa maelezo juu ya madai ya ukiukwaji wa Sheria uliofanywa na viongozi wa umma na mashirika ya umma katika kashfa hii. Pamoja na maelezo yatayotolewa , Kambi Rasmi ya Upinzani inataka Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi maalum juu ya matumizi ya fedha zilizotolewa na TANAPA na NSSF; msukumo uliofanya fedha hizo zitolewe na matumizi ya fedha hizo kwa kuzingatia masharti yanayosimamia fedha za umma na utawala bora katika usimamizi wa fedha za umma.
 Aidha, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ifanye uchunguzi juu ya malipo na matumizi husika kwa kurejea masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Sheria nyingine zinazohusika. Kwa upande mwingine, kwa kuwa suala hili linahusu mbunge na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayohusika na usimamizi wa fedha za umma, Kamati ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge nayo ifanye uchunguzi wake juu ya madai ya masharti ya Katiba ya Nchi, Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge na Kanuni za Bunge juu ya maadili ya kiongozi wa umma ikiwemo yahusuyo utangazaji wa maslahi.

MAANDALIZI MISS UKONGA 2014 YANAENDELEA








  Wasichana washiriki mashindano ya miss ukonga 2014 wilaya ya ilala jijini dar es salaam wapatao 16, ambapo kila mmoja ana ndoto za kuchukua ushindi.
warembo hao  wakiongea na mwandishi wa blog hii.walitaka
jamii hiyelewe  kuwa urembo siyo uhuni bali ni kipaji cha mtu kama vipaji vingine vilivyo hivyo wazazi wasiwakatalie watoto wao kushiriki
 mashindano hayo ya urembo kwani ni moja ya
ajira rasmi kama zingine..
katika mashindano hayo kwanza wanafundisha  maadili mema, nizamu, kujituma ,kushirikiana na jamii,kufanyakazi,pia nakujali imani ya mtu yeyote
warembo hao wamesama katika washiriki hao wengine ni wasomi wa vyuo vikuu ,kwani wemesama watakavyo pata nafasi hiyo itakuwa msaada kwa jamii  kuwa elimisha,tamaduni za

 asili ya tanzania na kuzitangaza nje 

WAZIRI DK. MUKANGARA AWASILISHA BUNGENI HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO BUNGENI




Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara akiwasilisha Bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara yake kwa mwaka 2014/2015 mjini Dodoma jana. Waziri Mukangara ameomba Wizara yake iidhinishiwe kiasi cha Shilingi, 35,371,884,000 ambapo kati ya hizo jumla ya shilingi 20,371,884,000 ni za matumizi ya kawaida na kiasi kilichobaki ni fedha za miradi.

 Viongozi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Habari wakifuatilia Hotuba hiyo.
 Baadhi ya wadau wa Habari akiwepo Mkurugenzi wa Kituo cha Redio 5 cha jijini Arusha Francis Robert (kushoto) akifuatilia hotuba hiyo bungeni mjini dodoma leo.
 Innocent Mungy kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) akifuatilia mjadala wa Bajeti bungeni mjini Dodoma.
 Wadau mbalimbali wa sanaa, Michezo na Utamaduni walikuwepo.
 Wasanii wakifuatilia mjadala wa bajeti Bungeni, mtaalm Dude na kule P Funks mwaandaaji wa muziki na pia msaani wa muziki.

Wednesday, May 28, 2014

FILAMU YA JOTI SANDUKU LA BABU YAINGIA SOKONI




MSANII  Lucas Mhavile ‘Joti’baada ya kukaa kimya kwa mda sasa ameibuka na filamu yake ya Joti Sanduku la Babu ambayo amecheza katika husika tofauti tofauti filamu hiyo itakuwa ikisambazwa na   Kampuni ya proin promotions ya jinini Dar es salaam.
Akizungumzia filamu hiyo Joti alisema kuwa amekuja kivingini kwani kitu alichofanya katika filamu hiyo aijawai kutokea wala kufanywa na mtu yoyote yule katika tasinia hii ya filamu nchini.
 Hivyo wapenzi wangu wanunue filamu kwa ajili ya kuniunga mkono kwani kwa sasa imeshaingia sokoni na filamu hii si yakukosa mana unambiwa uzee mwisho chalinze mjini kila mtu honey.
Hivyo wapenzi wa filamu nawaomba wanunue nakala alisi ya filamu hiyo pindi itakapotoka ambapo nimelezea mambo mbalimbali ya ujana usichana pamoja na uzee.
 Mbali na hivyo filamu hiyo imebeba mambo matatu muhimu kwanza ina burudisha pia ina elimisha na kupata ujumbe muhimu kabisa katika jamii inayotuzunguka.'

Filamu hiyo ya kwanza tangu joti aweke kando mambo ya filamu na kujingiza katika mambo ya uchekeshaji kupitia luninga sasa ameludi tena katika filamu.
yake mwenyewe inayokwenda kwa jina la joti sanduku la babu.

WAREMBO MISS TABATA 2014 WAJIFUA DAR WEST PARK



 Warembo wanaoshindania miss Tabata 2014 wakiwa kwenye pozi wakati wa mazoezi ya shindano hil. Mashindano haya ya Miss Tabata 2014 yatafanyika kwenye ukumbi wa Dar West Park.
 Warembo watakaochuana vikali kwenye shindano la Miss Tabata 2014 wakiwa watokelezea kwenye pozi tofautitofauti wakati wa mazoezi yanayoendelea eneo la Tabata Dar West Park.
Warembo watakaochuana vikali kwenye shindano la  Miss Tabata 2014 wakiwa kwenye mazoezi.
Ilifika kipindi cha kutoa burudani ilikuwa ni noma sanaaaaaa!

SHIRIKA LA POSTA KUTOA HUDUMA KATIKA VIWANGO VYA KIMATAIFA


IMG_6281(2)Meneja Masoko wa Shirika la Posta Tanzania Bw. David George akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es salaam kuhusu mafanikio yaliyofikiwa na shirika hilo hadi sasa ikiwemo kuanza kutumika kwa anuani za makazi na Misimbo ya posta (Post code) inayolenga kuboresha huduma za shirika hilo,kulia ni Kaimu Meneja huduma za barua Bw.Jason Kalile.
(Picha na Idara ya Habari Maelezo)
Frank Mvungi- Maelezo
Shirika la Posta Tanzania linatarajia kuanza kutoa huduma zake kwa wananchi kwa kutumia mfumo wa anuani za Makazi na Misimbo ya Posta kabla ya Mwisho wa Mwaka huu.
Hayo yamesemwa na  Meneja Masoko wa Shirika hilo Bw. David George wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Akifafanua David  amesema kuwa kwa kuzingatia mpango kazi wake shirika hilo limedhamiria kufikia mwakani nusu ya Mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani iwe imefikiwa na huduma ya anuani za Makazi na Msimbo wa posta.
Aidha David amesema kuwa huduma hiyo tayari imeanza kutolewa katika Mikoa ya Arusha  ambapo imehusisha kata 8, Dodoma kata 8, na Dar es salaam  hadi kufika June 2014 kata 27 zitakuwa zimefikiwa ambapo lengo kuu ni kuboresha huduma  na kufikisha barua pamoja na vifurushi katika makazi ya wateja kwa wakati.
Pia David alieleza kuwa Shirika hilo lina mpango kabambe wa kuleta mabadiliko makubwa katika uendeshaji na utoaji huduma za Posta nchini ili kunufaika na fursa zinazoletwa na mabadiliko ya teknolojia,kuboresha huduma,kukidhi mahitaji ya soko na kukabiliana na ushindani.
Akifafanua Bw. David amesema lengo ni na kuongeza tija kwa kutoa huduma zenye viwango vya kimataifa.
Shirika la Posta Tanzania linatekeleza mpango wa miaka 10 ( 2014-2023) unaozingatia juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali kupitia utekelezaji wa sera na mipango mbalimbali ikiwa ni pamoja na Dira ya maendeleo ya Taifa 2025, Mpango wa Matokeo wakubwa sasa,sera ya posta 2003,Mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini (MKUKUTA),Mpango wa kurasimisha rasilimali za biashara za wanyonge (MKURABITA),Mfuko wa Taifa wa anuani za Makazi na Sera ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA.)

Zoezi la ukaguzi wa Stempu kwenye bidhaa za Filamu latikisa Dar


TRA1a Mjumbe wa Kamati ya Urasimishaji wa Kazi za wasanii wa Filamu na Muziki hapa nchini  ambaye pia ni Afisa kutoka Bodi  ya Filamu Tanzania Bw. Wilhad Tairo akifafanua jambo kwa mfanyabiashara wa duka la Filamu wakati wa Operesheni ya kukagua Bidhaa zisizo kuwa na Stempu za TRA, Operesheni hiyo ya wiki mbili iliyoanza jana jijini Dar es Salaaminatekelezwa kwa uhirikiano wa TRA, Bodi ya Filamu, Basata na Cosota 
TRA2 Mfanyabiashara wa duka CDs za Filamu lililopo maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam akieleza  jambo kwa maafisa wa Kikosi kazi kwa ajili yakukagua bidhaa ambazo azizingatii taratibu kabla ya kuingizwa sokoni leo jijini Dar es Salaam.
TRA3a Muuzaji wa duka la CD za Filamu katika mitaa ya Kariakoo jijini Dar es Salaam akiwaonyesha Stempu za TRA katika CD zake wakaguzi kutoka TRA,Bodi ya Fila, Basata na Costa ambao walifika dukani kwake kwa ajili ya ukaguzi wa bidhaa ambazo zimeingizwa sokoni bila kufuata taratibu za kisheria iliwemo kuweka Stika za TRA  kama sheria inavyotaka.Kamati ya urasimishaji wa kazi za wasanii wa Filamu na Muziki wameanza Operesheni ya wiki mbili katika jiji la Dar es Salaam ili kuleta ufanisi katika mapato ya Wasanii.
TRA5 Afisa Kodi Msaidizi Bi. Theophilda Majara( Mwenye blauzi nyekundu) akikagua baadhi ya CD za Filamu wakati wa Operesheni ya kukagua Filamu ambazo hazijafuata taratibu za kisheria ikiwemo kulipia Stempu ya TRA kabla ya kuingia sokoni. Zoezi hilo linaendeshwa kwa ushirikiano wa TRA, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Bodi ya Filamu, Basata  na Costota .
TRA6Baadhi ya wananchi wakifuatilia namna Operesheni ya kukagua Filamu zilizoingia sokoni bila kufuata utaratibu namna inavyotelekelezwa  jana katika mitaa ya Kariakoo jijini Dar es Salaam.
 Picha na Frank Shija- Afisa Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

MASTAA WATEMBELEA KABULI LA MANGWEAR ALIPOZIKWA KATIKA KUMBUKUMBU YA KUFA KWAKE



R.I.P Mangwea

Tuesday, May 27, 2014

TANZANIA MOVIE TALENTS SASA KUANZA JIJINI DAR ES SALAAM



 
KARIBU  UCHUKUE  FOMU  NI  BUREEEEEEEEE
Baada ya Kumaliza shindano la Tanzania Movie Talents Kwenye Kanda tano za Tanzania yaani Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kati, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Kusini na Kanda ya Kaskazini sasa ni zamu ya kanda ya Pwani ambayo inahusisha Mikoa ya Dar Es Salaam, Morogoro na Mkoa wa Pwani kushiriki kwenye shindano la Kwanza na La aina yake ambalo halijawahi kutokea Afrika Mashariki na Kati likiendeshwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited.
Ratiba ya Dar Es Salaam
Ni kuanzia Umri wa Miaka 14 na Kuendelea.
UKUMBI NI MAKUMBUSHO YA TAIFA KARIBU NA CHUO CHA IFM KUANZIA SAA 2 ASUBUHI Kwa Mawasiliano Zaidi Piga  0658 700 400 0687 707  071
Au Tembelea Ukurasa Wetu wa Facebook: http://www.facebook.com/tztmt Instagram: @tmt_tz

MO ATAKA MADHEBEBU DINI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI ILI KULETA MAENDELEO ENDELEVU



DSC_0575
Mbunge wa jimbo la Singida Mjini, Mh. Mohammed Dewji (MO), akizungumza na waumini wa Msikiti wa kijiji cha Mtamaa wakati wa ziara yake ya siku tatu jimbo kwake.
Na Nathaniel Limu, Singida
MBUNGE wa Jimbo la Singida mjini, Mohammed Gulam Dewji amewahimiza waumini wa madhahebu mbalimbali ya dini kuendelea kushirikiana na serikali ili kurahisisha upatikanaji wa maendeleo endelevu.
Mbunge Dewji maarufu kwa jina la MO,ametoa wito huo hivi karibuni kwa nyakati tofauti wakati akikagua ujenzi wa misikiti na makanisa jimboni kwake.
Amesema madhehebu ya dini mbalimbali yana mchango mkubwa sana katika kusukuma gurudumu la maendeleo,kuanzia ngazi ya kaya hadi taifa kwa ujumla.
DSC_0467
Mbunge MO akijumuika na waumini wa Kanisa la FPCT kutoa burudani wakati wa ziara ya MO.
"Mchango wa madhehebu ya dini unasaidia mno kuendeleza amani na utulivu kuanzia ngazi ya kaya,kijiji hadi taifa.Amani na utulivu uliopo hivi sasa ndio unaotusaidia tumwabudu Mungu kwa uhuru na pia kujiletea maendeleo bila vikwazo",amesema.
Dewji amesema ili kuonyesha imani yake kubwa kwa madhehebu ya dini safari hii ameamua kukagua ujenzi wa makanisa na misikiti ya jimboni kwake ili aweze kuyaunga mkono katika ujenzi huo unaoendelea.
"Ninyi ni mashahidi wangu wazuri juu ya maendeleo ya sekta mbalimbali tuliyoyapata jimboni mwetu kwa kushirikiana mimi na ninyi.Baada ya kufanya makubwa kwenye sekta ya elimu,afya,barabara na maji,sasa nimeamua kwa moyo wangu wote kuboresha ustawi wa madhehebu ya dini",amesema.
Akifafanua zaidi, amesema kupitia kwa katibu mkuu wa CCM taifa,anatarajia kukabidhi misaada ya mabati na mifuko ya saruji yenye thamani ya zaidi ya shilingi 127 milioni kwa misikiti 51 na makanisa 30.

CHUO CHA ELITE LEARNING CHA KIJICHI KUDHAMINI TASWA SC



Mkurugenzi Mkuu wa Elite learning institute Co, Hassan Kashoba (Kushoto) akizungumzia udhamini wake kwa Taswa FC na Taswa queens. Kulia ni mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary.
****************************************************
Na Mwandishi wetu, Dar
Dar es Salaam. Chuo bora cha Elite Learning cha Mtoni Kijichi kimeahidi kusaidia timu ya soka na netiboli ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa SC) ili ziweze kusonga mbele katika shughuli zake.
Ahadi hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Elite learning institute Co, Hassan Kashoba baada ya kuvutiwa na jinsi waandishi wa habari wanavyojishughulisha kwa vitendo katika shughuli zao za kila siku.

Kashoba alisema kuwa wao mbali ya kusaidia vifaa vya michezo, pia wametoa ofa kwa waandishi wa habari wa Taswa SC kupata mafunzo ya Information and Communication Technology (Tehama), hotel, ualimu wa shule za awali na kompyuta.
Alisema kuwa wanajua kuwa waandishi wana taaluma ambayo wanaifanyia kazi, lakini katika maisha ya sasa, lazima uwe na elimu ya ziada ambayo itakuwezesha kufanya kazi nyingine mbali ya uandishi wa habari.

“Hii ni fursa kwa waandishi wa habari  wa Taswa SC, tumeona jinsi gani walivyo mstari wa mbele katika michezo, tena kwa kufanya kwa vitendo, sisi kwa vile tumebobea katika elimu, tumewapa ofa hiyo, ni jukumu lao kuikubali au kuikataa,” alisema Kashoba.
Aliongeza kuwa kwa muda wa miaka mitatu sasa, wameweza kutoa elimu bora kwa wanafunzi wengi wao wamepata ajira na kuamua kupanua wigo kwa waandishi.
Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary alikishukuru chuo hicho kwa malengo hayo na kuwaomba watimize ili wachezaji wake waweze kutumia vifaa hivyo kwa michezo na kusomea fani nyingine pia.

NSSF YASHIRIKI MAONESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA-TANGA



 Muuguzi, Elionora Mmasi akiwapima wanachama wa NSFF waliotembelea banda lao wakati wa maonesho ya pili ya kibiashara yanayofanyika mkoani Tanga.
Baadhi ya watu waliofika katika banda la NSSF wakipata maelezo kutoka kwa maofisa wa Shirika hilo kuhusu Fao la Matibabu wakati wa maonesho ya pili wa kibiashara yanayofanyika mkoani Tanga.

MSANII WA BONGO MOVIE RACHEL HAULE AFARIKI DUNIA ASUBUHI HII


Rachel Haule ‘Recho' enzi za uhai wake.
MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Rachel Haule ‘Recho,’ amefariki dunia asubuhi hii akiwa katika Chumba cha wagonjwa wanaohitaji Uangalizi Maalumu ICU.  Taarifa za awali zinasema kuwa Marehemu alijifungua jana Kwa Operesheni lakini Bahati Mbaya Mtoto akafariki na baada ya operesheni hiyo ndipo na yeye hali ikawa mbaya na kupelekwa ICU hadi mauti yalipomfika leo asubuhi.

 MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!

Ubongo Kids: Tanzania's Homegrown Edu-Cartoon Season 1



Ubongo Kids

Ubongo Kids is Tanzania's first homegrown cartoon series, designed to help kids discover the joys of math through fun, local stories and songs. We're turning to Kickstarter to help us adapt our first 13-episode TV season from Kiswahili to English, for broadcast to millions more kids across Africa and web viewers around the world.
Please help us spread the word about Ubongo Kids! Like us on Facebook, follow us on Twitter, and subscribe to our YouTube Channel!
Ubongo is a Tanzanian social enterprise that creates fun, localized edutainment for learners in Africa.  "Ubongo" means brain in Kiswahili, and we're all about finding fun ways to stimulate kids (and kids at heart) to use their brains.  Our entertaining media help learners understand concepts, rather than memorizing them. And we use catchy songs and captivating imagery to make sure they never forget!
Ubongo Kids follows Tanzanian cartoon kids Kibena, Kiduchu and Koba as they use their minds and math skills to solve problems in their village, with the help of their talking and singing animal friends: Mama Ndege (a math whiz bird), Uncle T (a rapping giraffe), and Da Chura (a frog who ribbits important vocab).
We use edutainment to help kids see math in a new light and learn fundamental math concepts through fun, relatable stories-- which we get out to as many learners as possible using widely available technologies. Internet and smartphone penetration is still low in Sub Saharan Africa, but 37.5 million households have TV (Informa Telecoms & Media, 2011), and tens of millions more watch TV in communal screening spaces.  English is an official language in 23 African countries, and adapting Ubongo Kids to English will allow kids from Nigeria to Malawi to learn from Mama Ndege and friends!
We believe that Ubongo Kids is a small but important step towards transforming informal education in Africa.
Test screening in a rural school, Kigoma Region
Test screening in a rural school, Kigoma Region
Watch a webisode with English captions to see it for yourself:
Our core team worked unpaid for 7 months to create the concept of Ubongo Kids and produce the first six episodes. Now, thanks to sponsorship from CRDB Bank in Tanzania, the first season of Ubongo Kids (in Kiswahili) is showing on Tanzanian national TV... and on YouTube as weekly webisodes. We have an SMS-based live interaction system, which allows viewers to answer multiple-choice questions while watching the show, and get feedback and encouraging messages from our cartoon characters.

Sunday, May 25, 2014

VURUGU ZATAWALA KATIKA NGUMI MSHINDI ASHINDWA KUTANGAZWA





Bondia Said Mbelwa kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Karama Nyilawila wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa UBO uliofanyika katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaam hata hivyo mshindi ajapatikana kutokana na fujo zilizotokea katika raundi ya nane picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Zumba Kukwe kushoto akioneshana umwamba na Josef Njelekela wakati wa mpambano wao waliotoka droo picha na  picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Zumba Kukwe kushoto akioneshana umwamba na Josef Njelekela wakati wa mpambano wao waliotoka droo picha na  picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimpongeza khalid chokolaa baada ya kuibuka mshindi katika mpambano wake
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimpongeza khalid chokolaa baada ya kuibuka mshindi katika mpambano wake
Bondia Tasha Mjuaji kushoto akipambana na Rajabu Mahoja wakati wa mpambano wao

Bondia Mada Maugo kushoto akiwa anapigana na Thomas Mahali mwenye rasta
Bondia Mada Maugo akiwa anazipanga kavukavu na bondia Thomas Mashali walipiokutana katika ukumbi wa Frends Corner Manzese picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Na Mwandishi Wetu

MPAMBANO wa ubingwa wa UBO umekosa kutangazwa mshindi mbele ya mashabiki baada ya vurugu kubwa kutokea katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita

ubingwa huo uliokuwa ukigombaniwa na mabondia Said Mbelwa na Karama Nyilawila alishindikana kupatikana mshindi baada ya raundi ya nane bondia Karama kumpiga kichwa Mbelwa cha wazawazi na kusababisha Mbelwa kuamaki kwa kulipiza kisasi na kumsukuma nje pia kumrukia kama ninja wakati alipotoka nje ya uwanja mpambano huo wa raundi kumi ulijikuta ukishia kwa raundi nane

na refarii pamoja na majaji wake kukimbia ukumbini wakiwaacha mashabiki bila kureta majibu ya mpambano huo hata hivyo mbelwa alirudi uringoni kwa ajili ya kuenderea kupambana na mpinzani waka alikimbia moja kwa moja kutokana na kuona kihama cha ngumi za mtaani zilivyuoanza

wakati huohuo bondia Mada Maugo alimpiga mwenzake Thomas Mashali kwa ngumi tatu mfululizo kavuvu 
bila kufata sheria ambapo ni kinyume na taratibu za mchezo wa masumbwi duniani kote mabondia hawo ambao wote walionekana wamelewa walipishana kiswahili mbele ya promota Ally Mwazoa ambaye ame haidi kabla ya kumaliza mwaka mabondia hawo wawe wameshapanda uringoni 
ambapo mpambano wao wa kwanza Thomas Mashali alimgalagaza kwa point Mada Maugo
katika mapambano ya utangulizi yaliyochezwa siku hiyo bondia Khalid Chokoraa ambaye ni mwanamuziki alimpiga kwa k,o ya raundi ya kwanza  Abdul Manyenza na Mwaite juma alimpiga Athumani Rashid wa Tanga kwa point wakati Selemani Galile alipigwa kwa point na Abdalah Pazi