Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (katikati) akifungua
semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa
Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti
Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Mstaafu
wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi akifungua semina ya
majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na
wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa
Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Salome
Suzete Kaganda (kwanza kushoto) akizungumza kwenye semina ya majadiliano
kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari
waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa
Viongozi wa umma.
Baadhi ya washiriki katika semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti
ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya
Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.

Katibu Msaidizi Kanda ya Mashariki, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi
wa Umma, Getrude Cyriacus (wa kwanza kushoto) akiwasilisha mada juu ya
Rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa
umma kwa wanasemina.
Baadhi ya washiriki katika semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti
ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya
Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Na Joachim Mushi, Dar
RAIS
Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi amesema bado viongozi
wa umma wanatumia madaraka yao na Ofisi zao kwa kujinufaisha wenyewe na
kuwasahau wananchi waliowaweka madarakani hivyo kuna kila sababu ya
kuleta sheria ya kuziba mianya hiyo kwa viongozi wanaokwenda kinyume na
maadili.
Alhaj
Mwinyi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua
semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa
Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti
Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Alisema
licha ya kuwepo kwa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995
inayotumika sasa bado kumekuwa na wimbi kubwa la mienendo ya matumizi
mabaya ya ofisi na madaraka kwa viongozi wa umma kwa kujinufaisha
wenyewe kimaslahi.
"...Maana
yake ni kwamba umma sasa haupewi kipaumbele unavyo stahiki. Maamuzi ya
viongozi yanatolewa kwa maslahi binafsi na hivyo kudhihirisha kuwepo kwa
tatizo la mgongano wa maslahi. Viongozi hao waliopewa dhamana na
wananchi wanatumia rasilimali za umma ili kujinufaisha binafsi au
shughuli zao ambazo wanazo pembeni," alisema Rais huyo mstaafu.
Alisema
hata hivyo sheria ya maadili ya viongozi wa umma imekuwa na mapungufu
kwa kuwabana baadhi ya viongozi wa umma na kuwaacha wengine pamoja na
watumishi wa umma hivyo kujikuta nao wakijihusisha na mgongano wa
kimaslahi.
Hata
hivyo, ameongeza kuwa tayari Serikali imeona mianya hiyo na hivyo kuanza
mchakato wa kuja na sheria maalum itakayo dhibiti hali hiyo.
"...Nadhani mmewahi kusikia mara kwa mara namna ambavyo Rais wetu
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiagiza Serikali kufanya jitihada za
dhati ili kuhakikisha kuwa viongozi wa umma wanaacha au wanajiepusha na
tabia ya kushiriki zaidi kwenye biashara na kuacha jukumu lao...,"
alifafanua Mwinyi akiwaeleza washiriki wa semina hiyo.
Aidha
aliipongeza Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kuanza
mchakato wa kutungwa kwa sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi
kwa Viongozi wa umma, ambapo itakapo kamilika huenda ikawa suluhisho la
mgongano wa kimaslahi kwa viongozi na watumishi wa umma.
Rais
huyo mstaafu aliwataka wanasemina kuijadili rasimu iliyowasilishwa na
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na kutoa maoni yao
kuiboresha zaidi ili itoke na majibu ya kero ya muda mrefu ya Mgongano
wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Kwa
upande wake, Katibu Msaidizi Kanda ya Mashariki, Sekretarieti ya Maadili
ya Viongozi wa Umma, Getrude Cyriacus akiwasilisha mada juu ya Rasimu
ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma kwa
wanasemina kabla ya mjadala alisema wataalam wa Sekretarieti hiyo
wamefanya utafiti kwenye mataifa mbalimbali na kutoka na mapendekezo
ambayo yataongoza mjadala kuelekea kupata sheria nzuri.
Naye
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Salome
Suzete Kaganda akizungumza katika semina hiyo, alisema Rasimu ya Sheria
Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma walioiandaa
itajadiliwa na wadau mbalimbali ili kupata maoni kabla ya kuwasilishwa
kwenye baraza la makatibu wakuu kuboreshwa zaidi kabla ya mchakato
kupanda ngazi za juu.
Aidha
aliwataka wananchi na wadau wengine kuendelea kuijadili Rasimu ya Sheria
Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma pindi
itakapo wafikia na kutoa maoni kwa lengo la kuiboresha zaidi ili itakapo
kamilika iweze kufanya kazi vizuri na kujibu kero zilizopo katika eneo
hilo la viongozi wa umma.
“...Mapendekezo
ya sheria hii hayalengi kuwafanya viongozi kuwa maskini, bali kasi yao
ya ukwasi iendane na hali halisi ya kipato chao. Sheria hii
itakapopitishwa itapunguza ubinafsi wa viongozi walioko madarakani
kujipendelea wenyewe na maeneo wanayotoka.” Alifafanua Jaji Kaganda.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com