Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, October 11, 2009

MTV AFRICA MUSIC AWARDS 2009 - LIVE

Huyu ni Wycleff Jean akiwa amevua shati akifanya makamuzi katika MTV AFRICA MUSIC AWARDS 2009 tamasha lililodhaminiwa na ZAINSasa hapa Akon na Wycleff Jean sijui walikuwa wanashindana kuvua nguo? lakini ilikuwa ni mizuka ya Show BabkubwaEbwana Jamaa alifunika ile mbayaKama vile anaimba GheeeeeeeetoEbwana amini usiamini jamaa alikuwa anatembea katika vichwa vya watu huku akiimbaHuyu ni Msenegal aliyelowea Marekani akikamua vilivyoWycleff akkiwa na sare ua NyumbaniAkon uzalendo ulimsinda na kuamua kuvamia steji na kuimba na WycleffWanamuziki wa Bongo Manaona wanamuziki wa Mbele, jamani jifunzeni kutumia vifaa
Wycleff AKiimba na kupiga ngomaWycleff Jean akiimba na kupiga GitaaShoo ilikuwa Show kweli usifanye MasiharaHapa wasanii wote waalikwa wakiimba wimbo wa "WE ARE THE ONE" wa Michael Jackson ikiwa ni sehemu ya kutoa heshima kwa mkali huyo wa POP Duniani, Huyu alikuwa ni mtoto wa Lacky Dube akimuwakilisha Baba yakeEbwana Siunajua tena wasanii wakishajua Akon na Wycliff wapo ndani, ilikuwa ni full kubanjukaNameless akiteta na fans wake baada ya kuchukua TuzoBlue 3 kaziniEbwana Blue 3 nao si mchezo, waliwakilisha UgandaWatu Shemejiiiiiiimwanamuziki wa Kenya Amani akiwajibikaEbwana Brother katika majukwaa ya kimataifa huwa hafanyi makosaMzee wa Komesho anakamuaHuyu ni Wahu akifanya vitu vyake StejiniUkumbini mambo yalianza hiviAkon Akila pozi kwa ajili ya pichaAkon akipiga InterviewHuyu ni Akon aki Holla na Fans wakeNameless na wife wake Wahu wakitinga ukumbini kwa poziEbwana ingekuwa Arusha Ungesikia.. Chalii yangu amekuja na tororooHapa Wycleff anapiga interviewMkali toka New Jersey Wyclef Jean akitinga ukumbini kwa MbwembweShaa aki Holla na fan wakeShaa akihojiwa na moja ya Radio zilizokuwa zikirusha LiveHuyu anayecheka ni Shaa akihojiwa kulikoni amevaa nguo inayofanan na msaa wa Blue 3 wa UgandaDe` Banji toka Nigeria nao wakipiga interview kabla ya kuzama ukumbiniMkali wa Twister toka Uganda Navio naye akivuta hatua katika Red CapetMzee wa Comarcial akifanya interviw na media za KenyaEbwana AY mtoto huyoo naona anataka kumhugHuyu ni AY moja ya Nominees katika tuzu aki Holla na fans wakehapo vipi..? Hapo Sawa...Huyu ni Profesa Jay wa Mitulinga kama mamtoni mwanangu ana Halla na mashabiki katika Red Capet kabla ya kutinga ndaniHaya kina nanii si masista Duu ni wasanii jamaniVanessa Bernad alikuwa anaona kama ndoto vile na gauni lake jekundu ndaniHawa ni mashabiki wakisubiri kuwalaki wasanii langoni
watu weeeweeeeeeeeeeeHali ilivyokuwa nje ya uwanja mashabiki wakianza kuingia, Totozi zilikuwa za kwamwaga yaani ilikuwa kama Ulaya vileSwala la ulinzi na usalama wenzetu wanajali kuliko jambo lolote wa Tanzania mmeona?Hali ilivyokuwa uwanjani kabla ya shughuli yenyewe kuanzaHii ni Kenya mdau akielekea kunako tamashaOfisa Uhusiano na Mawasliano wa kampuni ya Zain Bi.Celin Njuju Chungu (kulia) na mratibu wa masoko maeneo ya mijini Ellen Lupilli, mshindi wa wa shindano la tuzo za muziki kutoka Tanzania Vanessa Bernad na mwanahabari Babra Hassan wakiwasili nchini Kenya...
Mpiga picha wa viwanjani.blogspot.com pamoja na magazeti ya Majira, Dar Leo na Spoti Starehe akitinga ndani ya Kenya Airways tayari kwa kufuatilia kinachoendelea katika tamasha la MTV AFRICA MUSIC AWARDS 2009

Saturday, October 10, 2009

SERIKALI YA KENYA KUGHARAMIA SAFARI YA TIMU YA TAIFA YA TAEKWONDO

Hatimaye Serikali ya Kenya ameamua kusaidia timu ya taifa ya taekwondo katika michuano ya 21 ya Dunia huku chama cha mchezo huo nchini Kenya kilia na ukata.
Katibu mkuu wa chama hicho George Wesonga ameishutumu kamati ya IOlimpiki ya Kenya na kocha wa zamani kwa kutumia vibaya tiketi za wachezaji kwa kuchukua viongozi wengi kuelekea Denmark.
Amebainisha kwamba wamelazimika kuwaacha Mohamud Ali ambaye alitwa medali ya fedha mwaka 2007 katika michuano ya Dunia pamoja na Yahya Mohamed.
Wesonga sasa amemtaka waziri wa michezo wa Kenya Prof. Hellen Sambili kuingilia kati swala hilo na kuwapa nafasi wachezaji zaidi.
Timu ya taifa ya Kenya ya mchezo huo inatarajiwa kuondoka siku ya Jumanne wiki ijayo ikiwa ni siku moja kabla ya michuano hiyo kuanza.

WANJIRU YUKO TAYARI KWA CHICAGO MARATHON

Mkenya Samuel Wanjiru, ambaye alishinda katika michezo ya Olimpiki ya Beijing katika marathon mwaka jana, anatarajiwa kukutana na mpinzani mkubwa katika michuano ya Marathon itakayofanyika Chicago Jumapili hii.
Wanjiru, ambaye mwezi ujao anatimiza miaka 23, amepania kuvunja rekodi ya Dunia ya mwanariadha wa Ethiopia Haile Gebrselassie ya kukimbia saa mbili, dakika tatu na sekunde 59 mwaka jana jijini Berlin.
Lakini pia atakuwa amevunja rekodi yake ya muda mzuri wa saa 2:05.10 ambao uliuweka mwezi April jijini London.
Matokeo mazuri aliyapata katika michuano ya majira ya joto mwaka 2008 ambapo alikimbia huku hali ya hewa ikiwa ni ya joto la juu na kufanikiwa kutwaa medali ya dhahabu katika Olimpiki kwa kukimbia kwa saa 2:06.32, akiwa chini ya rekodi ya Dunia kwa dakika tatu.
Katika michuano minne aliyoshiriki ameshinda mara tatu na kushika nafasi ya pili.Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Wanjiru kuzuru nchini Marekani huku akitaraji kuchuana na wanariadha bora kumi toka Afrika, ikijumuisha wanariadha saba toka nchini Kenya, wa Morocco wawili na mmoja toka Ethiopia.
kwa upande wa Wanaume itajumuisha Abderrahim Goumri wa Morocco na Vincent Kipruto wa Kenya.

HARAMBEE STARS KUKIPIGA NA TUNISIA

Timu ya taifa ya soka ya Kenya Harambee stars Jumapili itashuka dimbani kucheza na timu ya taifa ya Tunisia maarufu Carthage Eagles katika mchezo wa kusaka nafasi ya kufuzu kucheza fainali za kombe la Dunia 2010.
Kikosi hicho kitashuka uwanjani bila ya mshambuliaji wake wa kimataifa wa anayecheza soka la kulipwa nchini Ufarnsa katika klabu ya Auxxere Dennis Oliech na Macdonald Mariga.
wakati huo huo, mshambuliaji wa kimataifa wa Tunisia Lassad Nouioui amesema Carthage Eagles wamefanya maandalizi mazuri na wanaamini wataibuka na ushindi.
Kwingineko, kikosi cha Super Eagles cha Nigeria kimerejea mjini Abuja katika uwanja wa taifa kucheza na Msumbiji ikiwa ni mwezi mmoja baada ya kushindwa kuwafunga vinara wa kundi la 2 Tunisia katika uwanja huo.
Uwanja wa Abuja wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 60,000 umetajwa pengine usiweze kujaa, kama ilivyokuwa katika mchezo dhidi ya Kenya na Tunisia.
Msumbiji wanarekodi ya kupoteza michezo miwli mfulululizo dhidi ya Tunisia na Kenya wakicheza ugenini.
Mchezo wa mwisho kushinda ni baada kuichapa Kenya 2-1 huku mfungaji akiwa Tico Tico walipocheza Maputo mwezi uliyopita na kupanda hadi nafasi ya tatu wakkiwa mbele dhidi ya wapinzani wao Kenya.

Friday, October 9, 2009

SIMBA YAPINGA UPOTEVU WA FEDHA ZA PUSH MOBILE

Klabu ya Wekundu wa Msimbazi Simba imepinga vikali tuhumu zinazowakabili viongozi wa timu hiyo juu ya uchukuaji wa fedha wa kiasi cha shilingi milioni tatu kinyemela kutoka kampuni ya Push Mobile iliyopo hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za timu hiyo Afisa habari wa Simba Cliford Mario Ndimbo amesema tuhuma hizo si za kweli isipokuwa anachokijua ni utaratibu wa kuchukua fedha kila baada ya miezi mitatu kama mkataba waliokubaliana na kampuni hiyo na huwa na watiaji saini wanne ambao ni Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Mwahazini wawili.

ZAIN YAZINDUA SHINDA NA ZAP

Meneja Huduma za Zap wa Kampuni ya Zain Tanzania Bw. Deogratias Tarimo,(kushoto)Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Bw.Costantine Magavilla na Meneja Huduma za Jamii Bi.Tunu Kavishe wakiwa wameshikilia kipeperushi kuashiria uzinduzi wa Promosheni Mpya ya 'Shinda na Zap' itakayofanyika kila Ijumaa.(Picha na Rajabu Mhamila)
Na Rajabu Mhamila
Kampuni ya Zainyazindua promosheni Mpya ya Shinda na Zap ambapo wateja wa kampuni hiyo wataewndelea kupata punguzo la asilimia 5 kwa kulipia huduma mbalimbali
Akizungumza na wahandishi wa habari makao makuu ya kampuni hiyo Kijitonyama Dar es salaam Meneja Masoko wa Kampuni ya Zain Tanzania Bwana Costantine Magavilla amesema kuwa Shinda na zAP imezinduliwa leo rasmi ambapo wateja wa Zain wataenderea kutuma,kupokea na kulipia huduma mbalimbali na kushinda.
Shinda na Zap ni promosheni mpya itakayowezesha wateja wa zain wanaotumia huduma ya zap kuweza kujishindia shilingi laki moja kila Ijumaa.
Ambapo wataendelea kuwazawadia wateja kwa huduma wanazozitumia ambapo huduma ya zain zap imekluwa na mafanikio makubwa kuanzia walipoizindua. na wanahamini wateja wao wana haki ya mtandao bora wenye uwigo mkubwa na huduma za kisasa zinazoweza kutumika popote siku na masaa yote.Ambapo mwaka jana walishughudia hudhinduzi wa hyduma yetu ya kuwazawadia wateja ijulikanayo kama Rewardz au zawadi kwa pesa wateja wetu wanazitumia katika simu zao
Na leo tunatoa sababu nyingine ya watanzania ya kuchagua kuenderea kutumia huduma za Zain kwa kukidhi maitaji yao ya mawasiliano Shinda na Zap itawawezesha wateja wa zain kuzawadiwa kwa kutumia huduma ya malipo kwa njia ya simu Zap
Ukiwa unatumia uduma za Zain ni sawa kuwa na pesa mkononi mwako wakati wowote alisema Magavilla jinsi ya kutumia huduma hii ni raisi sana na unachotakiwa kufanya ni kujiunga na huduma ya zap ambayo itakuwezesha
kutuma na kupokea fedha kutoka mtandao wowote nchini Tanzania kununuwa muda wa mahongezi na kutuma kwa mtu mwingine kulipia bili ya maji kulipia bili ya umeme Luku na kwa kila ijumaa kutakuwa na droo ambapo mteja mmoja atajishindia shilingi laki moja itakayoingizwa moja kwa moja kwenye akaunti yake ya Zap
huduma ya zap ilianzishwa mwanzoni kabisa mwa mwaka uhu na leo hii huduma hii ni huduma iliyo bora kabisa katika sekta ya mawasiliano

Thursday, October 8, 2009

TID KUZINDUA SAUTI YA JELA JUMAPILI CLUB BILICANAS

NATAFUTA PEEEEEESA, EEEEEEEEH ASHAA...
JAMANI TUKAMUUNGE MKONO TID KATIKA UZINDUZI WA SAUTI YA JELA (PRISON VOICE)
Msanii wa muziki wa kizazi Kipya Khalid Mohammed TID akiimba mbele ya waandishi wa habari wakati akizungumzia uzinduzi wa albamu yake mpya ya SAUTI YA JELA (PRISON VOICE) uzinduzi ambao utafanyika siku ya Jumapili katika ukumbi wa klabu Bilicanas jijini Dar es Salaam, kushoto ni meneja masoko wa klabu hiyo Antoni KizitoMsanii Khalid Mohamed 'tid' akiangali blog ya viwanjani wakati alipotambulisha uzinduzi wa albamu yake ambao utafanyika jumapili katika clabu ya bilicanas jijini Dar es salaam.(Picha na Rajabu Mhamila super D Mnyamwezi)

MSHINDI BSS KULAMBA MILIONI 25

Wasanii walioingia katika fainali za Bongo Star Seach zinazozaminiwa na kampuni ya Vodacom pamoja na Kampuni ya bia Tanzania (TBL) wakiimba wakati wa utambulisho wa zawadi Dar es salaam jana kutoka kushoto ni Beatrice William,Jackson George,Pascal Castan na Kelvin Mbati.(Picha na Rajabu Mhamila)
ZAWADI za mshindi wa Bongo Star Search mwaka 2009 zimetangazwa leo ambapo mshindi wa kwanza atalipwa kiasi cha shilingi milioni 25, wa pili shilingi milioni 5 wa tatu milioni tatu na nusu, wa nne milion moja na nusu nwa tano milioni moja.
Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa shindano hilo Madam Ritha Paulsen amesema, fainali za mpambano huo zitafanyika usiku wa mkesha wa kumbukumbu ya siku naliyokfa baba wa Taifa mwl Julius Kambarage Nyerere katika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam.Amesema fainal hizo zitapambwa na wasanii mahiri kama Shaa, FeisalIsmail, Baby Madaha Abubakar Mzur na wasanii wengine wengi wa nyumbani.
Madam Ritha amewataka wapenzi wa BSS kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili waweze kushuhdia nani anakuwa mshindi na kujinyakulia pesa hizo ambazo zinaweza kuyakomboa maisha yake kama atakuwa na malengo mazuri.
Mpambano huo wa kumsaka mshindi wa Bss mwaka 2009 ulianza na wasanii 15,000 kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania ambapo mpaka sasa katika fainali wamebakia Pascal Casian kutoka Mwanza, Peter msechu wa Kigoma, Jackson George wa Tanga pamoja na Kelvin Mbati anayewakilisha Jiji la Dar es Salaam.

Story writen by Adam Hussein.

UWAMADA WAKUTANA NA MKURUGENZI

Mkurungenzi wa Manspaa ya Ilala Bw.Gabeuz Fuime (kulia) akioneshwa moja ya barua za wanachama cha Umoja wa wauza samaki Dar es salaam UWAMADA na Katibu wa soko la feri Bi. Elifrida Mwambu 'mama kasanda' alipofanya kikao na wauzaji hawo wa samaki leo katikati ni Alhaji Makamba.(PIcha na Rajabu Mhamila super D Mnyamwezi)

MATIMBWA ACHUKUA FOMU

Mgombea nafasi ya Mwenyekiti wa Serekali ya mtaa wa Gerezani Magharibi Bw.Ramadhani Matibwa (kushoto) akirudisha fomu ya kugombea kwa Msimamizi msaidizi wa uchaguzi wa serekali ya mtaa uho Bw. Felex Nyange.(Picha na Rajabu Mhamila)

Wednesday, October 7, 2009

YANGA YAZIMA NGEBE ZA TOTO - LIGI KUU TZ

Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Yanga wameendeleza wimbi la ushindi kwa timu za mikoa ya Kanda ya Ziwa baada ya kuichapa leo Toto African ya Mwanza bao 1-0 katika mchezo uliyochezwa katika uwanja wa CCM KIRUMBA jijini Mwanza.
Goli pekee la ushindi lilifungwa na mchezaji Mrisho Khalfani Ngasa katika kipindi cha kwanza baada ya kuunganisha kona iliyopigwa na Abdi Kasim.
Kufuatia ushindi huo sasa Yanga inafikisha jumla ya Pointi 14 na kushika nafasi ya pili ikiwa nyuma ya vinara wa ligi kuu ya Tanzania Bara Simba ambayo inajumla ya pointi 18.
Kwa mujibu wa Msemaji wa klabu ya Yanga Luis Sendeu amesema kikosi cha Yanga kitaondoka kesho Jijini Mwanza kuelekea Shinyanga ambapo itacheza michezo mitatu ya kirafiki katika uwanja wa Kambarage na uwanja wa Kahama, kisha itatua mkoani Singida kucheza mchezo mmoja wa kirafiki na Singida United.
Michezo mingine iliyochezwa leo katika ligi kuu Tanzania bara ni pamoja na Kagera Suger ambayo imetoka sare ya bila kufungana na Maji maji katika uwanja wa Kaitaba, Kagera.Wakati Moro United imefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya JKT Ruvu.
Wafungaji wa Moro United ni Yona Ndabila aliyefunga goli la kwanza dakika ya 10 baada ya kuunganisha mpira wa kona uliyopigwa na Hussein Swedi, na goli la pili lilipatikana katika dakika ya 34 likifungwa na mchezaji Saidi Ahmed.
Goli la kufutia machozi la JKT Ruvu lilifungwa na Hussein Bunu katika dakika ya 45 akiunganisha krosi iliyopigwa na Sostenesi Manyasi.

HAPPYBIRTHDAY PRESDENT OF REPUBLIC OF TANZANIA JAKAYA MRISHO KIKWETE!

Raisi Jakaya Mrisho Kikwete alizaliwa tarehe 07 Octoba, 1950 katika kijiji cha Msoga Mkoani Pwani. Ni mtoto wa sita kuzaliwa katika familia ya watoto tisa ya mzee Khalfani Mrisho Kikwete (BABA) na Asha Jakaya (MAMA).

MWENYEZI MUNGU AKUJALIE AFYA NJEMA, KHERI NA FANAKA SIKU ZOTE!

HAPPYBIRTHDAY PRESDENT OF REPUBLIC OF TANZANIA JAKAYA MRISHO KIKWETE!