Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, December 6, 2013

MOJA YA BASI LIENDALO KASI LATUA JIJINI DAR TAYARI KWA MAJARIBIO YA BARABARA YA MABASI YAENDAYO KASI




Mabasi ya mwendo kasi 2014 kimara kivukoni.  Picha kwa hisani ya Deo Mutta Mwanatanga
Basi la kwanza la mradi wa mabasi yaendayo kasi limewasili nchini na kuanza kufanya majaribio katika barabara zilizokwisha kamilika huku mengine yakitarajiwa kuwasili mapema mwaka kesho.

Mtendaji mkuu wakala wa mradi wa mabasi yaendayo kasi Bi Asteria lambo amesema basi hilo ni miongoni mwa mabasi madogo yatakayoingia nchini yenye uwezo wa kubeba zaidi ya abiria 40 na makubwa yatabeba abiria zaidi ya 150 na kuwataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuendelea kuwa na subira na kuwahakikishia mradi huo sio ndoto na adha ya usafiri itapungua mapema mwaka kesho.

Nao baadhi ya wakazi wa jiji walioshuhudia gari hilo wameelezea kufurahishwa na kuanza kuwa na imani na serikali yao ambapo wamesema kama mradi huo utakamilika kwa muda uliopangwa utakuwa faraja sana kutokana na adha kubwa ya usafiri wanayokumbana nayo  huku wakitoa wito kwa mamlaka husika kupanga mikakati ya kupunguza nauli za mabasi hayo pindi yatakapoanza kufanya safari zao.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA KIFO CHA MZEE MANDERA




 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandera, aliyefariki usiku wa kuamkia leo wakati alipofika kwenye Ofisi za Ubalozi wa Afrika ya Kusini zilizopo Masaki  jijini Dar es salaam leo. Mzee Nelson Mandela (95) alifariki Dunia jana usiku nyumbani kwake Houghton, Jouhannesburg. Kushoto ni Balozi wa Afrika ya Kusini Nchini, Henry Thanduyise Chilize.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya picha ya marehemu Nelson Mandera baada ya kusaini kitabu cha maombolezo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Afrika ya Kusini Nchini Tanzania, Henry Thanduyise Chiliza (kulia) na baadhi ya Viongozi wa Ubalozi huo kwenye ofisi za Ubalozi wa Afrika ya kusini Masaki jijini Dar es salaam leo, baada ya kusaini kitabu cha maombolezo.

MAKAMU WA RAIS AKABIDHI TUZO ZA MUAJIRI BORA WA MWAKA 2013 JIJINI DAR

 


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya Muajiri Bora wa mwaka 2013, Meneja Rasilimali Watu wa Benki ya NMB, Rashid Nassoro, wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo hizo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempisky jijini Dar es Salaam, jana usiku.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya Muajiri Bora wa mwaka 2013, Meneja wa Sera wa CCBRT, Frederick Msigala, wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo hizo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempisky jijini Dar es Salaam, jana usiku. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya Muajiri Bora wa mwaka 2013, Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Francis Ndenje, wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo hizo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempisky jijini Dar es Salaam, jana usiku.
 Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya jumla ya Muajiri Bora wa mwaka 2013, Meneja Uhusiano wa Nje wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, Salum Mwalimu wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo hizo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempisky jijini Dar es Salaam, jana usiku.
 Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.
 Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.

Thursday, December 5, 2013

BONDIA KING CLASS MAWE KUZIDUNDA NA KASHINDE DESEMBA 31 MSASANI KLABU


Na Mwandishi Wetu

BONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' ameingia kambini kwa ajili ya mpambano wake utakaofanyika desemba 31 siku ya kufunga mwaka katika ukumbi wa msasani klabu ambapo atatupiana makonde na Mohamed Kashinde katika mpambano wa raundi sita siku hiyo

akizungumza na waandishi wa habari kocha wa kimatafa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'  amesema kuwa king class kesha ingia kambini kwa ajili ya mpambano uho wa kufunga mwaka kwani ndio itakuwa mpambano wa mwisho kabisa kwa mwaka uhu

bondia king class mawe yupo fiti na ana juhudi binafsi ya kujituma mazoezini ndio siri ya mafanikio aliyo nayo mpaka sasa na kuweza kuwachachafya mabondia mbalimbali nchini ikumbukwe kuwa class ni bondia chipkizi lakina amesha wachakaza mabondia wakongwe kama Amosi Mwamakula,Simba Watunduru na Said Mundi wa Tanga na Patrick Kavako wa Morogoro ambao wote hawo kawachakaza kwa vipindi tofauti hivyo Kashinde ajiandaee sana

kwa ajili ya kupambana na King Class Mawe

Katika mchezo huo kutakuwa na michezo mingine ambapo bondia Iddy Mnyeke ataoneshana ubabe na Cosmasi Cheka,Antony Mathias akizipiga na Fadhili Majiha katika mchezo mwingine ni kati ya Fransic Miyeyusho wa Tanzania akizichapa na David Chalanga kutoka Kenya

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Floyd Mayweathar,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo huo vitakaokuwa vikitolewa na Super D kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha ngumi

SMILE YATOA ‘ZAWADI YA KASI’



 
Mkurugenzi Smile Tanzania na Uganda Fiona McGloin ( katikati) Kushoto Deo Ndejembi Mkuu wa Mauzo na Madaha Fancis Mkuu wa Mtandau (Kulia)  wakizindua Smile 4G LTE broadband jijini Arusha
Hon Makamba kwenye uzinduzi ya Smile 4G LTE jijini Arusha akiwa na mkurugenzi wa Smile Tanzania na Uganda Fiona McGloin

For Immediate Release
DAR - ES- SALAAM 5Desemba, 2013
Katikakusherekeamwishowamwaka, Smile inafurahakuwatangaziapromosheniya ‘ZawadiyaKasi’, promosheniambayobiasharanawatubinafsiwatawezakununua “Mi-FI” ya Smile, kifaa cha kurushaintanetichenyematumizimengi, saiziyamfukoninakinachotumiabetriiliyojengewandani, kinachokujanakifurushi cha intaneti cha bure cha kuanzia.
MkuuwaMauzoyamojakwamojawa Smile, DeogratiusNdejembi, alisema “TunazinduapromosheniyaMi-Fi ambayoitadumukwamiezimiwili, kwanamnahiiwatuwengizaidiwatawezakufurahiaintanetiya Smile yenyekasizaidikatikamsimuhuuwasikukuukwabeinafuu.
“Biasharanyingi, marafikinafamiliasiotukwambawanahitajikutumiaintanetibalipiawanazidikutegemeaupatikanajiwaintanetiyenyeuboranakasizaidikatikashughulizao. Ili kuwasaidiawatuhawa, tunatoavifaavyetuvyakurushiaintanetivyaMi-FikatikabeiyapromosheniyaTsh 149,000 tu.Piatutawekakifurushi cha GB 5 kwenyekifaahicho,” aliongezaBw. Ndejembi.
Kifaahichochenyeuzitomdogonaukubwasawanasimundogoyamkononihufanyakazikama modem napiaMi-Fi inawezakuunganishampakavifaa 8 kwenyeintanetikwawakatimmoja; vifaahivivinawezakuwa tablet, komputampakato, simuzamkononinavifaavinginevyenyeuwezowakuunganishaintaneti.
"KwakutumiaMi-Fi watumiajiwanawezakuchangiaintanetiyenyekasiya Smile 4GLTE wakiwaofisini, nyumbani au wakiwanjiani. Masaayamawasilianobilayabugudhasasayanawezekanakwakutumia Smile Mi-Fi, ambayoinabetriinayokaamudamrefumpakamasaa 8 yamatumiziyakawaidayaintaneti" alisemaBw.Ndejembi.
Smile Mi-Fi inamuundowakuvutianawakisasa. Kioochakekinaruhusumtumiajikuonakwaurahisihaliyamawasiliano, matumiziyakifurushi, nguvuyamawasiliano, kalendanamuda. Kutumiakifaahikinirahisi, “chomekanatumia” (Plug and Play), nahakihitajikuwana program yoyoteilikiwezekufanyakazi.
"Tuna furahakubwakutangazapromoshenihii, nakutoanafasikwaWatanzaniazaidikujioneakasinaufanisiwamtandaowetuambaounaendasambambanamitandaoyenyekasidunianiilikuendananamahitajiyanayobadilikayajamiiyaWatanzania” alisema Fiona McGloin, Menejawa Smile Tanzania na Uganda.
------ MWISHO ---------
KUHUSU SMILE COMMUNICATIONS TANZANIA
Smile Communications Tanzania nisehemuya Smile Telecoms Holdings Limited (Smile), ambayoilianzishwamwaka 2007 nchini Mauritius. Smile Telecoms Holding inafanyabiasharanchini Tanzania, Uganda, JamhuriyaKidemokrasiayaKongo (DRC) Nigeria naAfrikaKusini. Katikamasokoyakeyote, Smile imekuwamuanzilishikatikakutumiateknolojiazakisasa, kama vile 4GLTE ilikuongezakasiyaupatikanajiwaintanetinakujipenyezakatikasoko.
Witonamalengoya Smile nikutoahudumazamawasilianozilizo bora, rahisikutumianazagharamanafuukwakilamtukatikabara la Afrika, kwakutumiaubunifuwakibiasharanateknolojiazakisasazenyegharamanafuu.
Kwamaswaliyavyombovyahabari:
MuffadalEssaji
Head of Marketing, Smile Communications Tanzania
Barua-pepe: muffadal.essaji@smilecoms.com  
Tel: + 255 (0) 758 811164
TovutiyaSmile: www.smile.co.tz
https://twitter.com/SmileComsTZ

KUTOKA KWENYE VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA



Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid (kushoto) na Mbunge wa Mkanyageni, Mohamed Habib Mnyaa,kabla ya kuanza kwa kikao cha Bunge mjini Dodoma Desemba 5, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wabunge kabla ya kipinda cha maswali kjwa Waziri Mkuu, Bungeni mjini Dodoma Desemba 5, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijibu maswali Bungeni Mjini Dodoma Desemba 5, 2013.
Mbunge wa Viti Maalum, Martha Mlata (kushoto) akizungumza na Mbunge wa Nkenge, Asumta Mshama kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Desemba 5, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr. Fenella Mukangara kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Desemba 5, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu (kushoto) na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid, kwenye jengo a Utawala la Bunge Mjini Dodoma December 5, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma, Desemba 5, 2013.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KAPUMZIKE KWA AMANI TATA MADIBA


Na. M. M. Mwanakijiji .

Mpigania haki za weusi na alama kuu ya udhalimu wa mfumo wa Ubaguzi wa Rangi nchini Afrika ya Kusini Mzee Nelson ‘Madiba’ Mandela amefariki dunia baada yakuugua kwa muda mrefu kufuatia maambukizi ya mapafu kushindwa kutengemaa kwa muda sasa. Mzee Mandela ambaye kwa miezi kadhaa sasa amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya maambukizi kwenye mapafu yake amefariki dunia nyumbani kwake ambako alipelekewa toka hospitali ya Moyo ya Mediclinic mjini Pretoria, chini Afrika ya Kusini baada ya familia yake kuomba kufanya hivyo. 

Mzee Mandela alipelekwa hospitali hiyo Jumamosi ya tarehe 8 Juni ikiwa ni baada ya kuanza tena kusumbuliwa na mapafu; miaka ya themanini akiwa kifungoni Mandela alipata ugonjwa wa Kifua Kifuu (TB) kutokana na kazi ngumu ya kupasua mawe kama sehemu ya adhabu ya kifungo chake. Aliondoka hospitali hapo Septemba 1, 2012 baada ya familia kuomba hivyo na kuahidiwa huduma nzuri ya kitabibu nyumbani. Wakati anaondoka hospitali hali yake bado ilikuwa ya utulivu kidogo lakini isiyo na mabadiliko makubwa. Mipango ya mazishi ambayo inatarajiwa kuvuta maelfu ya watu na mamia ya viongozi wa kimataifa inatarajiwa kutangazwa punde.


Mandela akiwa na Walter Sisulu gerezeni Kisiwa cha Robben.

Bw. Mandela (95) alikuwa Rais wa kwanza mweusi wa Afrika ya Kusini kufuatia kutokomezwa kwa utawala wa ubaguzi wa rangi uliofanywa na Makaburu kwa karibu miaka 400 ambapo watu weupe walijipa haki ya kuwatawala na kuwabagua watu weusi. Kabla ya kuwa Rais wa Afrika ya Kusini Mzee Mandela alitumikia kifungo cha miaka 27 jela ambako pamoja na kazi ngumu aliendelea kuongoza kundi la wapigania haki wengine kudai usawa, utu, na umoja wa Waafrika ya Kusini. Mandela alikuwa ni mfungwa maarufu zaidi wa kisiasa duniani ambapo harakati za kutaka afunguliwe zilipiganwa na wanaharakati sehemu mbalimbali duniani licha ya upinzani wa Serikali ya Afrika ya Kusini na Baadhi ya Nchi za Kimagharibi ambazo zilimuona Mandela kama Ghaidi na mchochezi.

Maisha yake ya awali.

Mzee Mandela alizaliwa Julai 18, 1918 katika kijiji cha Mvezo mji mdogo wa Umtatu Jimbo la Cape. Akiwa ni mmoja wa watoto wa Mzee Gadla Henry Mphakanyiswa Nelson Mandela alikulia kwa mamake – mke wa tatu wa Mzee Gadla – katika kijiji cha Qunu ambako pamoja na shughuli nyingine za nyumbani alikuwa mvulana mchunga ng’ombe. 


Baadaye alianza masomo ya shule ya msingi na baadaye Sekondari ambapo aliamini kuwa alikuwa anaandaliwa kwa ajili ya utumishi katika nyumba ya Chifu wa Kabila lake la Xhosa kama mshauri. Hata hivyo baada ya kurudi nyumbani kutoka masomoni mwaka 1940 alikuta kuwa Chifu Jongintaba ameandaa ndoa Nelson Mandela pamoja mtoto wa kiume wa Chifu huyo aitwaye Justice walitoroka nyumbani na kwenda kwenye Jiji la Johannesburg. Alifanya kazi kama mlinzi katika Kampuni ya Madini ya Crown lakini alifukuzwa kazi na msimamizi wa pale baada ya kugunduliwa kuwa alikuwa ametoroka kwao. 


Mandela akiwa amevaa mavazi ya kabila lake la Xhosa; alitoka katika familia ya kichifu.
Kuingia Katika Siasa.

Alipokuwa akiishi kwa muda na mmoja wa binamu zake Nelson Mandela alitambulishwa kwa mwanaharakati wa chama cha ANC Bw. Walter Sisulu ambaye baadaye walifungwa pamoja – Sisulu akitumikia miaka 25 jela. Walter Sisulu alimtafutia kazi ya ukarani katika kampuni ya Wanasheria ya Witkin, Sidelsky and Edelman. Akiwa hapo alifanya masomo ya elimu kwa njia ya Posta ambapo alikuwa anatafuta shahada yake ya kwanza. Mwaka 1943 alihitimu masomo yake ya sheria na kuanza kazi kama Mwanasheria badala ya kurudi kijijini kutumika kwa Chifu. 

Akiwa ameanza kazi kama Mwanasheria Mandela aliendelea kuwa chini ya uangalizi wa Walter Sisulu ambaye alikuwa anaendeleza harakati za kudai haki za weusi. Akikutana mara kwa mara na wanaharakati wengine nyumbani kwa Sisulu Mandela alikutana tena na rafiki yake Oliver Tambo. Ilikuwa ni katika mikutano hiyo alikutana na mwanamama Evelyn Mase ambaye walianza uhusiano wa mapenzi na baadaye kufunga ndoa yake ya kwanza Oktoba , 1944. Walijaliwa watoto wawili wa kiume na wa kike; wa kiume Madiba “Thembi” Thembikile alizaliwa Februari 1946 na wa kike Makaziwe alizaliwa mwaka uliofuatia lakini alifariki miezi tisa baadaye baada ya kupata maambukizi ya ugonjwa uti wa mgongo. 



Mandela na mtoto wake wa kwanza wa kiume Themi.

Baada ya uchaguzi wa 1948 ambapo watu weupe peke yao walishirikia vyama vya Herenigle Nacionale Party na Afrikaner Party viliungana na kuunda chama cha National Party ambacho kilikuwa na sera ya wazi ya ubaguzi na kikapisha na kupanua ukali wa sera ya ubaguzi kupitia sheria mbalimbali za ubaguzi wa rangi. Serikali ya Kikaburu ikaja na mojawapo ya Sheria kali kabisa za kupambana na wanaharakati ambayo inajulikana kama Ukandamizaji wa Ukomunisti ya 1950. Sheria hii ilikuwa inashughulikia karibu mambo yote yanayohusiana na kuipinga serikali na ikiwahusu watu wote. 

Migongano kati ya ANC na Serikali ya Kikaburu ilianza kupamba moto.

Mwaka 1952 Nelson Mandela alikamatwa na utawala wa Makaburu kwa kile kilichodaiwa kujihusisha na vitendo vya Kikomunisti chini ya ile sheria iliyopitishwa miaka michache nyume. Alihukumiwa miezi tisa jela na “kazi ngumu” lakini utekelezaji wa hukumu hiyo ulisitishwa kwa miaka miwili. Lakini mwezi Disemba mwaka huo huo Mandela alipigwa marufuku kuzungumza na zaidi ya mtu mmoja kwa miezi sita. Akiwa kiongozi wa ANC hii ilimaanisha kuwa asingeweza kufanya mikutano na wanachama wake. Mwaka 1953 Mandela na rafiki yake Oliver Tambo walifungua kampuni yao ya Wanasheria katika Jiji la Johannesburg na kuifanya kuwa kampuni ya kwanza ya Wanasheria Weusi katika Afrika ya Kusini. Walijishughulisha na malalamiko mbalimbali ya wananchi hasa yanayohusiana na ukatili wa kisiasa. 

Hata hivyo serikali ikitumia sheria nyingine ikalazimisha kufungwa kwa ofisi hiyo iliyokuwa na wateja wengi na kuihamisha sehemu nyingine ambapo ilikuwa ni vigumu kwa wateja kuifikia. Mwaka 1955 Mandela na wenzake walishirikiana kuandaa kongamano kubwa la watu wa Afrika Kusini ambao wanaamini katika taifa moja la watu wamoja japo wanatoka katika makabila na rangi mbalimbali. 

Katika kongamano hili kulisainiwa kile kinachoaminika kama mojawapo ya nyaraka muhimu kabisa za kutetea usawa na utu wa watu wote ambayo ilijulikana kama Freedom Charter. Kufananisha hii ni sawasawa na Azimio la Uhuru la Marekani au ile nyaraka ya Waingereza ya Magna Carta. Kwa Tanzania tunaweza kufananisha kabisa na Azimio la Arusha. Freedom Charter ilitengeneza ramani ya kujenga taifa la watu walio huru na sawa katika Afrika Kusini. 

Nelson Mandela na Oliver Tambo – wanasheria


Marafiki wawili – miaka mingi toka Kisiwa cha Robben
Hata hivyo kwa upande wa familia ndoa yake kwa Evelyn ilianza kuwa matatani. Kulikuwa na tuhuma za kukosa uaminifu ambapo alidaiwa kuwa na mahusiano ya mapenzi na baadhi ya kina dada wa ANC. Evelyn alijaribu watengane lakini pamoja na jitihahada mbalimbali za kupatana Nelson Mandela aliamua kupeana talaka na mke wake wa kwanza mwezi Machi 1958. Walikuwa wamejaliwa mtoto mwingine wa kike. Wakati huo wa mchakato wa talaka Nelson Mandela alikuwa ameanza mahusiano na Winnie Madikizela mmoja wa wafanyakazi wa mambo ya kijamii. Walifunga ndoa Mwezi Juni 1958.

muongozaji bora wa filamu,JACK KABIGIRI AFUNGA MWAKA KWA KUWASHUKRU WADAU WA FILAMU.


MUONGOZAJI bora wa filamu Swahiliwood Jackson Kabirigi ‘Jack’ anawashukru wadau wote wa tasnia ya filamu kwa ujumla wake kutokana na mchango wake ambao wamempa kupitia kazi zake ambazo ameshiriki katika kuigiza na kuongoza sambamba na filamu ya Mdundiko iliyomletea sifa baada kuchaguliwa nchini Marekani.

Akiongea na wanahabari msanii huyo ambaye ana sifa za kimataifa amesema kuwa baada ya filamu yake ya Mdundiko kushinda tuzo nje ya nchi na si ndani ya nchi ambapo hata tuzo za ZIFF ilinyimwa, lakini Jack anasema kuwa amejifunza mengi na anatoa shukrani kwa wadau wa filamu ambao wamekuwa bega kwa bega katika kuhakikisha anasonga mbele kisanaa.

“Nawashukru wote wanahabari jamaa zangu hata wale ambao wamekuwa wakinishauri kupitia njia mbalimbali, kila mtu kwangu ana mchango mkubwa sana naheshimu hilo kwa kila mtu kwa nafasi aliyo nayo na kuhakikisha wanafanya jambo kubwa kwa ajili yangu mimi Jack nasema Asanteni sana na Mungu awabariki,”anasema Jack.

Aidha msanii huyo ameamua kuanzisha utaratibu wa kutoa taarifa za maendeleo ya kazi yoyote ambayo atakuwa akiifanya na taarifa kuwafikia wapenzi wa filamu nchini nzima na kuwa ndio njia ya wasanii kujenga mahusiano mema na watazamaji wao ambao kuna wanataka kujua maisha ya wasanii ya kawaida nje ya uigizaji lakini si rahisi.

Jack pia anawashukru sana wapenzi wa filamu Swahiliwood baada ya kuipokea kazi yake vema ya Kisate filamu iliyoingia sokoni hivi karibuni na kufanya vizuri kwa kuteka soko la filamu Bongo, sinema hiyo kaongoza na kuigiza mwenyewe akishirikiana na wasanii wengine wakali kama Tino, Dino, Dennis, Mzee Magari, Hamis Korongo na wasanii wengine wanofanya vizuri.

Msanii huyo ana filamu nyingi sana lakini yeye amechagua filamu kadhaa kuwatambulisha wanahabari na wadau wote kwa ujumla, sinema hizo ni  My Nephew, Money Transfer, filamu hizo kaigizia Afrika ya kusini, Born to Suffer, filamu ya Nunda, The Close, Home village,Ania.

Filamu zingine  ambazo kaingiza na kuzingoza ni Filamu ya Hatia Nguvu ya Imani, CID, Single O, Kigodoro, Kisate na filamu bora ya Mdundiko hizi ni baadhi ya filamu ambazo zote zipo katika ubora wa juu na ameahaidi kufanya mambo makubwa mwaka ujao.

Kazi nzuri ya Jack kutoka Bongo filamu yake aliyoongoza ya Mdundiko kuibuka kama filamu bora iliyofanikiwa katika kipengere cha mafanikio ya hadithi katika filamu (Achievement Narrative in Feature Film) ni ushindi mkubwa kwa mapinduzi ya filamu Bongo Movie. Huyu ndio Jackson Kabirigi muongozaji wa filamu wa Kimataifa 

“NAWAPENDA SANA NAOMBA USHIRIKIANO HUU UENDELEE MIMI NI KIJANA WENU SITOWAANGUSHA KATIKA KULETA MAPINDUZI YA KWELI YA FILAMU TANZANIA MUNGU AWABARIKI NYOTE,” Jackson Kabirigi. 05.December. 2013

KERO YA UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA YAPATIWA UFUMBUZI, NAFASI KUTANGAZWA MTANDAONI




001-2Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Mhe,Makongoro Mahanga akitoa hotuba yake. HABARI PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE DAR ES SALAAM 

SERIKALI imezindua mfumo maalumu wa kielektroniki wa taarifa za soko la ajira, ambao utamuwezesha mtafuta kazi kufahamu nafasi mbalimbali za kazi zinazotangazwa ndani na nje ya nchi.

Mtandao huo ambao umeelezwa kuwa utakuwa msaada mkubwa hususani kwa vijana, utamuwezesha muomba kazi kuomba nafasi hizo moja kwa moja katika makampuni husika kulingana na vigezo vitakavyokuwa vikihitajika.

Akizundua mtandao pamoja na maonyesho ya shughuli za huduma za ajira jana jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Makongoro Mahanga alisema, mbali na kutangaza nafasi za ajira pia mfumo huo utawawezesha watu wenye nia ya kuwekeza hapa nchini kutambua aina ya ujuzi unaopatikana nchini na kuwarahisishia katika kuajiri.

“Hii itapunguza waajiri kuajiri wageni zaidi katika zile nafasi ambazo zina wataalumu nchini kutokana na kufahamu mapema. Pia kwa wanafunzi wqa vyuo vikuu watafahamu mapema ujuzi na taalumu wanazopaswa kusoma kwa kuwa utatoa taarifa zitakazowezesha mtu kujua mahitaji ya sasa na ya siku za usoni katika soko la ajira,” aliongeza.

Kwa upande wa waajiri mfumo huo utawawezesha kutangaza nafasi za kazi walizonazo ikiwa ni pamoja na sifa za mtafuta kazi wanayemhitaji.
“Wataweza kupata wafanyakazi wenye viwango wanavyovitaka kwa urahisi kwa kujiunga na mtandao huu,” alisema.

Alisema hatua ya mtandao huo utasaidia kupunguza ukosefu vwa ajira kwa vijana kwani kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2006 tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana lilikuwa kwa asilimia 13.4 hivyo ni matarajio kiwango hicho kitapungua baada ya waajiri wengi kutangaza ajira kupitia mtandao huo.

Mahanga ametoa wito kwa waajiri wote nchini kutumia mfumo huo kutangaza ajira na watafuta kazi na kuutumia kupata taarifa sahihi ili kuweza kuomba nafasi hizo.
Mtandao huo ambao umezinduliwa ni www.ajiralmis.go.tz, vijana wametakiwa kuutumia kwa usahihi zaidi ili kunufaika na ajira zinazotangazwa
002-2Huu ndio mtandao uliozinduliwa.
003Wanafunzi na wahitimu wa vyuo mbalimbali wakiwa kwenye kongamano la  siku mbili jinsi ya kuandika barua ya maombi ya kazi  katika  ukumbi wa Mw. Julius Kambarage Nyerere jijin dar es Salaam. 004Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Mhe Makongoro Mahanga, akimsikiliza Kaimu Mtendaji Mkuu wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaEsA), Boniface Chandaruba wakati akielezea kazi wanazofanya kuhusiana na ajira kwa vija mara baada ya kutembelea banda hilo, 007Wafanyakazi wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaEsA), wakiwa kwenye picha ya pamoja katika kongamano la  siku mbili jinsi ya kuandika barua ya maombi ya kazi  katika  ukumbi wa Mw. Julius Kambarage Nyerere jijin dar es Salaam.

BENKI YA BARCLAYS TANZANIA YACHEZESHA DROO YA PILI YA KAMPENI YA "DOUBLE YOUR SAVING" LEO NA KUWATAJA WASHINDI WATANO




 Mkuu wa Kitengo cha Affluent Banking wa benki ya Barclays Tanzania Ms Neema Rwehumbiza akiongea na waandishi wa habari waliofika katika ofisi za Benki hiyo katika tawi lililopo Alpha House barabara ya Ali hassan Mwinyi kwaajili ya kushuhudia washindi wa Droo ya Pili ya "Double your Saving"kutoka benki ya Barclays.
 Mmoja wa Wafanyakazi wa Benki ya Barclays tawi la Alpha house Barabara ya Ali Hassan Mwinyi akizungusha pipa lenye kuponi za washiriki wa droo ya pili ya "Double Your Saving" kwaajili ya kupata washindi wa tano wa Mwezi November, huku akiongozwa na afisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
  Mkuu wa Kitengo cha Affluent Banking wa benki ya Barclays Tanzania Ms Neema Rwehumbiza akisoma jina la Mshindi wa Kwanza aliyepatikana mara baada ya pipa hilo kuzungushwa katika droo ya pili ya "Double your saving' kutoka Benki ya Barclays Tanzania iliyochezeshwa leo katika Ofisi ya Benki hiyo katika tawi lililopo barabara ya Ali Hassani Mwinyi
Mmoja wa Wafanyakazi wa Benki ya Barclays tawi la Alpha house Barabara ya Ali Hassan Mwinyi akichukua moja ya kuponi za washiriki wa droo ya pili ya "Double your Saving" kwaajili ya kumtaja mshindi wa Pili katika droo iliyochezeshwa leo na Kupelekea kupatikana kwa washindi watano ambao kila Mmoja ataondoka na Kitita Cha shilingi Milioni Moja
.................................
5 Disemba 2013 , Baclays Bank Tanzania leo imefanya droo yake ya Pili kwa wateja wake katika kampeni ijulikanayo kama "Double Your Saving". Kampeni hii ilianza rasmi tarehe 16 septemba 2013 na itaendelea hadi tarehe 16 Januari 2014.

Kila Mwezi, droo hii itawapatia wateja watano nafasi ya kujishindia hadi shilingi milioni moja za kitanzania kila mmoja kwa kipindi chote cha kampeni. Droo za mwezi, zitakuwa zinafanyika wiki ya mwisho ya mwezi husika.

Akiongea na waandishi wa habari Mkuu wa Kitengo Cha Affluent cha Benki ya Baclays Ms Neema Rwehumbiza amesema; "Ushiriki upo wazi kwa wateja wote binafsi(waliopo na wapya) kupitia akaunti zao za akiba na za hundi.

Wanachotakiw kufanya ni kuongeza na kutunza akiba zao kwa kiwango cha Shilingi laki tatu (300,000) za kitanzania au zaidi. Kiwango hiko kitampa mteja nafasi ya kushiriki katika droo ya mwezo husika tu. Baada ya kuongeza akiba kwa kiwango husika, mteja ataingia kwenye droo ya mwezi na kupata nafasi ya kujishindia hadi shilingi milioni moja za Kitanzania. Kila ongezeko la shilingi laki tatu litampatia mteja nafasi moja ya kushiriki.

Wateja wote watakaoongeza salio kwenye akaunti zao kwa shilingi laki tatu au zaidi katika kipindi hiki cha kampeni wanajipatia nafasi ya kushinda zawadi kubwa kabisa ya shilingi za kitanzania Milioni Thelathini (30,000,000) mwishoni mwa kampeni hii.

Aliongeza kuwa, "hii ni droo ya pili ambao tunapata washindi wengone watano. Baclays inawapongeza washindi wote na kuhamasisha watanzania wote kushiriki katika kampeni hii hususani katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa Mwaka

DR SLAA AITEKA KAHAMA KATIKA ZIARA YAKE



Katibu mkuu  wa  Chadema  Dr  Wilbroad Slaa akiwahutubia  wananchi  wa Kahama mara  baada ya  kuwasili mjini hapo kwa  ziara  yake  ya  kichama jana
Dr Slaa akisalimiana na  wananchi waliofika  kumpokea mjini Kahama  jana. leo Desemba 5, atakuwa Wilaya ya Kakonko, Jimbo la Buyungu na Desemba 6, atakuwa Jimbo la Muhambwe.

MALORI MANNE YA MIZIGO YAPATA AJALI JUZI KATIKA DARAJA LA WAMI



 Gari aina ya Fuso likiwa limepinduka Juzi Jumanne mara baada ya tairi la mbele kuchomoka Eneo la Wami Darajani pembeni ni gari aina ya fuso ambalo likuwa likibeba mizigo iliyokuwa imebebwa na fuso hilo lililopinduka
 Kwa mbele gari aina ya Fuso lilivyopinduka juzi jumanne eneo la Wami Darajani
 Hapa napo ni Wami darajani ambapo lori la mizigo nalo lilipiga mweleka mbaya sana Jumatatu ya wiki hii lakini halikuweza kutolewa hadi juzi jumanne usiku
 Fuso likibeba mizigo uiliyokuwa kwenye lori lililopinduka 
 Lori la Mizigo likitengenezwa mara baada ya kupata ajali eneo hilo la Wami Darajani Jumatatu ya Wikii hii na kushindwa kabisa kuondolewa hadi kufikia juzi jumanne usiku
Tera la lori likiwa limekatika kutoka kwenye lori la mizigo lililopata ajali Jumatatu ya Wiki hii eneo la Wami Darajani na kupelekea tera hilo kushindwa kuondolewa hadi kufikia jana Usiku
 Hili nalo 
 Wafanyakazi wa lori wakiendelea na zoezi la Uokoaji wa mizigo iliyokuwa kwenye lori hilo juzi Jumanne katika ajali iliyotokea Wami Darajani
 Hivi ndivyo lilivyokuwa mara baada ya kutoka nje ya barabara
Kwa Mbali linavyoonekana

Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, afungua Kongamano la kitaifa la Ajira Afrika




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua Kongamano la Kitaifa la Ajira kwa bara la Afrika kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam leo Disemba 5,2013.
Baadhi ya washiriki wa kongamano la kitaifa la Ajira barani Afrika wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipokua akifungua Kongamano hilo leo Disemba 5,2013 katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalim Julius nyerere Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal katikati, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Kitaifa la Ajira kwa bara la Afrika mara baada ya kufungua kongamano hilo leo Disemba 5-2013 kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri wa kazi na Ajira Mhe. Gaudensia Kabaka mara baada ya kufungua kongamano la kitaifa la Ajira kwa bara la Afrika kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam leo Disemba 5,2013. (Picha na OMR)

Tuesday, December 3, 2013

WASANII KIBAO WAJITOKEZA KUSHIRIKI MKESHA WA MBIO ZA UHURU MARATHON



Katibu wa kamati ya maandalizi ya mbio za uhurumarathon, Innocent Melleck, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya maandalizi na wasanii watakaoshiriki kwenye mkesha wa Uhuru utakaofanyika viwanja vya Leaders Club baada ya kukamilika kwa mbio za uhuru. Kushoto ni katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania Selemani Nyambui.
*********************************
Na Mwandishi Wetu, Dar
ZIKIWA zimebaki siku chache kwa ajili ya shindano la mbio ndefu za Uhuru, 'Uhuru Marathon', kufanyika, wasanii watakaotoa burudani siku ya mkesha wa uhuru wapania kufanya kweli.
Wasanii wanaotarajiwa kutoa burudani ni Roma Mkatoliki, Joh Makini, G Nako, Nick wa Pili, Mrisho Mpoto, Mrisho Mpoto, TMK Wanaume, Mfalme Siboka na kundi la Twanga Pepeta.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wasanii hao walisema wanashukuru kupewa heshima kubwa kutumbuiza siku hiyo na hasa ukichukulia umuhimu wa amani, umoja na mshikamano miongoni mwetu.
“Nitafanya makamuzi ya kweli siku hiyo na watu wategemee mistari iliyokwenda shule,” alisema Roma Mkatoliki, huku Mrisho Mpoto akidai ana vitu vikali zaidi atakavyoweka hadharani siku hiyo.
Naye Katibu wa Kamati ya Uhuru Marathon, Innocent Melleck alisema, homa ya mbio hizo imepanda, hasa baada ya kujitokeza kwa wanariadha wengi wa mataifa, kutoka nchi mbalimbali.
Melleck alisema, mbali na wengi kujitokeza bado anaamini wengi wataendelea kujiandikisha ili kufanikisha lengo la mbio hizo.
Aidha alisema kuwa usajili bado unaendelea kwa wale wanaotaka kushiriki ambapo fomu zitakazotolewa kwa mshiriki wa kilomita 3 atalipa Sh 100,000 yule wa kilomita 5 Sh 2,000 na washiriki wa kilomita 21 na 42 watalipia Sh 6,000.