MWENYEKITI
wa TEFA, Peter Muhunzi na Sizza Chenja
wameshinda
rufaa baada ya kuwekewa pingamizi kwenye mchakato wa uchaguzi wa Chama cha Soka
mkoa wa Temeke. (TEFA)
Akitoa
maazimio ya Kamati ya Uchaguzi ya DRFA,Mwenyekiti wa Kamati, Advocate Rashid Saadallah, alisema kamati yake ilipitia mapingamizi
yake kwa makini na kina kwa kufuata katiba ya TEFA, DRFA na ya chama mama
ambacho ni TFF na kutoka na maamuzi ambayo hata hivyo alikiri kama mgombea
hataridhika anaweza kukata rufaa kwenye ngazi nyingine ambayo ni TFF.
“Peter
Muhunzi ambaye anagombea nafasi ya mwenyekiti wa TEFA, ameshinda rufaa yake
baada ya kuthibitisha kigezo cha elimu kwa
maana ya kumaliza kidato cha nne na Sizza Chenja kamati imempitisha
aendelee na mchakato wa uchaguzi baada ya kuthibitisha kuwa ana uzoefu wa
kutosha katika uongozi wa mpira wa miguu kama katiba ya TEFA Ibara ya
(31)(1)(j) inavyotaka”, alisema Saadallah
Pia alisema Rashid Salim, ambaye pia
anagombea nafasi ya Mwenyekiti -ameshindwa
kuleta vielelezo kuthibitisha uzoefu wake katika masuala ya mpira kama Ibara ya
31(1)(j) inavyosema pia Aziz Mohamed Khalfan, kamati imegundua kwamba
alienda kwenye mchakato wa uchaguzi akiwa hana sifa kwa sababu alifungiwa na
kamati ya nidhamu na usuluhishi ya kutokushiriki au kujihusisha na mpira kwa
muda wa miezi kumi na mbili (12) na TEFA.
Saadallah alisema kwenye nafasi ya
Makamu wa kwanza wa Mwenyekiti, Shufaa Jumanne amepitishwa aendelee na mchakato wa uchaguzi baada ya
kuridhika na uthibitisho wa uzoefu wa zaidi ya miaka mitatu katika uongozi wa
soka Daudi Mumbuli, kamati inaitupilia mbali rufani baada muweka pingamizi
kushindwa kutokea mbele ya kamati kuthibitisha madai yake.
Naye Omary Kapilima ambaye anagombea
makamu wa kwanza wa Mwenyekiti ameondolewa baada ya kushindwa kuleta cheti cha kidato cha nne kinachotambulika na Baraza la Mitihani la
Taifa yaani (NECTA) ili kukidhi kigezo cha elimu kama inavyotakiwa na Ibara ya
31(1)(b) ya katiba ya TEFA japo kathibitisha
uzoefu wa uongozi wa mpira na Salehe Mohamed kamati inamuengua katika
mchakato wa uchaguzi kwa kushindwa kuthibitisha kiwango chake cha elimu kwa
kushindwa kuleta cheti cha kidato cha nne(Academic Certificate) kama
inavyotakiwa na Ibara ya 31(1)(b) ya katiba ya TEFA pia Bakili Makele ambaye
alikuwa anagombea makamu wa pili ameenguliwa kwa kigezo hicho cha elimu kwani
amekiri kwamba elimu yake ni ya darasa la saba
Amack Nabola ambaye anagomea Ujumbe
wa soka la wanawake na vijana ameenguliwa katika mchakato kwa kukosa sifa
ya elimu ya kidato cha nne kama ibara ya 31(1)(b) ya katiba ya TEFA inavyotaka
lakini Fikiri Magoso ambaye anagombea mjumbe wa kamati ya Utendaji amepitishwa
kugombea nafasi hii kwa sababu anakidhi vigezo kwa kuwa na cheti cha darasa la
saba kama katiba ya TEFA anavyomtaka mgombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya
utendaji kuwa na elimu isiyo chini ya darasa la saba.
Mgombea Muhibu Kanu ambaye alikuwa
nagombea nafasi mbili, ya makamu Mwenyekiti na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji kamati
imemuengua kwa sababu ni kinyume cha kanuni za uchaguzi za TFF za mwaka
Ibara 10(9) ambayo inakataza mgombea kugombea nafasi zaidi ya moja.
No comments :
Post a Comment