Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, July 20, 2016

Airtel yaipiga jeki Serikali ya Mtaa wa Kumbukumbu jijini Dar



Katibu tarafa wa Kinondoni Bw, Fortunatus Fulgence Isakafu (wa pili kulia), akipokea msaada wa mapipa ya kukusanyia takataka kwaajili ya mtaa wa Kumbukumbu kutoka kwa Afisa Mazingira wa Airtel, Ncheye Mazoya (kulia), katika hafla iliyofanyika kwenye ofisi ya serikali za mtaa huo, Wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.  Wanaoshuhudia (kutoka kushoto) ni Mwenyekiti wa Mtaa Kumbu kumbu, Bw, Shaban Majeshi na Diwani wa Kata ya Kinondoni, Mustafa Muro. 
Afisa Mazingira wa Airtel Bwana, Ncheye Mazoya na  Katibu tarafa wa Kinondoni Bw, Fortunatus Fulgence Isakafu wakikabidhi mapipa yakukusanyia uchafu kwaajili ya mtaa wa kumbukumbu kwa Diwani wa Kata ya Kinondoni Bw, Mustafa Muro na Mwenyekiti wa Mtaa Kumbukumbu Bw, Shaban Majeshi. Hafla ya makabidhiano imefanyika leo katika ofisi ya serikali za mtaa huo.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imetoa msaada wa mapipa 15  ya kukusanya na kutunzia takataka  kwa serikali ya mtaa wa kumbukumbu   kata ya kinondoni yenye thamani shilingi milioni 3 na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika shughuli mbalimbali za kutunza mazingira ili kuiwezesha jamii kuishi katika mazingira bora yatakayopelekea kuwa na afya bora.
Akiongea wakati wa hafla ya makabidhiano Afisa mazingira wa Airtel Bwana, Ncheye Mazoya alisema “Airtel tunatambua sana jitihada zinazofanywa na serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania  katika kutunza na kuweka mazingira ya jamii kuwa safi. kwetu sisi Airtel Tunaamini  kwamba  ili tuweze kufanya biashara lazima tuwe na mazingira safi na wateja wenye afya bora, na ndio maana leo hii tunaunga mkono harakati za serikali za kuhakikisha swala hili la kufanya usafi kila mahali linaendelea kufanikiwa
“Tunaamini  mapipa haya ya kutunzia taka yatasaidia jamii inayotuzunguka hapa kinondoni na kuweka mazingira katika hali ya usafi na kusaidia kuepusha magonjwa ya milipuko ambayo yamekuwa ni changamoto kubwa sana nchini” alieleza Mazoya
Kwa upande wake Katibu tarafa wa Kinondoni Bwn Fortunatus Fulgence Isakafu Aliwapongeza Airtel kwa mchango wao na kuongeza kwamba tarafa yake ina mpango  mkakati wa kutekeleza kwa vitendo kampeni ya usafi kwa kuhamasisha jamii kujitolea katika kutunza mazingira yanayowazunguka na kuyaweka kuwa safi wakati wote.
“Airtel msaada wenu umekuja wakati sahihi kwa kuwa zoezi la usafi kwetu sisi ni endelevu, mapipa haya ya kuhifadhi taka yatasaidia sana kupunguza kuzagaa kwa taka kila mahali  na kurahisisha ukusanyaji taka kwa ajili ya kuzipeleka sehemu maalum kwa uteketezaji”
Tunatoa wito kwa wadau mbalimbali kutuunga mkono na kuungana nasi katika kampeni hii kama walivyofanya wenzetu wa Airtel leo. Alimaliza kwa kusema Bwn, Isakafu

No comments :

Post a Comment