Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, February 3, 2013

MATEMBEZI YA MATEMBEZI YA MSHIKAMANO YA MIAKA 36 YA CCM YAFANA KIGOMA

Mwenyekiti wa CCM Rais Janakaya Kikwete akiongoza matembezi ya maadhimisho ya miaka 36 ya CCM, leo asubuhi kutoka eneo la Mnarani hadi ofisi ya CCM mkoa wa Kigoma leo. Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk. Amani Kaborou, Mama Salma Kikwete, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kulia)
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiongoza matembezi ya mshikamano ya Miaka 36 ya CCM, mjini Kigoma leo
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiongoza matembezi ya Mshikamano ya Maadhimisho ya Miaka 36 ya CCM mjini Kigoma leo
Matembezi hayo yakipita eneo la Burega, Barabara ya Kigoma-Ujiji
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akiwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Sadifa Abdalla na Mkuu wa wilaya ya Kigoma Jumanne Maneo
Wananchi wakishangilia wakati matembezi yakipita barabara ya Ujiji Kigoma kwenda Ofisi ya CCM ya mkoa wa Kigoma leo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimsalimia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana baada ya kuwasili eneo la Mnarani mjini Kigoma tayari kwa matembezi hayo. Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula na wengine ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwapungia mkono wananchi msafara wa matembezi hayo ulipokaribika kufika Ofisi ya CCM mkoa wa Kigoma
Rais Kikwete akiwa na Nape na Kinana baada ya msafara wa matembezi hayo kuwasili
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikweye akiwa na muaasisi mmoja wa CCM ( ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja) baada ya matembezi kufika Ofisi ya CCM mkoa wa Kigoma
 
 Mama Salma Kikwete akisalimia baada ya msafara wamatembezi hayo kufika Ofisi ya CCM mkoa wa Kigoma
Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete na msafara wake wakiwa wameketi meza kuu Ofisi ya CCM mkoa wa Kigoma baada ya matembezi hayo.
"NDUGU WANANCHI, NAWAPONGEZA KWA KUSHIRIKI KWA WINGI KWENYE MATEMBEZI HAYA. HAPA SISEMI MENGI TUKUTANE MCHANA PALE UWANJA WA LAKE TANGANYIKA" Akasema Rais Kikwete wakati akizungumza na wananchi baada ya matembezi hayo. (PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO@Daily Nkoromo Blog)

BENKI YA EXIM YAIPIGA JEKI KLABU YA GYMKHANA



Kapteni wa mchezo wa squash wa klabu ya Gymkhana Akil Hirji (katikati) akikabidhi zawadi kwa Mkrugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim Anthony Grant (wapili kushoto) kama ishara ya kutambua jitihada za kukarabati viwanja viwili vya mchezo wa squash mwishoni mwa wiki. (Na Mpiga Picha Wetu)
                                                                

Mkrugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim Anthony Grant (katikati) na Mwenyekiti Msaidizi wa Klabu ya Gymkhana William Chiume (wapili kulia) wakikata utepe ulikuzindua viwanja viwili vya mchezo wa Squash vilivyokarabatiwa na benki ya Exim. 



DAR ES SALAAM, Tanzania
KATIKA jitihada zake za kusaidia maendeleo ya michezo nchini, Benki ya Exim Tanzania, imeipiga jeki Klabu ya Gymkhana ya jijini Dar es Salaam kwa kuikarabatia viwanja vyake viwili vya mchezo wa Skwashi.
Akizungumza mwishoni mwa wiki katika hafla ya ufunguzi wa viwanja hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim, Anthony Grant alisema mchango wa benki yake unatokana na kutambua umuhimu wa michezo katika maisha ya kila siku na kwamba anaamini utasaidia kuendeleza mchezo huo. 
 
“Benki ya Exim tumeamua kushirikiana na Klabu ya Gymkhana kukarabati viwanja viwili vya skwashi ili kujenga mazingira mazuri ya uchezaji wa mchezo huo kwa wachezaji. Tunapongeza dhamira ya kitaifa ya Gymkhana, hasa jitihada zake za kujenga uelewa kwa vijana katika michezo,” alisema Grant.
Grant alibainisha kuwa uwekezaji katika michezo ni suala muhimu kama nchi inahitaji kupata mabalozi wazuri wa kuliwakilisha taifa nje ya mipaka na ndiyo maana benki yake imeamua kusaidia ukarabati wa viwanja hivyo, huku akiyataka makampuni mengine kuiga mfano wa Exim katika uwekezaji.
Kwa upande wake, nahodha wa mchezo wa skwashi wa Klabu ya Gymkhana, Akil Hirji, alisema kuwa ukarabati wa viwanja hivyo ni msaada mkubwa utakaoinua maendeleo ya mchezo huo na kusema kuwa klabu itatumia vizuri miundombinu hiyo iliyoboreshwa.
“Naishukuru Exim kwa msaada wao na nina imani utakuza maendeleo ya skwashi nchini. Kwa viwanja hivi vya kisasa, wachezaji watakuwa katika nafasi nzuri ya kushindana kitaifa na kimataifa,” alisema Hirji na kuongeza Gymkhana imeandaa mashindano ya uzinduzi wa viwanja hivyo yatakayohusisha wachezaji 30.

BONDIA WA ZAMANI MUHAMMAD ALI YUPO KITANDANI AKISUMBILIWA NA MARADHI




Bondia Muhammad Ali akimdondosha chini mpinzani wake katika moja ya mapambano yake

LONDON, England
Rahman Ali ndugu wa kuzaliwa wa Muhammad, amefichua: “Ndugu yangu hawezi kuongea, hawezi hata kunitambua mimi. Yuko katika hali mbaya kwa kweli. Ali anaumwa sana”
NDUGU wa kuzaliwa wa bondia wa zamani Muhammad Ali, 71, Rahman Ali amesema kuwa hali ya kaka yake ni mbaya na anapigania maisha yake kujikoa na kifo, huku siku zake za mwisho zikizua shaka, simanzi na vilio kwa mke wake.
Rahman, 69, amesisitiza kuwa homa pekee si sababu inayoyaweka hatarini maisha ya nduguye, bali shambulio la moyo lililochukua fahamu zake lina mchango mkubwa wa kuhitimisha zama za mkongwe huyo.
Akiwa katika mahojiano juu ya hali ya kaka yake, Rahman alidondosha machozi chini kwa uchungu na kusema yeye binafsi angependa kumuona kaka yake akifariki sasa, ili kumuepushia na matatizo anayokumbana nayo.
Rahman alifichua kwamba: “Ndugu yangu hawezi kuongea, hawezi hata kunitambua mimi. Yuko katika hali mbaya kwa kweli. Ali anaumwa sana.
“Inaweza kuwa miezi, inaweza kuwa baada ya siku kaddhaa. Mimi sijui kama atafika majira ya joto. Yuko katika mkonono ya Mungu. Tunatarajia kuona Mungu akimponya.
“Aliniambia hapo kabla ya kuzidiwa kwamba haumwi na hasikii maumivu yoyote. Alinyanyua mkono wangu na kunipa wasiwasi kwa kuniaga, ‘Rahman, nimefanikiwa katika kila kitu na nimekamilika kimafanikio. Usilie kwa ajili yangu, mimi siumwi na sina maumivu yoyote,’
“Ali ataenda peponi, hakuna shaka juu ya hilo. Kama atakufa na kuzikwa kesho, mataifa yote na watu wote duniani watageuka na kuungana kwa ajili yake. Ali alimgusa na kumvutia kila mmoja kuanzia maskini hadi matajiri.
“Nampenda ndugu yangu kuliko mtu yeyote. Katika watu wote maarufu walio hai, huyu ni bora zaidi yao. Kila mmoja anajua kwamba Muhammad Ali. Yeye yuko juu pamoja na Yesu Kristo.
“Mimi nalia kwa sababu nina machungu juu yake, ananivunjaa moyo wangu. Nina matumaini ya ya kumuona tena akiwa hai, lakini ninaweza tu kutumaini.”
…….The Sun……

RAIS KIKWETE ATUA KIGOMA KUONGOZA MAADHIMISHO YA MIAKA 36 YA CCM



 Ndege iliyombeba Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Rais Jakaya Mrisho Kikwete ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mkoani Kigoma jioni hii,tayari kwa kuhudhulia Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi (CCM),yatakayofanyika kitaifa kesho kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.
Wananchi lukiki wakiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma kumpokea Rais Jakaya Kikwete leo.nyuma yao ni Ndege ya Rais ikiwasili.
Mwenyekiti wa Chama cha Mainduzi (CCM),Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Mh. Issa Machibwa wakati alipo wasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma,Jioni ya leo tayari kwa kuhudhulia Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi (CCM),yatakayofanyika kitaifa kesho kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mainduzi (CCM),Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu CCM,Abdulrahman Kinana wakati alipo wasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma,Jioni ya leo tayari kwa kuhudhulia Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi (CCM),yatakayofanyika kitaifa kesho kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.Wa tatu kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM - Bara,Phillip Mangula.
Mwenyekiti wa Chama cha Mainduzi (CCM),Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea salamu kutoka kwa vijana wa Chipukizi wa CCM mkoani Kigoma,wakati alipo wasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma,Jioni ya leo tayari kwa kuhudhulia Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi (CCM),yatakayofanyika kitaifa kesho kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mainduzi (CCM),Rais Jakaya Mrisho Kikwete akivishwa skafu na Chipukizi wa CCM mkoani Kigoma wakati alipo wasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma,Jioni ya leo,tayari kwa kuhudhulia Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi (CCM),yatakayofanyika kitaifa kesho kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mainduzi (CCM),Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM - Bara,Mh. Mwigulu Nchemba.
Mwenyekiti wa Chama cha Mainduzi (CCM),Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM mkoani Kigoma.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na wananchi wa Mkoa wa Kigoma waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma kumlaki.
Mwenyekiti wa Chama cha Mainduzi (CCM),Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM CCM,Nape Nnauye.
 Baadhi ya Viongozi wa Chama na Serikali wakiwa tayari kumpokea Rais Jakaya Kikwete.
 Kutoka kulia ni Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye,Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha - Rose Migiro na Katibu wa NEC,Oganaizesheni,Dkt. Mohamed Seif Khatib.
 WanaCCM wakiwa uwanjani kumpokea Rais Kikwete.
 Burudani.
Rais Kikwete akisikiliza swali lililokuwa likulizwa na Mwandishi wa Habari wa Radio Uhuru,
Msafara wa Rais ukipita barabarani.
Rais Kikwete akiwapungia wananchi.
Wanahabari waliopo mkoani Kigoma tayari kwa kuripoti Maadhimisho ya Miaka 36 ya CCM,wakiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma kwa ajili ya kukava tukio la kuwasili Rais Jakaya Kikwete Mkoani Kigoma.

PAMBANO LA YANGA, MTIBWA SUGAR LAINGIZA MIL 125/-



 
Mechi namba 100 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa jana (Februari 2 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 limeingiza sh. 125,181,000.
Watazamaji 22,030 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 30,356,002.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 19,095,406.78.
Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo 19,583 walikata tiketi hizo na kuingiza sh. 97,915,000.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 15,435,255.48, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 9,261,153.29, Kamati ya Ligi sh. 9,261,153.29, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 4,630,576.64 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 3,601,559.61.
WANYARWANDA KUCHEZESHA MECHI YA STARS, CAMEROON
Waamuzi kutoka Rwanda wanaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ndiyo watakaochezesha pambano katika Tanzania na Cameroon litakalochezwa Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mwamuzi wa katikati atakuwa Munyemana Hudu wakati wasaidizi wake ni Simba Honore na Ndagizimana Theogine wakati mwamuzi wa mezani ambaye pia anatambuliwa na FIFA atakuwa Oden Mbaga wa Tanzania.
Hudu na wenzake watawasili nchini kesho (Februari 4 mwaka huu) saa 12.40 jioni kwa ndege ya RwandAir na wamepangiwa kufikia kwenye hoteli ya JB Belmont. Mechi ambayo ni moja kati ya nyingi zitakazochezwa siku hiyo (FIFA Date) itafanyika kuanzia saa 11 kamili jioni.
KUNDI LA AKINA ETO’O KUTUA KESHO DAR
Wakati kundi la kwanza la timu ya Cameroon lenye watu 13 linaingia nchini leo (Februari 3 mwaka huu) saa 4.40 usiku, kundi la pili linaloongozwa na nahodha wa timu hiyo Samuel Eto’o linatua kesho (Februari 4 mwaka huu) saa 3.45 asubuhi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Eto’o anayechezea timu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi atatua kwa ndege ya Kenya Airways akiwa na Herve Tchami wa Budapest Honved ya Hungary, beki Nicolas Nkoulou wa Marseille ya Ufaransa, mshambualiji Jean Paul Yontcha wa SC Olhanense ya Ureno na daktari wa timu Dk. Boubakary Sidik.
Saa moja baadaye baada ya Eto’oo kutua na wenzake, Kocha wa timu hiyo Jean Paul Akono na msaidizi wake Martin Ndtoungou watawasili saa 4.40 asubuhi kwa ndege ya Kenya Airways wakitokea Afrika Kusini.
Kesho pia kuna kundi lingine litakaloingia saa 4.40 usiku kwa ndege ya KLM ambalo lina beki Jean Kana Biyick wa Rennes ya Ufaransa, mshambuliaji Fabrice Olinga wa Malaga FC ya Hispania, beki Allan Nyom wa Udinese ya Italia ambaye yuko kwa mkopo Granada ya Hispania na beki wa kushoto Henri Bedimo wa Montpellier ya Ufaransa.
Wachezaji waliobaki wakiongozwa na kiungo wa Barcelona, Alexandre Song watawasili Februari 5 mwaka huu kwa muda tofauti kwa ndege za KLM na Kenya Airways.

UHAMISHO WA DROGBA WAISHTUA SHANGHAI SHENHUA YASEMA HAIUTAMBUI



Uhamisho wa Didier Drogba kuelekea Galatasaray ya Uturuki uko mashakani kufuatia klabu yake ya Shanghai Shenhua kusisitiza kuwa mshambuliaji huyo ana mkataba nao.
 
Galatasaray ilitangaza kumsaini Drogba jumatatu kwa mpango wa uhamisho wenye thamani ya euro milioni €6 mpaka kiangazi 2014.
Shenhua imesema imesema inajipanga kuweka pingamizi.

Taarifa iliyotolewa na Shenhua kupitia mtandao wa klabu hiyo ikisomeka "Klabu imeshtushwa sana. Drogba bado ni mchezaji wa Shanghai Shenhua kwa kuwa ana mkataba nasi nab ado yuko katika kipindi halali cha mkataba.

"Shanghai Shenhua iko tayari kuepeleka ushahidi FIFA ili kupinga jaribio hilo”

MGOMBEA SAID MOHAMED ANAYEGOMBEA NAFASI YA MAKAMU MWENYEKITI WA BODI YA LIGI AONDOLEWA PINGAMIZI



Wakati mchakato wa uchaguzi ndani ya shirikisho la soka nchini TFF na bodi ya ligi kuu ukizidi kupamba moto huku baadhi ya wagombea wakiwekewa mapingamiz na wadau mbalimbali wa soka nchi hatimaye pingamizi alilowekewa mgombea wa nafasi ya makamu mwenyekiti Said Mohamed limeondolewa.

Pingamizi liliwekwa kwa mgombea huyo lilitoka kwa katibu wa zamani wa chama cha soka mkoa wa kisoka wa Kinondoni Frank Mchaki ambaye aliweka pingamizi hilo kutokana na kwamba mgombea huyo hakuwa kiongozi wa klabu yoyote nchini.

Hata hivyo kufuatia kamati ya uchaguzi kukutana na wagombea na wawekaji wa mapingamizi hayo kwa lengo la kufanyika mapitio ya mapingamizi mbalimbali na sababu za mapingamizi hayo imedhihika kuwa Mzee Said Mohamed ni kiongozi wa Azam fc kwa nafasi ya mwenyekiti.

Akiongea na waandhishi wa habari hii mwekaji wa pingamizi hilo Mchaki amesema ameridhishwa na zoezi la kuhakiki nafasi ya uongozi ya mzee Said Mohamed ndani ya Azam kwani aliweka pingamizi kwa kuwa alikuwa hana uhakika kama Said Mohamed ni kiongozi wa kuchaguliwa wa Azam licha ya kwamba amekuwa akisikia kuwa ni kiongozi wa klabu hiyo.

Mchaki amesema mzee Said Mohamed alikuja na vielelezo kamili ambavyo vimeonyesha kuwa alichaguliwa kuwa makamu mwenyekiti 1/10/2012 alikuwa ni mwenyekiti wa Azam.

Kumbuka moja ya sifa ya kuwania nafasi ya uongozi ndani ya bodi ya ligi, mgombea anapaswa kuwa kiongozi katika moja ya vilabu vya ligi kuu.

HIVI NDIVYO MOTO ULIVYODHIBITIWA PPF TOWER.




Kikosi kazi cha zimamoto kutoka makampuni mbalimbali wakiwa kwenye sehemu ya juu ya ghorofa la PPF Tower lililopo Mtaa wa Ohayo (Ohio) eneo la Posta jijini Dar es Salaam baada ya kuwaka motoleo asubuhi, ambao chanzo chake bado hakijafahamika. Hata hivyo sehemu iliyowaka moto ni sehemu yenye mitambo mingi inayotumika kwa shughuli mbalimbali ndani ya jengo hilo.
Timu iliyodhibiti moto ikiendelea kuzima kabisa moto huo

Pichani askari wa kikosi cha uokoaji cha zimamoto wakiingia kwenye chumba chenye mitambo inayoungua kilichopo sehemu ya juu ya ghorofa hiyo kwa zamu kutokana na kuwepo kwa moshi mzito.
Baadhi ya mashuhuda wakiwa nje ya jengo hilo sehemu ya chini ya ghorofa huku shughuli za uzimaji zikiendelea juu ya ghorofa.
Kama kawaida ya matukio mengi yanayotokea jijini Dar es Salaam mashuhuda hawakosi kama unavyoona pichani huku kila mmoja akitaka kushuhudia kinachoendelea.
Kikosi cha zimamoto kikijipanga eneo la nje ya sehemu ya juu ya ghorofa hilo na kuingia kwa zamu sehemu iliyokuwa ikiteketea.

Saturday, February 2, 2013

MASHINDANO YA KLABU BINGWA YA NGUMI KATIKA PICHA



Mabondia Kombe Ally wa Luaha Galax akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Said Hofu wa JKT Makao Makuu wakati wa mashindano ya Klabu Bingwa yaliyofanyika uwanja wa Ndani wa Taifa.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Said Hofu
Mabondia wa timu ya JKT Makao Makuu kutoka kushoto ni Ismail Gaitano,Hmidu Alfani,Khamis Husein na Wambura Amiri klabla awajaingia kwenye mipambano yao picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Wambura Amir akipasha misuri moto  picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Selemani Kidunda wa Ngome kulia  akimuazibu Mohamedi Chibumbui wa Magereza wakati wa mashindano ya Klabu bingwa yaliyofanyika uwanja wa ndani wa taifa Kidunda alishinda kwa K,O rauni ya kwanza na kuzima ngebe za Chibumbui na kusababisha kumpoteza fahamu kwa takribani dakika 4 ambazo alikuwa akipewa uduma ya kwanza uringoni alipodondoka baada ya kupata makonde yenye kilo nzito Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Mohamedi Chibumbui kushoto akitafuta mbinu ya kumkepa bondia Selemani Kidunda wakati wa mashindano ya klabi bingwa ya Masumbwi Kidunda alishinda K,o raundi ya kwanza Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Selemani Kidunda wa Ngome kushoto akipigwa konde na Mohamed Chibumbui wa Magereza wakati wa mpambano wa Klabu bingwa Kidunda alishinda kwa K,O raundi ya kwanza Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Selemani Kidunda wa Ngome kushoto akipigwa konde na Mohamed Chibumbui wa Magereza wakati wa mpambano wa Klabu bingwa Kidunda alishinda kwa K,O raundi ya kwanza Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Selemani Kidunda akikimbilia kona Nyeupe baada ya kumkalisha chini Mohamed Chibumbui kwa konde zito wakati wa mchuano wa Klabu Bingwa TAIFA iliyofanyika uwanja wa ndani wa Taifa Kidunda alishinda  K,O raundi ya kwanza Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Selemani Kidunda akikimbilia kona Nyeupe baada ya kumkalisha chini Mohamed Chibumbui kwa konde zito wakati wa mchuano wa Klabu Bingwa TAIFA iliyofanyika uwanja wa ndani wa Taifa Kidunda alishinda  K,O raundi ya kwanza Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

SIKU YA VALENTINE DAY DODOMA TUMEWAANDALI UZINDUZI WA FILAMU YA KUSISIMUA: KUTOKA KWA EFRANCIA WA MAISHA PLUS



WAKAZI WA DODOMA JIANDAENI VEMA SIKU YA VALENTINE DAY: TUMEWAANDALIA BONGE LA SHOO LA UZINDUZI WA MOVIE YA  EFRANCYA ,ALL EYE'S ON ME:SHILOLE NDANI YA NYMBA PAMOJA NA WASANII WACHEKESHAJI KIBAO:NA PIA SURPRISE KIBAO ZITAKUWEPO , VILE VILE  WALE WATAOTUPIA PAMBA NA KUPENDEZA ZAIDI WAJIANDAE KWA ZAWADI KIBAO:

RAIS KIKWETE AKAMILISHA USAJILI WA KITAMBULISHO CHA TAIFA



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitia saini baada ya  kuthibitisha maelezo yake binafsi kwenye Fomu ya Kitambulisho cha Taifa wakati alipokamilisha taratibu za kupatiwa Kitambulisho hicho  nyumbani kwake jijini Dar es salaam  leo, Ijumaa, Februari Mosi, 2013. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Bwana Dickson E Maimu.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha kwa ajili ya Kitambulisho cha Taifa wakati alipokamilisha taratibu za kupatiwa Kitambulisho cha Taifa nyumbani kwake asubuhi ya leo, Ijumaa, Februari Mosi, 2013.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitia saini Kitabulisho cha Taifa wakati alipokamilisha taratibu za kupatiwa Kitambulisho cha Taifa nyumbani kwake asubuhi ya leo, Ijumaa, Februari Mosi, 2013. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Bwana Dickson E Maimu.

FECAFOOT YATAJA NYOTA WAKE 21, ETO’O NDANI



 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Cameroon (FECAFOOT) limetaja msafara wake wa watu 36 wakiwemo wachezaji 21 wa timu yao ya Taifa Indomitable Lions) wakiongozwa na nahodha Samuel Et’oo Fils kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumatano.
Kiongozi wa msafara wa timu hiyo itakayoanza kuingia nchini keshokutwa (Februari 3 mwaka huu) ni Mwakilishi wa Serikali ya Cameroon, Dieudone Wassi. Naibu kiongozi wa msafara wa Cameroon itakayofikia hoteli ya New Africa ni Makamu wa Rais wa FECAFOOT, John Ndeh.
Mbali ya Et’oo, wachezaji wengine waliomo kwenye msafara huo ni Charles Itandje, Benoit Assou Ekoto, Jehu Rustand Youthe (Union Douala), Fabrice Olinga Essono, Allam Nyam, Bouba Aminou, Benoit Angwa, Herve Tchami, Henri Bedimo, Nicolas Nkoulou, Jean Makoun, Jean Kana Biyick, Joel Matip, Vincent Aboubakar, Alexandre Song, landre Nguemo, Pierre Wome, Jean Nyontcha, Achille Emana na Charles Eloundou.
Wengine ni Andre Nguidljol Nlend (Mkurugenzi wa Utawala FECAFOOT), Jean Paul Akono (Kocha Mkuu), Martin Ndtouungou Mpile (Kocha Msaidizi), Jacque Songo’O (Kocha wa makipa), Dk. Baoubakary Sidiki (Daktari wa Timu) na Emmanuel Francis Ambane (Psychologist).
Pia wapo Tchonkontey Monkam (Fitness Trainer), Rigobert Song (Meneja wa Timu), Aoudou Mvotoung (Team Security), Fouda pascal Linus (Ofisa Habari FECAFOOT), Boubakar Ndou (Meneja Vifaa), Daniel Tcheuffa Tecky (Physiotherapist), Elias Kalaguem (Physiotherapist) na Justin Addo (Wakala wa Mechi).
Wakati huo huo, kikosi cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kitaingia kambini kesho jioni (Februari 2 mwaka huu) kwenye hoteli ya Tansoma.
KUONA TAIFA STARS, CAMEROON 5,000/-
Kiingilio cha chini kwenye mechi ya FIFA Date kati ya Taifa Stars na Cameroon itakayochezwa Jumatano (Februari 6 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa ni sh. 5,000 kwa viti vya kijani.
Viti vya bluu ni sh. 7,000 wakati viti vya rangi ya chungwa itakuwa sh. 10,000. Kwa viti vya VIP viingilio ni kama ifuatavyo; VIP C sh. 15,000, VIP B sh. 20,000 na VIP A sh. 30,000.
Tiketi zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohia/Samora, kituo cha mafuta OilCom Ubungo, Dar Live Mbagala na kituo cha mafuta Buguruni.