Shirikisho
la Mpira wa Miguu Cameroon (FECAFOOT) limetaja msafara wake wa watu 36
wakiwemo wachezaji 21 wa timu yao ya Taifa Indomitable Lions)
wakiongozwa na nahodha Samuel Et’oo Fils kwa ajili ya mechi dhidi ya
Taifa Stars itakayochezwa Jumatano.
Kiongozi
wa msafara wa timu hiyo itakayoanza kuingia nchini keshokutwa (Februari
3 mwaka huu) ni Mwakilishi wa Serikali ya Cameroon, Dieudone Wassi.
Naibu kiongozi wa msafara wa Cameroon itakayofikia hoteli ya New Africa
ni Makamu wa Rais wa FECAFOOT, John Ndeh.
Mbali
ya Et’oo, wachezaji wengine waliomo kwenye msafara huo ni Charles
Itandje, Benoit Assou Ekoto, Jehu Rustand Youthe (Union Douala), Fabrice
Olinga Essono, Allam Nyam, Bouba Aminou, Benoit Angwa, Herve Tchami,
Henri Bedimo, Nicolas Nkoulou, Jean Makoun, Jean Kana Biyick, Joel
Matip, Vincent Aboubakar, Alexandre Song, landre Nguemo, Pierre Wome,
Jean Nyontcha, Achille Emana na Charles Eloundou.
Wengine
ni Andre Nguidljol Nlend (Mkurugenzi wa Utawala FECAFOOT), Jean Paul
Akono (Kocha Mkuu), Martin Ndtouungou Mpile (Kocha Msaidizi), Jacque
Songo’O (Kocha wa makipa), Dk. Baoubakary Sidiki (Daktari wa Timu) na
Emmanuel Francis Ambane (Psychologist).
Pia
wapo Tchonkontey Monkam (Fitness Trainer), Rigobert Song (Meneja wa
Timu), Aoudou Mvotoung (Team Security), Fouda pascal Linus (Ofisa Habari
FECAFOOT), Boubakar Ndou (Meneja Vifaa), Daniel Tcheuffa Tecky
(Physiotherapist), Elias Kalaguem (Physiotherapist) na Justin Addo
(Wakala wa Mechi).
Wakati
huo huo, kikosi cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium
Lager kitaingia kambini kesho jioni (Februari 2 mwaka huu) kwenye hoteli
ya Tansoma.
KUONA TAIFA STARS, CAMEROON 5,000/-
Kiingilio
cha chini kwenye mechi ya FIFA Date kati ya Taifa Stars na Cameroon
itakayochezwa Jumatano (Februari 6 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam kitakuwa ni sh. 5,000 kwa viti vya kijani.
Viti
vya bluu ni sh. 7,000 wakati viti vya rangi ya chungwa itakuwa sh.
10,000. Kwa viti vya VIP viingilio ni kama ifuatavyo; VIP C sh. 15,000,
VIP B sh. 20,000 na VIP A sh. 30,000.
Tiketi
zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo katika vituo vya Shule ya
Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko Mtaa
wa Ohia/Samora, kituo cha mafuta OilCom Ubungo, Dar Live Mbagala na
kituo cha mafuta Buguruni.
No comments :
Post a Comment