Kamati ya uchaguzi ya shirikisho la soka nchini imesitisha zoezi la uchaguzi wa shirikisho hilo kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni matatizo ya kikanuni.
Akitangaza
kusitisha zoezi hilo mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Deogratius Lyato
amesema kamati yake imepitia mchakato mzima wa uchaguzi wa shirikisho la soka nchini TFF na uchaguzi wa Tanzania Premier League Board(TPL Board) ili kujiridhisha kuwa mchakato mzima wa uchaguzi unakidhi kikamilifu matakwa ya kanuni za uchaguzi na katiba TFF.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF imebaini kuwa kuna matatizo ya kikanuni ambayo yanapaswa kuzingatiwa kwanza kabla ya kuendelea na mchakato wa uchaguzi.
Lyato amesema amesema kamati ya uchaguzi ya shirikisho la mpira wa miguu Tanzania kwa mamlaka ilinayo kwa mujibu wa Ibara ya 10(5) ya kanuni za Uchaguzi za TFF INASITISHA zoezi la uchaguzi wa Tanzania Primier League Board(TPL Board) na uchaguzi wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF hadi hapo matatizo hayo ya kikanuni yatakapopata utatuzi.
Pia Lyato amesema kamati yake ya uchaguzi itawatangazia baadae tarehe mpya za uchaguzi wa Tanzania Premier League Board(TPL Board) na shirikisho la mpira wa miguu Tanzania(TFF)
Kwa maana hiyo ni kwamba mchakato wa kampeni uliokuwa uanze kesho kwa mujibu wa kanuni ambayo inataka kampeni kufanyika katika kipindi cha siku tano sasa hautakuwepo tena.
No comments :
Post a Comment