Movie
mpya ya Msanii wa kuigiza sauti za Viongozi Stive Nyerere, iliyokuwa
ianze kurekodiwa leo imeingia dosari baada ya msanii huyo kupata ajali
na kuswekwa lupango katika kituo cha Polisi cha Mabatini, asubuhi hii.
Msanii
huyo amepata ajali hiyo maeneo ya karibu kabisa na kituo cha Mabatini,
wakati akiwa na msafara wa wasanii wenzake wanaoshiriki katika Movie
hoyo, wakati wakielekea kuanza kurekodi.
Wasanii
hao pamoja na Stive, walikuwa wakitokea katika Kambi yao iliyokuwa
maalum kwa maandalizi ya kuanza kurekodi ikiwa ni pamoja na kufanyia
mazoezi katika kambi hiyo iliyodumu kwa wiki kadhaa.
Ajali
hiyo ilikuwa kama hivi:- Wakati Stive akiwa na baadhi ya washiriki wa
movie yake katika gari lake na wakiwa katika mwendo kuelekea eneo la
kushuti sini zao, ghafla aliona gari aina ya funcargo ikiwa imesimama
mbele yake huku katikati ya barabara akiwapo jamaa aliyekuwa
akisimamisha magari katika eneo hilo.
Baada ya kushindwa kusimama kwa ghafla ndipo alipoigonga gari hiyo kwa nyuma na gari hiyo kutumbukia mtaroni.
Mashuhuda
wa ajali hiyo walieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni Fundi umeme
aliyekuwa akisimamisha magari katika eneo hilo ili kuweza kuondoa waya
wa Umeme uliokatika na kulala katikati ya barabara huku ukiwa na moto,
ili kuepusha madhara zaidi.
Baada
ya ajali hiyo, walifika askari Polisi wakiambatana na askari wa usalama
barabarani, ambapo alianza kupima ajali hiyo huku madereva wakijibizana
na fundi aliyesimamisha magari, ambapo majibizano hayo yaliingiliwa
kati na mmoja kati ya askari waliofika eneo hilo.
Katika
majibizano hayo baina ya fundi, Askari na madereva wote wawili, ndipo
kulitokea kupishana kauli baina ya Stive na Askari huyo, aliyediriki
kumuita Stive mjinga, ambapo Stive alishindwa kuvumilia na kuamua
kumjibu na ndipo alipokunjwa 'Tanganyika Jeki' na kukokotwa hadi katika
gari walilokuja nalo askari hao na kumpakia na kisha kuondoka naye
kuelekea katika Kituo cha Mabatini.
Eneo la tukio la ajali hiyo.
Mashuhuda wakishuhudia ajali hiyo, gari likiwa mtaroni.
Kushoto
ni gari ya Stive yenye namba za usajiri T 779 BZL na (kulia) ni gari
lililohusika na ajali hiyo lenye namba za usajiri T 584 BQV.
Huu ndiyo waya wa umeme uliosababisha ajali hiyo.
Askari wa usalama barabarani, akipima ajali hiyo.
Askari akimkunja Stive na kumpakia katika gari lao ili kuondoka naye kumpeleka kituoni Mabatini.
Gari la Stive likiwa limebondeka kwa mbele lilikogongana na gari jingine.
Gari husika na ajali likiwa limetumbukia mtaroni.
Baadhi
ya warembo walikuwa na Stive katika gari lake ambao ni miongoni mwa
washiriki wa Movie hiyo, wakiwa eneo la tukio. ICHA ZAIDI http://www.sufianimafoto.com/
No comments :
Post a Comment