Na Bryceson Mathias
Ubabe
wa Naibu Spika Job Ndugai hivi karibuni ulibadilika na kusubiri hadi
akatoa Kauli na kuwaambia wananchi akisema, “Watanzania jioneeeni utovu
wa nidhamu unaofanywa waziwazi”..alisema Ndugai.
Baada
ya kusema hayo, Naibu Spika aliposema hivyo alinyamaza akisema waachwe
waendelee kupiga kelee hadi wanyamaze ndipo kikao kiendelee, ambapo
haikusaidia hadi Mwanasheria wa Serikali Fredrick Werema aliposimama
kuokoa Jahazi lakini hakufua Dafu.
Wapenda
Haki, Wakristo na wasomaji wa Biblia Takatifu isiyo na uongo kama
walivyo baadhi ya wawakilishi wetu walimo bungeni! katika Mithali 14:34
inasema, “ Haki huinua taifa; Bali dhambi ni aibu ya watu wote”.
‘Kila siku
inapokuwepo Haki, Taifa huinuliwa, na ndiyo maana katika enzi ya Mwalimu
Taifa liliinuliwa kufikia kuitwa Tanzania ni Kisiwa cha Amani. Lakini
Haki inapokosekana, hapo ndipo Dhambi huinuka aibu na utovu ukiasisiwa
na wanaoongoza, na kupelekea Utovu wa nidhamu’.
Mstari unaofuata- Mithali 34: 35 ambao hata Ndugai kwa kuwa ni Mkristo amejifunza unasema, “Upendeleo wa mfalme humwelekea mtumwa atendaye kwa busara; Bali ghadhabu yake itakuwa juu yake aletaye aibu.
Ninachotaka
niseme bila kumung’unya maneno, kwa Mtazamo wangu! Naona kila
kunapotokea Malumbano ya wabunge bungeni, mara nyingi hutokea akiwepo
Ndugai kwenye kiti, hii ina maana Upendeleo wake unawaelekea watumwa
watendao bila busara!.
Kwa
msingi huo inaonesha gadhabu yake saa zote inakuwa juu yao waletao hoka
zenye werevu! Na kwa kuwa sasa hakuna mtanzania atakayekula mlenda
halafu akadanganywa mlenda huo ni nyama, hawakai kimya tuu!! Bali
wanamuomba Mungu wao ili haki ipatikane na ndipo vurugu hutokea.
Bunge
lililopita vurugu na utovu wa nidhamu ulipotokea Ndugai ulikuwa kwenye
Kiti, Safari hii tena Utovu wa Nidhamu ambao ulikuwa unaomba watanzania
wauone umetokea wewe ukiwa kwenye Kiti, sasa itafika watanzania
watajiuliza kwani ukiwepo wewe kwenye kiti kunakuwa na vurugu?
Ni
rai yangu kukikumbusha Kiti cha Spika kwamba!! Kwa upendeleo huo
mnakotupeleka sasa mkiwa mmekalia Kigoda hicho, ni kwenye kisiwa cha
Migogoro, Vurugu na ukosefu wa Nidhamu uliokithiri, nawataka waelewe wao
ni vijana wa Juzi, sasa Vijana wa Jana na wa Leo wanajifunza
mnachofanya kwa upendeleo; hivyo nao watafanya, muone mkiwa na
mikongojo.
Kama
Ndugai anataka watanzania waone utovu wa nidhamu unaofanywa na wabunge
bungeni, basi watanzania aelewe pia watanzania waona Upendeleo na Ubabe
unaofanywa na kiti chake katika kujadili hoja ambazo saa nyingine
zingine zinapingwa kwa kulidumaza Taifa badala ya kuliinua.
Ieleweke
kwamba, Mtanzania wa leo huwezi ukamuonyesha mtu aliyevaa nguo ya
Kaniki, akavaa kofia ya Majani, Klauni ya Lakiri na Mkanda wa Kamba za
Mgomba, Viatu vya Magurudumu ya Gari na Fimbo ya Unyasi, ukamwambia huyu
ni Askari halafu akakubali! Atakataa.
Ni
Busara yangu kumshauri Spika Makinda na Naibu wake, waone umuhimu wa
kuwatendea haki kwa sababu hata Baba na Mama wa Familia akianza
kuwabagua watoto kwa Jinsia na Uzaliwa wao, kuwa huyu ni mwembamba,
Mfupi, Mnene, Mlemavu au Mzima, utakuwa Ubaguzi.
Nzi
ni mdudu mchafu, lakini kuna mambo mazuri tunaweza kujifunza kwake. Nzi
akitua popote, huanza kuchezesha miguu yake yake kwenda mbele na nyuma,
na baadaye ya nyuma, na hatima mbawa za kushoto na kulia!! watalaam wa
viumbe wanasema, Nzi huwa anasema, kama unajua ya mbele, yeye anajua ya
nyuma, na kama unajua ya nyuma, yeye anajua ya Mbele.
Hitimisho
la Ishara na Maelezo yake, wanadai husema kama unajua ya Unaba wa
kushoto, yeye anajua ya ubawa wa kulia, na kama unajua ya ubawa wa
kushoto, yeye huweza akaruka na kutoa kweye chakula chakula na kukuachia
uchafu na hatimae utaugua. Tujifunze na kukubali kushauriwa, badala ya
kubisha tuu na kutumia ubabe wa kiti hata kwenye hoja za kweli na msingi
kama za akina James Mbatia-NCCR Mageuzi.
Aidha
nimepata faraja kwa Kauli ya Ndugai ambayo amesema atamshauri Mkuu wa
Kiti Anne Makinda ili aone utaratibu wa kutoa nafasi sawia za kuchangia
toka kwa Wabunge wa Chama Tawala na wale wa Upinzani. Ikifanywa hivyo
hapo ndipo Haki huinua Taifa.
Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa
0715-933308
No comments :
Post a Comment