Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi (hayupo pichani) akiwaongoza wageni waalikwa wakati akipokea magari mawili maalumu ya kusafirishia dawa. |
Mfanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD), akionesha jinsi ya kubeba dawa ndani ya bohari hiyo kwa kutumia toroli maalumu. |
Dereva wa Bohari ya Dawa (MSD), akionesha jinsi ya kubeba dawa ndani ya bohari hiyo kwa kutumia foku lifti. |
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi (katikati), akiwa na viongozi mbalimbali kwenye hafla hiyo |
Wafanyakazi wa Bohari ya Madawa (MSD), wakiwa kwenye hafla hiyo |
Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dk.Donan Mmbando akihutubia kwenye sherehe hiyo.
Na Dotto Mwaibale
RAIS Jakaya Kikwete ameiagiza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Jeshi la Polisi
nchini kufanya msako na kuwafichua watu wote watakaopatikana na dawa za Serikali
katika maduka binafsi.
Maagizo hayo ylitolewa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii kwa niaba ya Rais Kikwete ambaye angekuwa mgeni rasmi kwenye
sherehe za ufunguzi wa ghala la kisasa la kuhifadhia dawa katika Makao Makuu ya Bohari ya
Dawa jijini Dar es Salaam leo.
"Natambua kuwa lipo tatizo la dawa na vifaa tiba vya serikali kupatikana katika maduka ya dawa ya watu binafsi jambo ambalo linanikera sana nawaagizeni wachukukieni hatua za kisheria wale wote watakao patikana na dawa hizo" alisema Rais Kikwete. Alisema Serikali haiwezi kuendelea kununua dawa kwa dharama kubwa na zikaishia katika mifuko ya watu wachache badala ya wananchi walio wengi hususani wa vijijini. Alisema Bohari ya dawa iliundwa mwaka 1994, ikiwa nadira ya kufikisha dawa na vifaa tiba karibu na wananchi ambapo tumeambiwa kuwa shughuli za MSD zimepanuka sana hususani uwezo wa maghala umefikia mita za mraba 51,800 na nusu ya hizo ni za kukodisha kwa watu binafsi.
"Natambua kuwa gharama za ukodishaji wa magahala ni kubwa sana na ni vema MSD
ikawa na maeneo yake yenyewe bila kutegemea maghala binafsi" alisema Rais Kikwete.
Rais Kikwete alizielekeza Halmashauri husika katika kanda za MSD kuisaidia Bohari ya
dawa kupata maeneo mkakati ya uhifadhi wa dawa na maeneo waliyonayo tayari
yaweze kupewa haki miliki. Alisema chanjo ni hatua muhimu kwa ajili ya ya afya
za mama na mtoto ambapo mpango wa taifa wa chanjo ulianza mwaka 1975 ukiwa unatoa
chanjo dhidi ya magonjwa kama Kifua Kikuu, Polia, Surua, Dondakoo, kifaduro na
Pepo Punda. Alisema magonjwa mengine yaliyongezeka ni kinga
dhidi ya Homa ya Ini, Homa ua Uti wa mgongo, nimonia na kinga dhidi ya magonjwa
ya kuhara. Rais Kikwete aliongeza kuwa kinga ni haki ya kila
mtoto hivyo mahitaji ya chanajo yamekuwa yanaongezeka kwaka hadi mwaka
kutokana na ongezeko la idadi ya watu. "Ongezeko la idadi ya chanjo pamoja na ongezeko
la aina za chanjo imesababisha kuwa na hitaji kubwa la maeneo ya kuhifadhi chanjo na kuzisambaza" alisema Kikwete. Alisema Utunzaji wa chanjo unahitaji mfumo wa
mnyororo baridi hivyo kuhitaji vyumba maalumu vyenye ubaridi, pamoja na gari lenye
vifaa vya kutunza ubaridi huo ili
kuhakikisha mnyororo baridi. Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein
Mwinyi alisema ufunguzi wa gahala hilo ni sehemu ya kutekeleza mpango mkakati wa MSD wa
kuhakikisha upatikanaji wa dawa
na vifaa tiba vyenye ubora unaokubalika na kwa bei nafuu. "Mpango huu umeandaliwa kwa kuzingatia Sera ya Afya ya kufikisha huduma bora za afya kwa kila Mtanzania" alisema Mwinyi.
Alisema vyumba vya kuhifadhia chanjo na magari maalumu ya kusafirishia chanjo
uliozinduliwa vitasaidia katika kutunza na kusafirisha chanjo katika hali ya ubaridi kwa
mujibu wa miongozo ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) ambayo Tanzania inatekeleza.
Alisema ghala hilo linauwezo wa kuhifadhi dawa na vifaa tiba lina mita za mraba 4,280
na kuwa limejengwa kwa msaada wa Serikali ya Marekani na Mfuko wa Dunia wa
Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu, Malaria na limegharimu jumla ya Dola za Marekani
milioni 4 sawa na takribani sh.bilioni 6.4 za Kitanzania. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani alisema ujenzi wa ghala hilo ni matunda yaliyotokana na
safari za Rais Kikwete nje ya nchi hususan Marekani ambapo mei 2 mwaka 2009 akiwa katika
ziara nchini Marekani Rais wa nchi hiyo Barack Obama aliahidi kuendelea kutoa
misaada katika maeneo mbalimbali likiwemo la kuboresha huduma za kupambana na
maradhi ya Ukimwi kupitia shirika la PEPFAR.
Alisema moja ya miradi inayoratibiwa na PEPFAR ni ujenzi wa maghala makubwa katika
kanda za Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya, Tanga na Tabora. Mwaifwani alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais Kikwete kwani matokeo ya juhudi zake zimeleta matunda ambayo yanaonekana kwa Taifa. Alisema ukamilishwaji wa miradi hiyo utaisaidia Bohari ya Dawa kukomboa jumla ya
shilingi za Tanzania bilioni 1 katika mwaka ujao wa fedha ambazo wamekuwa wakilipa
kwa ajili ya kukodi maghala ya watu binafsi kwa ajili ya kuhifadhi dawa, vifaa tiba na
vitendanishi kabla ya kusambazwa kwa walengwa. Alisema Bohari ya Dawa imeendelea kutekeleza jukumu lake la msingi la kusambaza dawa na vifaa tiba katika vituo vya afya hapa nchini
kwa niaba ya Serikali. Aliongeza kuwa katika kutekeleza majukumu hayo
Bohari ya Dawa imefanikiwa kufanikisha upatikanaji wa dawa ambapo imefikia
kati ya asilimia 70 hadi 75 ya mahitaji dhidi ya asilimia 44 wakati Taasisi hiyo ilipo
anzishwa mwaka 1994.
Alisema mikoa 10 imeingizwa katika mfumo wa
kufikisha dawa moja kwa moja hadi vituo vya afya na mikakati imewekwa ya kuingiza
mikoa yote ya Tanzania katika mfumo huo kuanzia julai 2013 na kuwa mkakati huu unazihusu pia hospitali za Wilaya, Mikoa na Hospitali za Rufaa. Mwaifwani alisema MSD imefungua mfumo
mpya wa kisasa wa TEHAMA (EPICOR) ili kurahisisha shughuli za usambaji ambao pia umefadhiliwa na USAID.
kufikisha dawa moja kwa moja hadi vituo vya afya na mikakati imewekwa ya kuingiza
mikoa yote ya Tanzania katika mfumo huo kuanzia julai 2013 na kuwa mkakati huu unazihusu pia hospitali za Wilaya, Mikoa na Hospitali za Rufaa. Mwaifwani alisema MSD imefungua mfumo
mpya wa kisasa wa TEHAMA (EPICOR) ili kurahisisha shughuli za usambaji ambao pia umefadhiliwa na USAID.
No comments :
Post a Comment