Walter Chilambo akipagawisha |
Shabiki wa kike akijiachia kwa Wababa |
Na Princess Asia
WASANII
wa Muziki wa Kizazi Kipya walioshiriki shindano la kuimba la Epiq Bongo
Star Search, Norman, Husna, Menina, Wababa, Geofrey na Walter jana
walionyesha wao ni moto wa kuotea mbali baada ya kuwapagawisha mashabiki
zaidi ya elfu tatu waliohudhuria katika ukumbi wa Club Maisha Dodoma.
Show
hiyo kali ilianza majira ya saa tano usiku, kwa mkali kutoka THT Ali
Nipishe anayetamba na kibao chake cha ‘MY’, na baadaye kumtambulisha
Norman Severino ambaye kwa mara ya kwanza alizindua wimbo wake wa ‘Si
Wewe’.
Steji
ilizidi kuwaka moto pale kijana tokea Dodoma, Godfrey Levis alipopanda
kuimba wimbo wake wa ‘MAYA’ na kufuatiwa na malkia kutoka THT, Linah,
aliyeimba nyimbo zake zote kali.
Lakini
alikuwa ni mwanadada, Nsami aliyeonyesha kwamba wanawake waliopo kwenye
tasnia wajipange alipopanda kuimba wimbo wa ‘MUONGO’ na hatimaye mdada
wa taarab, Husna akawamaliza wanadodoma kwa kuimba wimbo wake wa
‘Nawamimina’, huku akisifiwa na wengi kwa uwezo wake mkubwa wa
kulimiliki jukwaa.
Kama
hiyo haitoshi, mashabiki pia waliburudishwa vya kutosha na mwimbaji
bora wa kiume wa mwaka, Barnaba, ambaye aliiimba nyimbo zake kama
Magubegube na Sorry, ambao unafanya vizuri sana sasa hivi na kuwafanya
mashabiki kupiga kelele kwa kumshangilia.
Ukumbi
ulizidi kulipuka kwa mayowe baada ya Barnaba kumtambulisha mwanadada
mwingine, Menina, ambaye wimbo wake wa Dream tonight unafanya vizuri
kwenye vyomba vya habari hapa nchini. Menina, ambaye alimsaidia Barnaba
kuitikia wimbo wake wa Wrong Number, alionyesha uwezo mkubwa katika
kumiliki jukwaa.
Hadi
wakati mshindi wa tatu wa shindano la EBSS, Wababa Mtuka anapanda
jukwaani kuimba kibao chake cha ‘My Wife’ watu wa Dodoma walikuwa bado
wakishangilia namna alivoonyesha uwezo katika kuimba.
Wa
mwisho kabla ya mshindi wa milioni hamsini kupanda alikuwa ni Ben Paul,
ambaye aliwakonga nyoyo mashabiki wake kwa nyimbo zake kali kama Pete
na Samboira kabla ya kumkaribisha jukwaani Walter.
Mashabiki
hao waliokuwa wakimsubiri kwa hamu, walianza kupiga kelele Walter
Walter, kabla ya kuwatuliza kwa kuimba wimbo wake mpya wa ‘Siachi’
akifuatiwa wimbo wake mwingine wa ‘Mamy Love’ ambao aliutoa kama zawadi
kwa mashabiki zake wa Dodoma.
Walter
alipata wakati mgumu jukwaani ambapo mashabiki walimuomba azirudie
nyimbo zake zaidi ya mara tatu hali iliyoonyesha kukubalika kwa hali ya
juu.
Mashabiki wengi wakizungumza baada ya burudani hiyo walionyesha kuwakubali vilivyo wasanii wa EBSS, huku wakiwatabiria makubwa.
‘Hakika
vijana wana vipaji na wanajua hasa kutoa burudani, wakipewa sapoti
watafika mbali sana’ alisema Maliki Abdul mkazi wa Dodoma aliyehudhuria
burudani hiyo.
Ziara hiyo ya washindi wa Epiq BSS inaelekea Dar mwisho wa mwezi huu kabla ya kuelekea Mtwara.
No comments :
Post a Comment