Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya
Habari Bw. Raphael Hokororo akiwafundisha maafisa habari na mawasiliano
wa serikali kutoka Wizara, Taasisi, wakala, mashirika ya Umma, mikoa na
wilaya upigaji wa picha bora za mnato kwa matumizi ya habari wakati
wa kuhitimisha kikao cha maafisa hao mjini Dodoma.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Clement Mshana ambaye alikua miongoni mwa
waalikwa waliohudhuria kikao kazi cha maafisa habari na mawasiliano wa
serikali akiongea na mafiasa hao mjini Dodoma.
Maafisa Habari na Mawasiliano wa
Serikali wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania mjini Dodoma kufuatia mwaliko wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Anne Makinda na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Dkt. Fenella Mukangara.
Maafisa habari na mawasiliano wa
serikali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutoka nje ya
Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Baadhi ya viongozi wa Idara ya
Habari (MAELEZO), Mkurugenzi wa Idara hiyo Bw. Assah Mwambene (wa nne
kutoka kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Usajili wa
Magazeti Bw. Raphael Hokororo (wa pili kutoka kushoto) wakiwa wamesimama
ndani ya ukumbi wa Bunge kuwasalimia waheshimiwa wabunge mara baada ya
kuombwa na Mh. Spika wakiwaongoza maafisa habari wa serikali.
Maafisa Habari na Mawasiliano wa
serikali wakiwasili Chuo Kikuu cha Dodoma kushiriki zoezi la upandaji wa
miti chuoni hapo ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika kuhifadhi
mazingira ya chuo hicho.
Mhasibu mkuu msaidizi wa Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Swalehe Chondoma akishiriki
zoezi la upandaji wa miti katika kampasi ya chuo kikuu cha Dodoma.
Naibu katibu mkuu wa Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akizindua zoezi
la upandaji wa miti lililowahusisha mafisa habari wa Serikali katika
kampasi ya chuo kikuu Dodoma.
Maafisa habari na Mawasiliano wa Serikali wakiendelea na zoezi hilo Chuo kikuu cha Dodoma.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
No comments :
Post a Comment