Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Monday, February 11, 2013

TTCL YAUNGANISHA OFISI ZA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI NA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO




 MAKABIDHIANO: Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Ludovick Utoh (kushoto) akipokea mkataba wa kumalizika kwa mradi  wa awamu ya kwanza wa vituo 11 kutoka kwa Mkuu wa Mauzo kutoka Kampuni ya SimuTanzania (TTCL), Bw. Tambwe Kisamba.
 Baadhi ya wafanyakazi wa TTCL  na NAO wakimsikiliza Bw. Utoh
 Wafanyakazi wa Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).
 DAR ES SALAAM,Tanzania

Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) imekabidhi vituo 11 vilivyounganishwa na mkongo wa taifa kwa mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali uliogharimu shilingi milioni 477.

Akiongea katika halfa hiyo mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali Bw. Ludovick Utoh ameishukuru TTCL kwa kukamilisha awamu ya kwanza ya mradi huo, na kuongeza kuwa uwepo wa mawasiliano hayo kutasaidia ofisi zote za mkaguzi wa hesabu za serikali kuwa salama zaidi na kutaongeza uadilifu kwani watakuwa na uwezo wa kuzuia tovuti ambazo hazina manufaa katika utendaji wa kazi.

Aliongeza kuwa, faida nyingine ya mawasiliano hayo kutawawezesha kuanzisha mawasiliano ya ndani "intranet" hivi karibuni baada ya kupata mtandao wa uhakika kutoka TTCL, pia  kupunguza kazi za makaratasi kwani sasa watakuwa wanatumia zaidi barua pepe kuwasiliana badala ya kuandikiana ujumbe mfupi kwa njia ya karatasi, kuwa na uwezo kwa kupokea taarifa kutoka mikoa mbalimbali kwa njia ya mtandao badala ya mtu kusafiri kutoka mkoani kuleta ripoti Makao Makuu.


Naye Mkuu wa Mauzo kutoka Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Kisamba Tambwe amemuahidi Mkaguzi na Mdhibiti mkuu wa hesabu  za serikali kuwa, TTCL itakuwa bega kwa bega kuhakikisha inawasaidia pale watakapohitaji msaada kutoka TTCL na itawapa mafunzo watu wa ufundi kutoka Ofisi za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ili waweze kutatu a matatizo madogo madogo ya kiufundi endapo yatatokea

No comments :

Post a Comment