Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Monday, February 11, 2013

CCM YAFANYA UCHAGUZI WA KAMATI KUU MJINI DODOMA LEO




Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete. akipiga kura, wakati wa uchaguzi wa Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM uliofanywa na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, jioni yaleo, wakati wa Kikao cha NEC kilichofanyika katika ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. 
 Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha NEC kwa kuendelea na semina, leo kwenye Ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na Kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha NEC kwa semina iliyoanza jana, na kuendelea leo kwenye ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma. Pamoja naye ni Dk. Sheni na Kinana
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishauriana jambo na Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Zakia Meghji, kabla ya kuanza kikao hicho leo.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisahuriana jambo ukumbini na Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Zakia Meghji na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, kabla ya kikao kuanza leo
 Mjumbe wa NEC, Mama Salma Kikwete akimsalimia Katibu wa NEC Siasa ana Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro kabla ya kikao kuanza ukumbini. Katikati ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
 Hali ndani ya ukumbi ilikuwa kama hivi kabla ya kikao kuanza. Kushoto Kabisa ni Nape na Zakia Meghji na juu-kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisalimia wajumbe. Na Kulia chini ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Muhamed Seif Khatib na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai wakiteta jambo
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Vuai Ali Vuai kabla ya kikao kuanza  
 Wajumbe wa NEC  Profesa Anna Tibaijuka na Mzee Mtandika wakibadilishana mawazo ukumbini
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akichati jambona Mjumbe wa NEC, Samwel Sitta na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kabla ya kikao
 Nape (kulia) akichangia kwenye mazungumzo hayo kati yake na Dk. Asha-Rose na Sitta
Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, ambaye sasa ni Mjumbe wa NEC, William Mukama akibadilishana mawazo na mjumbe mwenzake wa NEC Profesa Juma Kapuya ukumbini
 Hii ndiyo Sekretarieti inayofuatilia na kuweka kumbukumbu ya mijadala inayozungumzwa kwenye mkutano huo
Mjumbe wa NEC, Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe akiteta jambo na Mzee Mtandika
 Katibu Mkuu wa UWT, Sophia Simba akijadiliana jambo wa Wajumbe wenzake wa NEC ukumbini. Kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuia hiyo Ana Makilagi.
 Dk. Asha-Rose Migiro akishauriana jambo na Nape
 TUKIFANYA HIVI MAMBO YATANYOOKA AU SIYO? Inaelekea ndivyo Dk. Asha-Rose Migiro alivyokuwa akisema kumwambia Nape katika mazungumzo yao ukumbi kabla ya kikao
 Katibu wa Oganaizesheni Dk. Muhammed Seif Khatib anaonekana kumuuliza Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai wakati wakibadilishana mawazo kabla ya kikao kuanza
 Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Taifa, Alhaj Abdallah Bulembo akiwasalimia wajumbe wenzake wa NEC ukumbini kabla ya kikao kuanza
 Wajumbe wakisubiri kwa hamu kikao kuanza
 Makamu wa Rais Dk. Muhammed Gharib Bilal (kulia) na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakiwa safu ya mbele na baadhi ya wajumbe kwenye kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe wakipitia nyaraka muhimu kabla ya kikao kuanza
Aliyekuwa Katibu wa NEC Oganaizesheni, Asha Abdallah Juma aka Mama Mshua (kulia) akimsalimia Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabiba nje ya ukumbi. Katikati ni Mwenyekiti wa UWT, Sophia Simba
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba anaonekana kumuuliza swali hilo Mjumbe wa NEC, aliyekuwa mbunge wa Igunga  Dk. Dalaly Kafumu walipokutana nje ya ukumbi kabla ya kikao kuanza
Kaim Katibu wa CCM wa mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda akiwa na Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, William Mukama nje ya Ukumbi. Sixtus amewahi kuwa Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Itikadi na Uenezi kabla ya kuhamishiwa Morogoro mwaka jana wakati Mukama akiwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa.
 CCM MAMBO SAFI TU! Mukama akimwambia Mjumbe wa NEC, Steven Wasira nje ya ukumbi
 Wajumbe wa NEC wakiangua kicheko cha kutaniana kaba la kuingia ukumbini. Kutoka kulia ni Dk. Rafael Chegeni, Januari Makamba, Halimenshi Mayonga na Samwel Sitta
Wajumbe wakiwa tayari kuingia ukumbini kuanza kikao leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

No comments :

Post a Comment