Mwakilishi wa
Extra Bongo, Super Nyamwela akimkabidhi fedha taslim sh 200,000 kwa
mwandishi wa Kampuni ya Free Media, Clezencia Tryphone 'Tasha' kwa
ajili ya maandalizi ya michunao ya NSSF Cup hafla hiyoilifanyika katika
ukumbi wa Meeda Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. (Picha na Habari
Mseto Blog)
Na Mwandishi Wetu
KATIKA hatua
zaidi za kufanikisha maandalizi ya michuano ya Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii(NSSF Cup), Bendi ya Muziki wa Dansi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’,
imedhamini katoni 33 za maji ya Kilimanjaro kwa timu ya wanawake ya Netboli ya
Free Media Queens.
Akikabidhi
udhamini huo wenye thamani ya sh 200,000, mwakilishi kutoka Extra Bongo Super
Nyamwela katika ukumbi wa Meeda jijini Dar es Salaam juzi usiku alisema, bendi
yao imeamasika mara baada ya Free Media Queens kuhitaji sapoti yao katika suala
muhimu la kimichezo.
Nae Mmiliki wa
bendi hiyo, Ally Choki alisema, sapoti hiyo wameitoa kwa moyo mkunjufu kutokana
na umuhimu wa michuano hiyo inayojenga afya zaidi na kudai kuwa, mara baada ya
kupata ombi hilo hakusita kusapoti.
“Michuano hii
ni mizuri sana, nawapongeza NSSF kwa kuona umuhimu wa waandishi kama mimi
nilivyoona na kutoa sapoti walau kidogo kwa timu hii ya Free Media Queens ili
iweze kufanya vema maandalizi yake,”alisema Choki.
Mbali na sapoti
hiyo, Choki ameitaka timu hiyo kujipanga kikamilifu ili iweze kufanya vema
katika michunao hiyo inayotarajia kuanza kutimua vumbi Machi 9 katika uwanja wa
TCC Chang’ombe pamoja na DUCE Jijini Dar es Salaam.
Michuano ya
NSSF, inashirikisha timu mbalimbali za wanahabari kutoka Bara na Visiwani,
ikiwa na lengo la kudumisha amani na undugu katika kazi.
Katika hatua
nyingine, Choki amewataka wasichana kujitokeza kwa wingi na kuchukua fomu za
kushiriki shindano la Kigoli wa Manywele linalotarajiwa kutimua vumbi hivi
karibuni, ambapo fomu za ushiriki zinaanza kutolewa leo katika ofisi za
Manywele na Extra Bongo.
“Wanadada
wakati ni wenu jitokezeni kwa wingi, kuchukua fomu zinazoanza wiki ijayo, ili
muweze kuibuka na gari la kisasa kwa mshindi wa kwanza, wa pili makochi na wa
tatu atapata zawadi kali ambayo nitaitoa mimi binafsi,”alibainisha Choki.
No comments :
Post a Comment