Mdau wa muziki wa dansi, Maimatha Jesse
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWANADADA machachari katika sekta ya utangazaji na udau wa
muziki, Maimatha Jesse, aliwaacha watu hoi kwa kuwatangazia watu kuwa waache
kumuangalia mara mbilimbili kwasababu nafasi zimeisha kwa kusema eti ameolewa.
Kauli hiyo iliwafanya watu waanguwe kicheko wakati mwanadada
huyo anazungumzia kuanzisha upya kwa shindano lake la Kigoli wa Extra Bongo na
Manywele mwaka 2013, ambalo hadi sasa mipango ya kulitangaza kwa wadau
inaendelea.
Huku akirembua macho yake na kubinua barabara mdomo mbele ya
hadhira ya waliohudhuria kikao hicho mchana wa leo, Maimatha alishindwa
kujizuia na kutamka kuwa yoyote anayemuangalia kwa matamanio ajuwe ameolewa.
“Jamani, ngojeni niwaangalie vizuri nyie wote lakini hadi
mwisho mjuwe nimeolewa,” alisema dada huyo ingawa pia hakusema yupo kwenye ndoa
na mtu gani.
Hata hivyo kauli kama hii, mwanadada huyo mwenye sura ya
mvuto, aliitoa kama sehemu ya kuchangamsha baraza na wala hakuwa na lengo la
kujitangaza kwa wadau waliokwenda kusikia kauli ya harakati za Kigoli, akiwa
sambamba na Mkurugenzi wa bendi ya Extra Bongo, Ally Choki, mwenye mipango ya
kuiweka juu zaidi bendi yake.
Katika kikao hicho, Choki pia alitumia fursa hiyo kumtangaza
repa Papy Catalogue, Adam Mbombole na Nadine Conpresor,
alijiunga na bendi hiyo akitokea Akudo Impact.
No comments :
Post a Comment