Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Saturday, February 9, 2013

MASHINDANO YA BODABODA CUP KINONDONI YAZIDI KUSHIKA KASI, TEGETA YAPIGWA 3-0 NA KAWE



k6 
Wachezaji wa timu za waendesha Bodaboda kutoka Tegeta na Kawe, wakichuana kuwania mpira wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Bodaboda 'Bodaboda Cup'  inayoendeshwa na Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani. Katika mchezo huo timu ya Kawe imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tegeta,  mchezo uliofanyika katika uwanja wa Tanganyika Pakers Kawe jijini Dar es salaam leo.

Mashindano hayo yanashirikisha timu za mkoa wa kipolisi wa Kinondoni ambazo zinatoka katika maeneo ya Kimara, Kawe, Tegeta, Mabibo na Ubungo, ambapo wachezaji washiriki wa mashindano hayo wanatakiwa kuwa ni waendesha pikipiki za kupakia abiria tu 'Booda'. Awamu ya kwanza ya ligi hiyo ilikuwa na timu 32 na sasa ni awamu ya pili ambapo timu 16 zinashindana ili kupata timu 8 zitakazoshiriki Ligi ya Nane Bora na hatimaye kupata mshindi wa mashindano hayo ya 'Kinondoni Bodaboda Cup'.

Lengo la Mashindano hayo ni kuwakutanisha waendesha Bodaboda wote wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni ili waweze kufahamiana wao kwa wao, lakini pia ili jeshi la polisi Kikosi cha Usalama Barabarani liweze kuwaelimisha juu ya sheria za usalama Barabarani na Ulinzi Shirikishi kwa jamii

No comments :

Post a Comment