Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Monday, February 4, 2013

TIKETI STARS, CAMEROON KUUZWA SIKU MOJA KABLA YA MECHI



Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Star)

TIKETI kwa ajili ya pambano la kimataifa la kirafiki kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Cameroon (Indomitable Lions) zinaanza kuuzwa kesho (Febaruari 5 mwaka huu) katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Viingilio katika pambano hilo litakalochezwa Jumatano (Februari 6 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11 jioni ni sh. 5,000 (viti vya kijani), sh. 7,000 (viti vya bluu), sh. 10,000 (viti vya rangi ya chungwa), sh. 15,000 VIP C, sh. 20,000 VIP B na sh. 30,000 VIP A.
Vituo vitakavyouzwa tiketi hizo kuanzia saa 2 asubuhi ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Samora/Ohio, Oilcom Ubungo, Dar Live Mbagala na kituo cha mafuta Buguruni.
Vilevile tiketi zitauzwa uwanjani siku ya mechi, na milango itafunguliwa saa 8 kamili mchana.
Wakati huo huo, kundi la kwanza na la pili la wachezaji wa Cameroon tayari limetua jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi dhidi ya Tanzania (Taifa Stars) itakayochezwa keshokutwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Cameroon chini ya Kocha Jean Paul Akono itafanya mazoezi kesho saa 11 jioni Uwanja wa Taifa. Nayo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager yenyewe itafanya mazoezi Uwanja wa Taifa leo saa 11 jioni.

Kikosi cha timu ya Taifa ya Cameroon (Indomitable Lions)

No comments :

Post a Comment