Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, wakati
alipowasili katika hafla ya ufunguzi wa mradi wa Upanuzi wa Barabara ya Kilwa,
eneo la Mbagala Rangi tatu leo. Katikati ni Waziri wa Ujenzi, Dkt.
John Pombe Magufuli.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza
jambo na kumpongeza Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, mara baada
ya balozi huyo kumaliza kusoma hotuba yake iliyochanganywa na Kiswahili, wakati
wa hafla ya ufunguzi wa mradi wa Upanuzi wa Barabara ya Kilwa, eneo la Mbagala
Rangi tatu leo. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe
Magufuli.
Balozi wa Japan Nchini Tanzania, Masaki Okada,
akishiriki kucheza sebene la bendi ya Msondo Ngoma na Vijana wa kikundi
cha uhamasishaji cha Temeke, wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya wanamuziki wa bendi ya Msondo Ngoma, wakishambulia jukwaa kutoa burudani wakati wa halfa hiyo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Balozi
wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, wakifunua kitambaa kwa pamoja ikiwa ni
ishara ya ufunguzi wa mradi wa Upanuzi wa Barabara ya Kilwa, eneo la Mbagala
Rangi tatu leo. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe
Magufuli.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Balozi
wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe
Magufuli na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (kushoto) wakishiriki kwa
pamoja kukata utepe ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa mradi wa Upanuzi wa Barabara
ya Kilwa, eneo la Mbagala Rangi tatu leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na baadhi ya Wazee wastaafu wa CCM, mara baada ya kumaliza kupiga
nao picha ya pamoja ya kumbukumbu wakati wa hafla ya ufunguzi wa mradi wa
Upanuzi wa Barabara ya Kilwa, eneo la Mbagala Rangi tatu leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana
na baadhi ya viongozi kutembea na kukagua sehemu ya Barabara ya Kilwa eneo la
Mbagala Rangi tatu, baada ya kufungua rasmi barabara hiyo iliyokamilika kwa Upanuzi
na ukarabati. (Picha na OMR)
No comments :
Post a Comment