Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, February 12, 2013

VYOU VIKUU VYA TANZANIA VYAAMBULIA MIKONO MITUPU MASHINDANO YA VYUO VIKUU VYA AFRIKA MASHARIKI YALIYOKUWA YAKIFANYIKA NCHINI



Mgeni rasmi Profesa Elifas Bisanda wa Chuo Kikuu Huria akitoa nasaha zake za kufunga mashindano ya vyuo vikuu vya Afrika Mashariki

Zaidi ya makombe 80 yalikabidhiwa washindi

Brass band ilikuwepo

Wanamichezo wa chuo kuikuu cha Kampala na baadhi ya lectures wao wakishangilia na makombe yao waliyotwaa. Chuo hiki kilitwaa makombe 15.

Mgeni rasmi Profesa Elifas Bisanda wa Chuo Kikuu Huria akimkabidhi Profesa Badru Kateregga wa chuo Kikuu cha Kampla kombe la mshindi wa kwanza wa mpira wa miguu.

Nahodha Okello Maxwell wa timu ya chuo kikuu cha biashara cha Makerere (Makerere University of Business School) akipokea kombe la mshindi wa pili kwa soka baada ya kufungwa na Kampala kwa penalti




Rais wa TOC Filbert Bayi akikabidhi kombe kwa timu ya  kuogolea


  Wakati Vyuo vya Uganda na Kenya vikiondoka na medali na makombe kibao vyuo vikuu vya Tanzania imeambulia mikono mitupu kwani ni Chuo Kikuu cha Mlima pekee kilichopata kombe kwa mchezo wa chess tena kwa nafasi ya tatu.

Tanzania ambayo ilikuwa wenyeji imetiaaibukwani pamoja na kuwa na vyuo vikuu vingi ni vyuo vikuu saba yt viliyoleta wawakilishi huku Kenya na Uganda wakileta vyuo 17 kila mmoja.

Zaizi ya makombe 80 yamekabidhiwa kwa washindi huku Chuo Kikuu cha Kampala na Ngejje wakitia fora kwa kuondoka na makombe mengi

Chuo Kikuu cha Kampala ambacho ndio mabingwa kwa mchezo wa soka kimechukuwa makombe 15 na mwakani mashindano ya vyuo Vikuu vya Afrika mashariki yatafanyika nchini Uganda.

Mshindi wa pili kwenye soka ni chuo kikuu cha biashara cha Makerere baada kufungwa na Chuo kikuu cha Kampala wenzao toka Uganda kwa penalti 4-5 baada ya kumaliza dakika 90 wakiwa hawajafungana ndipo zilipopigwa penalti ili apatikane mshindi.

Vyuo vikuu vyauganda vimefanya vizuri kwani ukiangalia kwenye miichezo kikapu, wavu, soka, handball  wanawake na wanaume wameingia fainali wenyewe.

No comments :

Post a Comment