Kama
majibu kwa ripoti za kupotosha za hivi karibuni katika vyombo vya
habari, David Lenigas, Mwenyekiti wa kampuni ya fastjet na Mwenyekiti wa
Five Forty Aviation Limited tawi la Kenya (“Fly540 Kenya”),
anathibitisha kuwa hakuna makubaliano yoyote halisi yanayohusu Leseni ya
Nembo, Makubaliano ya kifursa au yale ya kimenejimenti kati ya Fly540
Kenya na Fastjet au kampuni yoyote inayohusiana na Fly540 Afrika.
Matamshi yaliyofanywa na Don
Smith, Mkurugenzi wa Fly540 Kenya, kuashiria kuwa anayo haki ya kuondoa
nembo na pia leseni ya uendeshaji hayafai na hayana msingi. Bodi ya
wakurugenzi ya Fly 540 Kenya haijawahi kukutana kwa ajili hata ya
kufikiria suala hili na hii imethibitishwa na wakurugenzi wengine.
Imetambulika kwa mapana na umma wa Tanzania kuwa suala hili si kitu
kingine bali jaribio la kuhujumu sifa na uaminikaji katika kibiashara.
Fastjet ingetaka kuvishauri
vyombo vya habari na abiria ambao husafiri nasi katika Afrika nzima
katika ndege za fastjet, ndege za Fly540 au ndege za Fly540 Afrika,
kuwa, tunatazamia kupanua shirika letu lenye gharama za chini ili liwepo
katika bara zima la Afrika.
Hadi sasa, tunakaribia idadi ya
maombi ya kusafiria ya abiria 100,000, ambapo 30% wamelipia shilingi za
kitanzania 32,000 tu kwa ajili ya tiketi zao. Vile vile, tunafanya kazi
kwa kuzingatia muda na hatujakuwa na safari zilizofutwa au
zilizobadilishwa huku ndege zetu nyingi zikiwasili ziendako kabla ya
muda uliopangwa.
No comments :
Post a Comment