Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, February 8, 2013

MATUKIO KATIKA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA



 Baadhi ya Maofisa Habari  Mawasiliano wa Wizara za Serikali,  wakielekea katika Ukumbi wa Mkutano wa Bunge mjini Dodoma, leo. Maafisa hao  wamefanya ziara  Bungeni hapo ili kuona  shughuli za Bunge.
 Baadhi ya Maafisa Habari Mawasiliano Serikalini wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene (wa nne kutoka kushoto mstari wa mbele). Wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge leo kuangalia shughuli za Bunge mjini Dodoma.
 Baadhi ya Maafisa Habari Mawasiliano Serikalini wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge.
 Naibu Waziri, Ofisi ya  Waziri Mkuu (TAMISEMI) Aggrey Mwanri akiwakilisha hati mezani kuhusu Taarifa ya  Mwaka na Hesabu zilizokaguliwa na Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha,2010/2011.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi  Pereira Silima  akiwasilisha azimio la Bunge la Kujiunga na Mkataba wa Kimataifa wa Kuzuia Vitendo vya Ugaidi wa Kutumia Nyuklia. Azimio hilo limeungwa mkono leo  katika  mkutano wa kumi kikao cha nane.
 Waziri wa  Elimu na Mafunzo ya Ufundi Shukuru Kawambwa (kulia) akiongea  na James Mbatia (Kushoto)- katika viwanja vya Bunge leo. Baada ya   Spika Anne Makinda(hayupo pichani) kutangaza rasmi Mitala ya  Elimu inayotumika ni halali na ipo. (Pichani katikati) ni   Charles Mwijage (Muleba Kaskazini).
 Mwenyekiti wa Bunge Mussa Zungu Azzan akifafanua kanuni mbalimbali  Bungeni leo.

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe(kushoto) akiongea na  Joshua Nassari(Arumeru Mashariki) ndani  ya ukumbi  wa Bunge. Picha  Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.

No comments :

Post a Comment