Mechi
namba 100 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa jana (Februari 2 mwaka
huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa timu hizo kutoka
sare ya bao 1-1 limeingiza sh. 125,181,000.
Watazamaji
22,030 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa kwa viingilio
vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu
ikipata mgawo wa sh. 30,356,002.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) iliyolipwa ni sh. 19,095,406.78.
Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo 19,583 walikata tiketi hizo na kuingiza sh. 97,915,000.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 15,435,255.48,
tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 9,261,153.29, Kamati ya Ligi
sh. 9,261,153.29, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
4,630,576.64 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 3,601,559.61.
WANYARWANDA KUCHEZESHA MECHI YA STARS, CAMEROON
Waamuzi
kutoka Rwanda wanaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA) ndiyo watakaochezesha pambano katika Tanzania na Cameroon
litakalochezwa Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mwamuzi
wa katikati atakuwa Munyemana Hudu wakati wasaidizi wake ni Simba
Honore na Ndagizimana Theogine wakati mwamuzi wa mezani ambaye pia
anatambuliwa na FIFA atakuwa Oden Mbaga wa Tanzania.
Hudu
na wenzake watawasili nchini kesho (Februari 4 mwaka huu) saa 12.40
jioni kwa ndege ya RwandAir na wamepangiwa kufikia kwenye hoteli ya JB
Belmont. Mechi ambayo ni moja kati ya nyingi zitakazochezwa siku hiyo
(FIFA Date) itafanyika kuanzia saa 11 kamili jioni.
KUNDI LA AKINA ETO’O KUTUA KESHO DAR
Wakati
kundi la kwanza la timu ya Cameroon lenye watu 13 linaingia nchini leo
(Februari 3 mwaka huu) saa 4.40 usiku, kundi la pili linaloongozwa na
nahodha wa timu hiyo Samuel Eto’o linatua kesho (Februari 4 mwaka huu)
saa 3.45 asubuhi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
(JNIA).
Eto’o
anayechezea timu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi atatua kwa ndege ya
Kenya Airways akiwa na Herve Tchami wa Budapest Honved ya Hungary, beki
Nicolas Nkoulou wa Marseille ya Ufaransa, mshambualiji Jean Paul Yontcha
wa SC Olhanense ya Ureno na daktari wa timu Dk. Boubakary Sidik.
Saa
moja baadaye baada ya Eto’oo kutua na wenzake, Kocha wa timu hiyo Jean
Paul Akono na msaidizi wake Martin Ndtoungou watawasili saa 4.40 asubuhi
kwa ndege ya Kenya Airways wakitokea Afrika Kusini.
Kesho
pia kuna kundi lingine litakaloingia saa 4.40 usiku kwa ndege ya KLM
ambalo lina beki Jean Kana Biyick wa Rennes ya Ufaransa, mshambuliaji
Fabrice Olinga wa Malaga FC ya Hispania, beki Allan Nyom wa Udinese ya
Italia ambaye yuko kwa mkopo Granada ya Hispania na beki wa kushoto
Henri Bedimo wa Montpellier ya Ufaransa.
Wachezaji
waliobaki wakiongozwa na kiungo wa Barcelona, Alexandre Song watawasili
Februari 5 mwaka huu kwa muda tofauti kwa ndege za KLM na Kenya
Airways.
No comments :
Post a Comment