Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, September 27, 2011

MBWANA, MIYAYUSHO WATAMBULISHA MPAMBANO WAO


Bondia Fransic Miyayusho (kushoto) naMbwana Matumla kulia wakitunishiana misuli wakati wa utambulisho wa mpambano wao wa ubingwa wa Mabara (UBO) Dar es Salaam , utakaofanyika mwishoni mwa mezi ujao katikati ni mratibu, Mohamed Bawazir.



MABONDIA WA KINONDONI
MABONDIA WA TEMEKE

Bondia Mbwana Matumla (kushoto) na Fransic Miyayusho kulia wakitunishiana misuli wakati wa utambulisho wa mpambano wao wa ubingwa wa Mabara (UBO) Dar es Salaam , utakaofanyika mwishoni mwa mezi ujao katikati ni mratibu, Mohamed Bawazir.

Monday, September 26, 2011

YOHANA ROBART KUTETEA UBINGWA WAKE


BINGWA wa mkanda wa TPBO Yohana Robert amechezea kichapo kutoka kwa Jonas Godfrey katika pambano lake la maandalizi la kutetea ubingwa huo lililofanyika juzi katika ukumbi wa DDC Magomeni Dar es Salaam.

Kutokana na kichapo hicho Robert atakuwa amejipunguzia heshima ya kutetea ubingwa huo ambao anatarajia kuutetea Septemba 30 mwaka huu jijini Tanga kwa kutwangana na bondia Alan Kamote.

Awali Robert alitakiwa kutwangana na Mohamed Shaaban ambaye hakutokea siku ya kupima uzito hivyo kumfanya Robert kubadilishiwa mpinzani katika dakika za mwisho.

Akizungumzia kichapo hicho Kocha wa Robert, Rajab Mhamila alisema kitendo cha bondia wake kubadilishiwa mpinzani ndicho kilichopelekea kichapo kwa bondia wake.

"Mimi sijafurahishwa kabisa bondia wangu kupigwa kwa sababu imempunguzia heshima ya ubingwa wake pia kitendo cha Shaaban kuingia mitini nacho pia kimenikera kwa kuwa tulitegemea ndiye bondia atakayecheza nae,"alisema Mhamila.

Alisema hata hivyo mapungufu yaliyojitokeza kwa bondia wake atayafanyia kazi ili aweze kufanikiwa kuutetea mkanda huo jijini Tanga.

Bondia Robert alipigwa na Godfrey kwa pointi 40-39 ambapo pambano lao lilikuwa la raundi sita. aliongeza kuwa atatumia nafasi ya kumpereka bondia wake tanga na kuamasisha mchezo wa ngumi kupitia DVD zake za Super D Boxing Coach zinazoelekeza mafunzo ya mchezo huo

TBL YATOA VIFAA VYA MIL 10 WIKI YA USALAMA BARABARANI



Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Mohamed Mpinga (kushoto) akimshukuru Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo baada ya kupatiwa na TBL msaada wa fulana na kofia vyenye thamani ya sh. mil. 10 kwa ajili ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama yatakayofanyika mkoani Kagera kuanzia Oktoba 3-8, mwaka huu. Hafla hiyo ilifanyika Dar es Salaam juzi.

MKUU WA MKOA WA RUKWA AWAHAMASISHA WATANZANIA KUWEKEZA NA KUTOWAOGOPA WAGENI WA NJE YA NCHI



Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Mayanyanya akizun gumza na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa Idara ya habari Dar es salaam wakati alipozungumzia Kongamano la Owekezaji litakalofanyika mjini Mpanda Mkoani Rukwa, kushoto ni Katibu tawala wa mkoa huo Salim Muhamed Chima.
Mkuu wa mkoa Mhandisi Stella Manyanya akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wengine kutoka mkioa ya Rukwa, Kigoma na Katavi pamoja na maofisa kutoka kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo leo.

Na Ismail Ngayonga

Maelezo

Dar es Salaam

WATANZANIA na wadau wa maendeleo nchini wamehimizwa kujitokeza na kuwekeza katika vivutio vilivyopo badala ya fursa hizo kuwaachia wageni kutoka nje ya nchi.

Rai hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mkutano wa uwekezaji katika ukanda wa ziwa Tanganyika unaotajiwa kufanyika tarehe 17 oktoba mwaka huu.

Mhandisi Manyanya alisema wakati umefika kwa Watanzania kujitokeza na kuwa vinara katika sekta ya uwekezaji na kamwe wasitishwe na suala la uwezo, kwani katika mipango iliyopo inawasaidia pia wenye uwezo mdogo wa kuwekeza.

“Mikoa iliyopo katika ukanda wa ziwa Tanganyika ambayo ni Kigoma, Rukwa na Katavi ina fursa nyingi za uwekezaji, hivyo kila Mtanzania anahimizwa kuwekeza hata kama ana uwezo mdogo kifedha yapo baadhi ya maeneo unayoweza kuwekeza” Alisema Mhandisi Manyanya.

Alisema mikoa ya Kigoma, Rukwa na Katavi ni miongoni mwa mikoa yenye umuhimu mkubwa katika maendeleo ya nchi, hivyo katika kuharakisha maendeleo ya wananchi wa ukanda huo wadau wote wa ndani na nje ya nchi wana fursa sawa ya uwekezaji kupitia mipango iliyopo.

Manyanya alisema kwa muda mrefu ukanda wa ziwa Tanganyika tangu enzi ya ukoloni umesifika kwa miundombinu duni ya huduma za kiuchumi na kijamii, hatua hiyo iliyosababisha mikoa yake kusahaulika katika harakati za maendeleo ya mawasiliano ya barabara, usafiri wa majini, reli, usafiri wa ndege pamoja na mawasiliano ya simu, runinga na redio.

Aliongeza kwa kutambua changamoto hizo, Serikali ya awamu ya nne imefanya kazi kubwa katika kufungua ukanda huo kwa kujenga miundombinu ya barabara za lami, viwanja vya ndege, bandari katika ziwa Tanganyika, upatikanaji wa umeme wa uhakika, pamoja na kuboresha huduma za jamii.

Kwa mujibu wa wa Mhandisi Manyanya alisema kutokana na mabadiliko hayo yaliyofanyika katika ukanda huo, ni fursa kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuingia katika mikoa hiyo ili kuwekeza na hatimaye kuharakisha maendeleo ya wananchi.

“Wawekezaji wenye uzoefu wa biashara za hoteli za kitalii wanakaribishwa kujenga hoteli katika miji ya Kigoma, Mpanda, Sumbawanga, Mwambao mwa ziwa Tanganyika; pamoja na ujenzi wa mahoteli katika mbugas za hifadhi ya katavi, mahale na Gombe” alisema Manyanya.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Fedha na Utawala kutoka Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC), Bi. Beatrice Chonjo alisema katika kuchagiza mkutano huo, TIC imezihamisha sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika mkutano huo, kwani nafasi waliyonayo ni kubwa katika kuharakisha maendeleo ya mikoa ya ukanda huo na taifa kwa ujumla.

Mgombea Ubunge anapojipumzisha kwa kucheza pool table




Mgombea Ubunge Jimbo la Igunga kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Leopold Mahona akishiriki kucheza mchezo wa pool table katika mji wa Nkinga wilayani Igunga.

DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL ATOA MHADHARA KUHUSU CHANGAMOTO ZA SAYANSI NCHINI TANZANIA UPPSALA, SWEDEN



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mrembo Miss Africa Scandnavia 2010/2011, Michelle Jeng, baada ya kumalizika kwa mkutano baina yake na Watanzania waishio nchini Sweden, uliofanyika kwenye Ukumbu wa Hoteli ya Gillet Clarion, iliyopo Uppsala nchini hapa jana Septemba 25. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Muhammed Mwinyi Mzale. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mrembo Miss Africa Scandnavia 2010/2011, Michelle Jeng, baada ya kumalizika kwa mkutano baina yake na Watanzania waishio nchini Sweden, uliofanyika kwenye Ukumbu wa Hoteli ya Gillet Clarion, iliyopo Uppsala nchini hapa jana Septemba 25. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Muhammed Mwinyi Mzale. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Na Boniphace Makene
Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ametoa mhadhara kuhusu changamoto za kisayansi katika maadhimisho ya miaka 50 ya Idara ya Sayansi za Kimataifa kwa kifupi ISP ya Chuo Kikuu cha Uppsala kilichopo Uswidi ambapo amefafanua kuwa, mchango wa wanasayansi kutoka katika chuo hiki una manufaa makubwa katika kukuza teknolojia katika sayansi kwa nchi za Afrika.
Makamu wa Rais ambaye alikuwa mhadhiri wa somo la Fizikia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kabla ya kuingia katika siasa, amealikwa na wanasayansi wa kariba yake katika maadhimisho haya yaliyo na lengo la kutanua uwanda wa tafiti katika nchi za Afrika na hasa Tanzania, ambayo kwa sasa imeanzisha chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela kilichopo Arusha.
Katika ziara hii ambayo Makamu wa Rais ameambatana na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Telezya Huvisa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim pamoja na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Profesa Burton Mwamilwa.
Ujumbe wa Makamu wa Rais ulifika hapa na kupata nafasi ya kuzungumza na Watanzania waliopo Uppsala ambao wengi walitaka kujua kama Tanzania imejipanga vema kukabiliana na tatizo la umeme nchini. Makamu wa Rais ambaye katika ziara hii amekuwa akikutana na wanasayansi mbalimbali wa Sweden na hasa waliobobea katika sekta ya nishati aliwaeleza Watanzania waliokuwa katika mkutano naye kuwa; kama taifa tuna kila sababu ya kukubali kuwa tulifanya makosa huko nyuma kwa kutotambua utanuaji wa vyanzo vya umeme wa uhakika hali inayotuumiza sasa lakini pia akawaambia kuwa serikali imejipanga vema kuhakikisha kuwa tatizo la umeme linapata tiba katika kipindi kifupi na pia kuwa na umeme wa uhakika katika miaka miwili ijayo.
Maeneo makubwa ambayo Makamu wa Rais amekuwa akiwasikiliza kwa ukaribu wanasayansi wa Uppsala na Sweden ni kuhusu vyanzo mbalimbali vya uzalishaji wa umeme vikiwemo vile vya upepo na maji ya bahari huku pia ikiwa Tanzania imeshasaini mkataba wa uzalishaji wa umeme wa makaa yam awe na kampuni ya kutoka China, mkataba uliosainiwa wiki mbili zilizopita katika ya NDC na kampuni ya China ambazo zitashirikiana katika miradi mikubwa katika ukanda wa Mtwara.
Eneo jingine ambalo Makamu wa Rais amekuja kulihamasisha ni juu ya uhusiano wa chuo hiki kikongwe katika uwanja wa Sayansi na namna chuo hiki kitakavyozidisha ushirikiano wake katika kusomesha wataalamu wa Tanzania katika ngazi za Shahada za Uzamivu na mchango mkubwa ukiwa kukipatia uwezo Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela kilichopo Arusha.
Katika ziara hii ya kitaaluma aliyoalikwa Makamu wa Rais inayochukua siku mbili, Makamu wa Rais pia atakutana na Waziri wa Mambo ya Jamii wa Uswidi Ulf Kristersson na Waziri wa Mahusiano na Maendeleo Gunilla Carlsson. Katika ratiba hiyo pia Makamu wa Rais atatembelea Taasisi ya Mazingira ya Uswidi sambamba na kuzungumzia mafanikio ya Kilimo Kwanza kwa wadau wa maendeleo wa Uswidi.

Sunday, September 25, 2011

NGUMI, KICK BOXING ZAPINGWA DAR ES SALAAM JANA



Mabondia Deo Samuel (kushoto) na Mohamed Matumla wakipambana wakati wa mpambano wao pambano hilo lilitoka droo baara ya kugongana vichwa raundi ya kwanza
bondia Jonas Godfrey akioneshwa ushindi baada ya kumtwanga mpinzani wake Yohana Robart Dar es salaam jana
Kick Boxing Hamisi Mwakinye kulia akilusha teke dhidi ya mpinzani wake Said Mabunda Dar es salaam jana Mwakinye alishinda kwa KO raundi ya kwanza
Pendo Njau kushoto na kanda Kabongo wakiangalia mipambano
Kick Boxing Khalidi Manje kushoto akipambana na Amosi Mwamakula


mabondia chipukizi wakioneshana umaili wa kutupa masumbw

Friday, September 23, 2011

SUPER D , KINYOGOLI WATAMBA BONDIA WAO KUFANYA VIZURI


KOCHA wa bondia Yohana Robart, Rajabu Mhamila 'Super D' ametamba bondia wake kuibuka na ushindi katika pambano lake dhidi ya bondia Mohamed Ndonga litakalofanyika JUMAMOSI katika ukumbi wa DDC Magomeni.

Pambano hilo ni la maandalizi kwa bondia huyo kutetea mkanda wake wa Oganaizesheni ya Ngumi za KUlipwa (TPBO) litakalofanyika jijini Tanga Septemba 30 mwaka huu ambapo atapambana na Alan Kamote wa jijini Tanga.

Akizungumzia maandalizi ya bondia huyo Super D alisema maandalizi ya bondia huyo ni mazuri na anafanya mazoezi chini ya kambi ya ngumi ya Kinyogoli Foundation.

"Nategemea bondia wangu kuibuka na ushindi katika pambano lake la Septemba la jumamosi, ambalo kwa kiasi kikubwa litamsaidia katika maandalizi yake katika pambano la Tanga ambalo litakuwa la raundi 10,"alisema Super D.

Alisema bondia huyo atapigania uzito wa kg. 60 light weight ambapo katika pambano lake la kesho atapigana raundi sita.

Seper D alisema mapambano hayo ni moja ya muendelezo wa kuendeleza vipaji vya mabondia mbalimbali ambapo amewaomba wadau kujitokeza ili kusaidia juhudi hizo zinazofanywa na kambi ya ngumi ya Ilala.

Thursday, September 22, 2011

TAMASHA LA KWANZA LA BIA KUFANYIKA NCHINI



Manager wa bia ya Kilimanjaro George kavishe akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar leo akitangaza udhamini wa tamasha la bia litakalofanyika jijini Dar es Salaam wakishirikiana na bongo 5 media. kulia ni afisa uhusiano wa kampuni ya bia Doris Malulu
Hapa mratibu wa matutikio wa kampuny ya Bongo 5 media Olive nimagaakitoa shukrani zake mbele ya waandishi wa habari

TAMASHA LA KWANZA LA BIA KUFANYIKA NCHINI



Manager wa bia ya Kilimanjaro George kavishe akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar leo akitangaza udhamini wa tamasha la bia litakalofanyika jijini Dar es Salaam wakishirikiana na bongo 5 media. kulia ni afisa uhusiano wa kampuni ya bia Doris Malulu
Hapa mratibu wa matutikio wa kampuny ya Bongo 5 media Olive nimagaakitoa shukrani zake mbele ya waandishi wa habari

UBALOZI WA MAREKANI WADHAMINI WASANII WALIOSHIRIKI TAMASHA LA MTEMI MILAMBO TABORA.



Wasanii wa muziki wa asili walioshiriki Tamasha la tatu ta Mtemi Milambo mwaka huu lililofanyika Julai 8-10,201 katika viwanja vya Uyui sekondari Tabora na kufunguliwa na aliyekuwa mkuu wa mkoa huo Mhe.Abeid Mwinyimussa wamepata udhamini wa kurekodi nyimbo za muziki wa asili za makabila ya Kisukuma na Kinyamwezi.

Wasanii waliofanya vizuri mwaka huu Ali Mango,Asha Kaombwe,Hamis Mpiga,Paulina Muhala,Paul Magadala wataungana na wasanii wengine wa miaka iliyopita na kuunda bendi ya muziki wa asili iitwayo Mwana Milambo ambayo itakuwa inapiga muziki huo katika mahoteli,maharusi na kumbi mbalimbali za burudani.

Nyimbo zitakazorekodiwa ni Kamnyagara kane, Usoga wi kuwa, Kushoke kukaya, kana nabuta, Sensema malunde, Ng,ombe yalala, Wela wa kulya, Nzagamba ya Sukuma na Miaka hamsini ya Uhuru

Lengo kuu ni kuzihifadhi nyimbo mbalimbali zilizotumiwa na wazee wetu wa kale katika vita, kilimo, harusi,na mazishi.

Nyimbo hizi nyingi huimbwa sehemu mbalimbali lakini ni muhimu kuzirekodi kwa ajiri ya faida ya vizazi vya baadae.

Nyimbo hizo zote zitarekodiwa katika studio ya Aegies chini ya muandaaji maarufu Peter John a.k.a Nice P.
HABARI NA PICHA KWA HISANI YA http://fullshangwe.blogspot.com/

KUNDI LA T-MOTO MODERN TAARAB LATUA DAR KUFYATUA SITA MPYA KWA MPIGO



KUNDI jipya la muziki wa taarab la Tanzania Moto Modern Taarab (T-Moto) limetua jijini Dar es Salaam leo asubuhi kutoka mfichoni katika Visiwa vya Zanzibar, lililokuwa limejichimbia kwa ajili ya maandalizi ya uzinduzi wake uliosogezwa mbele hadi Oktoba 28 mwaka huu.
Kundi hilo limewasili jijini baada ya kusitisha mazozi yake kwa muda kwa ajili ya maombolezo ya msiba wa Meli ya Mv Spice na linatarajia kuingia studio kwa ajili ya kurekodi nyimbo zake mbili kati ya zilizosalia ili kukamilisha albamu yao.
Akizungumza katika Bandari ya jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa kundi hilo Amin Salmin, alisema kwamba kundi hilo litaingia katika stuio za Bakunde na kurekodi nyimbo sita ambazo zitakamilisha albamu yao iitwayo ‘Aliyeniumba Hajanikosea’.
Aidha alisema kuwa baada ya kumaliza zoezi la kurekodi nyimbo hizo, kundi hilo linatarajiwa kufanya ziara katika mikoa ya Tanzania na nchi jirani ya Kenya, kabla ya kufanya uzinduzi rasmi wa kundi na albamu yao Oktoba 28, jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wasanii wa kundi hilo ambaye ni mkongwe katika muziki huo wa Taarab, Bi. Mwanahawa Ally alisema anashukuru kambi hiyo imewaweka katika mwelekeo mzuri ambapo anaamini kazi zitakazotoka zitakuwa na viwango vya hali ya juu hivyo amewaomba mashabiki wakae mkao wa kula.
“Nataka niwaeleze mashabiki wa tasnia ya taarab kwamba tunakuja kwa moto kama lilivyo jina la kundi letu, moto ambao si rahisi kuzimika kwa kijipipa cha maji, hivyo mashabiki wetu wasubiri mambo mazuri na ya kupendeza kutoka kwetu, tunawaomba mashabiki watupokee vizuri kwa kujitokeza kwa wingi katika maonyesho yetu,”Alisema.
Tayari kundi hilo limeshatoa nyimbo mbili ambazo zimeweza kuliwatambulisha vyema.
Nyimbo hizo ni pamoja na uliobeba albamu hiyo‘ Aliyeniumba Hajanikosea’ ulioimbwa na Mwanahawa Ally, pamoja na ‘Unavyojidhani Mbona Hufanani’ ulioimbwa na Jokha Kassim.
Nyimbo nyingine zinazotarajiwa kuwamo katika albamu hiyo ni pamoja na ‘Mtoto wa Bongo’ ulioimbwa na Hassan Ally, ‘Mchimba Kaburi Sasa Zamu yake imefika’ ulioimbwa na Mrisho Rajab, ‘ Mwenye Kustiri Mungu’, ‘Kumbe Wewe ni Shoti’ ambazo zimeimbwa na Mosi Suleiman na ule wa ‘ Riziki na Shortcut’ ulioimbwa na Aisha Masanja.
Kundi hilo limesheheni wasanii wenye vipaji vya hali ya juu wakiwemo Mwanahawa Ally, Jokha KAssim, Jumanne Ulaya ‘Mkono wa Biashara’, Mrisho Rajab, Musa Mipango, Hassan Ally, Mosi Suleiman, Rajab Kondo, Fadhili Mnara, Moshi Mtambo, Ally Kabura, Sabha, Rahma , Asha Masanja na Hanifah Kasim na wengineo.

Kamati ya mambo ya Nje kutoka Bunge la Finland yatembela Bunge la Tanzania



Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama ya Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb) akieleza nafasi ya Bunge katika Maswala ya Mambo ya Nje kwa Mwenyekiti wa Kamati ya mambo ya Nje kutoka Bunge la Finland Mhe. Ine Marie Erikson (Mb) mara baada ya kamati hiyo kutoka Finland kutembela Bunge la Tanzania kwa ziara ya kubadilishana uzoefu leo.
Wajumbe wa kamati ya mambo ya nje kutoka Finland wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama ya Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb) pamoja na baadhi ya wabunge wa Bunge letu.
Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama ya Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao na Kamati ya mambo ya Nje kutoka Bunge la Finland iliyofanya ziara katika Bunge la Tanzania kwa lengo la Kubadilishana uzoefu

Wednesday, September 21, 2011

MATOKEO YA LIGI KUU


Young Africans 3 : 2 Villa Squad
Toto African 3 : 3 Simba SC
Coastal Union 0 : 1 Azam FC

Vodacom Premier League Vodacom Premier League 2011/2012

Rank Teams Played Wins Draw Lost GD Points
1 Simba SC 7 4 3 0 5 15
2 Azam FC 7 4 2 1 4 14
3 Mtibwa Sugar 6 3 2 1 3 11
4 JKT Ruvu 6 2 4 0 4 10
5 Toto African 7 2 3 2 2 9
6 Young Africans 7 2 3 2 0 9
7 Moro Utd 6 2 2 2 -2 8
8 Police Dodoma 6 1 3 2 1 6
9 Ruvu Shooting 5 1 3 1 0 6
10 African Lyon 6 1 3 2 -1 6
11 JKT Oljoro 5 1 3 1 -1 6
12 Kagera Sugar 6 0 5 1 -1 5
13 Coastal Union 7 1 1 5 -6 4
14 Villa Squad 7 1 1 5 -8 4









Mchezaji bora zaidi wa Uingereza katika mchezo wa tennis na nambari 4 duniani Andy Murray asema kuna uwezekano wa wachezaji wa kulipwa kufanya mgomo i

Andy Murray

Asema kuna uwezekano wa wachezaji tennis kufanya mgomo juu ya malalamiko ya ratiba

Andy Murray amesema wachezaji bora zaidi wa tennis ya kulipwa wangelipenda kuona mabadiliko katika ratiba ya mapambano yao, na kuna uwezekano wa kuyagomea mashindano ikiwa maslahi yao hayatatiliwa maanani.

Amesema wachezaji wengi wamekuwa wakiudhika mno kutokana na ratiba iliyosongamana, na watakutana mjini Shanghai mwezi ujao kujua hatua watakazoweza kuzingatia.

Murray ameielezea BBC kwamba kuna uwezekano wa mgomo kufanyika.

"Kuna uwezekano. Nafahamu hilo, kwani baada ya kuzungumza na baadhi ya wachezaji, wao hawana wasiwasi wa kufanya hivyo [kugoma].

"Tutumaini kwamba hatutafikia hatua hiyo, lakini nina hakika wachezaji wataifikiria."

Alipoulizwa ikiwa suala hilo la mgomo litajadiliwa nchini Uchina, alijibu: "Ndio, nafikiria hivyo".

Martin Mathathi ameibuka bingwa katika mashindano ya riadha ya Great North Run mjini Gateshead nchini Uingereza

Martin Mathathi

Mkenya Mathathi ameandikisha muda bora zaidi katika mashindano ya Great North Run

Ilikuwa ni fahari kwa Kenya siku ya Jumapili wakati wanariadha wake wawili walipoweza kutwaa ushindi katika mashindano ya Great North Run, mjini Gateshead, Uingereza, wakati Martin Mathathi alipomaliza wa kwanza na akiandikisha rekodi, huku kwa upande wa kina dada, mwanariadha mwenzake kutoka Kenya, Lucy Karbuu alimaliza katika nafasi ya kwanza pia, na akiwa wa tatu kuwahi kwenda kasi zaidi katika historia ya mashindano hayo.

Martin Mathathi aliandikisha muda wa kasi zaidi katika historia ya mashindano hayo kwa kumaliza katika muda wa dakika 58, sekunde 56.

Karbuu aliwashangaza wengi kwa muda alioandikisha, akimaliza mbio hizo katika muda wa saa moja, dakika saba na sekunde sita, huku Mreno Jessica Augusto akishikilia nafasi ya pili.

Wanariadha wawili wa Uingereza, Jo Pavey na Helen Clitheroe waliyatumia mashindano hayo katika kujiandaa kwa michezo ya Olimpiki ya mwaka 2012 mjini London, Olympics.

Pavey, mwenye umri wa miaka 37, alimaliza katika nafasi ya nne, huku Clitheroe akifuata katika nafasi ya tano.

Mathathi, ambaye alishinda medali ya shaba mita 10,000 katika mashindano ya dunia ya mwaka 2007 mjini Osaka, Japan, alifanikiwa kupunguza sekunde tisa katika rekodi ya Zersenay Tadese wa Ethiopia, iliyoandikishwa mwaka 2005, ya muda wa dakika 59, sekunde 5.

Huo ni kati ya muda bora zaidi, miongoni mwa sita bora, kuwahi kuandikishwa katika mashindano ya nusu-marathon.

Mkenya Jonathan Maiyo alijitahidi kutimka na kuwatangulia wenzake baada ya maili tano za mashindano, lakini kufikia maili nane, Mathathi alikuwa tayari ameshampita.

Wauzaji Tiketi YANGA v AZAM







Mmoja wa wauzaji tiketi kwenye mechi ya Azam na Yanga iliyochezwa Septemba 18 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Seleman Masoud aliripoti kupotelewa kitabu kimoja cha tiketi mara baada ya ugawaji wa vitabu hivyo kwa wauzaji kufanyika asubuhi ya siku ya mchezo kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Tiketi kutoka kwenye kitabu hicho ziliuzwa kwa mashabiki ambao walikamatwa. Walitakiwa kuonesha mahali ambapo wameuziwa tiketi hizo ambapo walionesha kwa muuzaji mwingine Salum Abdallah. Abdallah pia alikuwa mmoja wa wauzaji tiketi katika mechi hiyo.

Wauzaji wote wawili walikamatwa na TFF na tukio kuripotiwa Kituo cha Polisi Chang’ombe. Tukio hilo lilifunguliwa jalada namba CHA/IR/6257/2011 ambapo watuhumiwa wameshachukuliwa maelezo yao. Kitabu kilichoibwa kilikuwa na tiketi 100 zenye thamani ya sh. 300,000. Thamani ya kila tiketi ni sh. 3,000.

Wenger ataka "miaka mingine" 14 Arsenal

Arsene Wenger amesema wala hasumbuliwi na kelele zinazopigwa dhidi yake na anataka kuendelea kuingoza Arsenal kwa kipindi kirefu zaidi.

Arsene Wenger

Arsene Wenger

Wachambuzi wa soka wamekuwa wakihoji nafasi ya Wenger wakati huu Arsenal ikishikilia nafasi ya 17 ya msimamo wa Ligi Kuu ya England wakiwa wameuza wachezaji muhimu msimu huu.

Lakini baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Shrewsbury kuwania Kombe la Carling, Wenger amesema: "Sijali kabisa kutokana na uvumi uliopo dhid yangu kwamba nitatimuliwa.

"Nimekuwa katika klabu hii kwa miaka 14 na nimefanikiwa kuiweka katika kuwania ubingwa wa Ulaya kwa miaka hiyo 14. Natumai nitaendelea kuwepo miaka mingine 14."

Mtendaji mkuu wa Arsenal Ivan Gazidis ameiambia BBC kwamba kumfukuza Wenger sio jambo wamalofikiria kulitekeleza.

Zaidi anachokiangazia zaidi Wenger ni kuimarisha kikosi chake baada ya nahodha wake Cesc Fabregas kuhamia Barcelona na kiungo mwenzake Samir Nasri kujiunga na Manchester City mwezi wa Aprili.

Katika siku ya mwisho ya usajili, kiungo wa Everton Mikel Arteta, mshambuliaji Park Chu Young, beki wa kushoto Andre Santos na mlinzi wa kati Per Mertesacker walijiunga na Arsenal, wakati Wenger pia alimchukua kwa mkopo Yossi Benayoun kutoka klabu ya Chelsea.

Lakini mabadiliko hayo yamekuwa makubwa kuyazoea uwanjani, wakati Arsenal imeshinda mechi moja tu ya Ligi kati ya mechi tano huku ikiwa imefungwa mabao mengi hadi sasa.

Wenger amesema:"Naelewa watu hawana furaha na wanalaumu, lakini najua mnafahamu kama ninavyofahamu kwamba watu wanakuwa wepesi sana kufikia hatua ya kulaumu".

"Tunapofanya vizuri tunashangiliwa na kupongezwa, kwa hiyo tunawajibika kukubali lawama iwapo mambo yanapokwenda kombo - lakini kwa pande zote mbili pia tunatakiwa kuwa na subira.

Sunday, September 18, 2011

NAIBU WAZIRI CHARLES KITWANGA NA TTCL WAPANGA MIKAKATI YA KUIMARISHA SHIRIKA HILO



Naibu waziri wa Mawasiliano Mh. Charles Kitwanga akizungumza na wakuu wa vitengo Kampuni ya simu ya TTCL pamoja na wajumbe wa bodi ya kampuni hiyo baada ya kumalizika kwa kikao cha kujadili Changamoto mbalimbali zinazokabili shirika hilo, ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati mbalimbali ya kukuza na kuendeleza shirika hilo.
Waziri wa Mawasiliano Charles Kitwanga akiwa katika picha ya pamoja Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Said Amir Said, pamoja na mwenyekiti wa bodi ya kampuni hiyo Dr. Enos Bukuku mara baada ya kumaliza kikao chao leo.
Wakuu wa vitengo mbalimbali kutoka kampuni ya TTCL wakmionekana kufuatilia jambo katika mkutano huo.
Mh Waziri wa Mawasiliano Mh Charles Kitwanga akiwa katika akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya TTCL pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TTCL.

Thursday, September 8, 2011

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Septemba 8, 2011
 
VPL KUCHEZWA UWANJA WA TAIFA
Serikali imeruhusu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kutumika kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zinazohusu timu za Simba na Yanga. Hata hivyo ruhusa hiyo ni ya mechi mbili kwa wiki.
 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na klabu za VPL zenye maskani yake Dar es Salaam waliwasilisha tena maombi Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ili kutumia uwanja huo kwa mechi za ligi.
 
Kutokana na uamuzi huo wa Serikali mechi ambazo sasa zitachezwa kwenye uwanja huo ni Ruvu Shooting vs Yanga (Septemba 10), Azam vs Simba (Septemba 11), Simba vs Polisi Dodoma (Septemba 14), African Lyon v Yanga (Septemba 15), Azam vs Yanga (Septemba 18), Yanga vs Villa Squad (Septemba 21).
 
Nyingine ni Yanga vs Coastal Union (Septemba 24), Simba vs Mtibwa Sugar (Septemba 25), Yanga vs Kagera Sugar (Oktoba 14), Simba vs African Lyon (Oktoba 16), Simba vs Ruvu Shooting (Oktoba 19), Yanga vs Toto Africans (Oktoba 20), Simba vs JKT Ruvu (Oktoba 22), Yanga vs Oljoro (Oktoba 23), Yanga vs Simba (Oktoba 29) na Moro United vs Simba (Novemba 5).
 
TWIGA STARS, BANYANA BANYANA 2-2
Timu ya Taifa ya wanawake ya Tanzania (Twiga Stars) imetoka sare ya mabao 2-2 na Afrika Kusini (Banyana Banyana) katika mechi ya michezo ya All Africa Games (AAG) iliyochezwa leo Uwanja wa Machava jijini Maputo, Msumbiji.
 
Banyana Banyana ndiyo iliyoanza kupata bao kabla ya Twiga Stars kusawazisha dakika ya 25 kupitia kwa Mwanahamisi Shuruwa. Banyana Banyana ilianza kipindi cha pili kwa nguvu na kupata bao la pili. Zena Khamis aliisawazishia Twiga Stars dakika 60.
 
Twiga Stars itacheza mechi yake ya mwisho hatua ya makundi Septemba 11 mwaka huu dhidi ya Zimbabwe kwenye uwanja huo huo. Katika mechi yake ya kwanza Zimbabwe ilifungwa na Banyana Banyana mabao 4-1.
 
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Kenny Dalglish amtetea Andy Carroll

Fabio Capello na Andy Carroll
Meneja wa England amemtaka Carroll kurekebisha maisha yake kwa kupunguza ulevi
Meneja wa klabu ya soka ya Liverpool, Kenny Dalglish, amemtetea mchezaji Andy Carroll, kufuatia madai ya kocha wa timu ya taifa ya England, Fabio Capello, kuhusu starehe za kibinafsi za mchezaji huyo.
Carroll alikuwa ni mchezaji wa zamu katika mechi ambayo England ilipata ushindi ilipocheza dhidi ya Wales.
Capello awali alikuwa amesema: "Ikiwa anataka kuwa mchezaji mzuri, basi ni lazima apunguze kinywaji zaidi wa wenzake".
Lakini Dalglish amesisitiza: "Hali yake ya afya ni bora zaidi kumshinda yeyote yule.
"Sidhani maisha na starehe zake za kibinafsi sio kama inavyofikiriwa katika kutafuta cha kuandika kumhusu".
Meneja wa Liverpool aliongezea: "Andy hakuwa katika hali nzuri msimu uliopita kutokana na jeraha la goti.
"Tunafurahia hali yake ya afya msimu huu kwa kwa jeraha hilo limetoweka".
Carroll, mwenye umri wa miaka 22, amecheza tangu mwanzo katika mechi mbili, kati ya mechi nne za Liverpool, tangu alipofika katika uwanja wa Anfield, kufuatia kuhama kutoka Newcastle mwezi Januari.
Mchezaji huyo alifunga mara moja katika pambano la Kombe la Carling dhidi ya Exeter, lakini msimu uliopita, aliweza kutumbukiza magoli mawili katika lango la Manchester City, wakati timu yake ilipopata ushindi wa magoli 3-0.
Dalglish aliongeza: "Nadhani Andy anapokea mawaidha vyema hasa kutoka kwa yeyote yule mwenye uzoefu katika mchezo wa soka".
"Nadhani amepokea vyema mawaidha ya Capello kwa kuwa anamheshimu sana, na nadhani, Fabio Capello naye amheshimu sana Andy Carroll".

Tuesday, September 6, 2011

WACHEZAJI WA MPIRA WA KIKAPU MAREKANI WATOA ELIMU KWA SHULE YA MSINGI CHAN'GOMBE LEO




Kamishina Maendeleo ya watoto na mashuleni Seleoni Semunyu katikati akiwa katika picha ya pamoja na Tamika Raymond na Dee Brown wakati wa clinich ya mpira wa kikapu leo











Mchezaji wa Mpira wa kikapu Marekani,Tamika Raymond akiagana na watoto wa shule ya Msing Chang'ombe leo alipokwenda kutoa elimu ya bule kuusu mchezo huo

Nizar Khalfan AKUTANA NA Rais Dkt.Jakaya Kikwete


Mtanzania anayecheza Soka ya kulipwa katika timu ya White Caps ya jijini Vancouver Canada Nizar Khalfan akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Kikwete jezi ya timu yake wakati alipokwenda kumsalimu na kumshukuru ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.(picha na Freddy Maro)


Mtanzania anayecheza Soka ya kulipwa katika timu ya White Caps ya jijini Vancouver Canada Nizar Khalfan akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Kikwete jezi ya timu yake wakati alipokwenda kumsalimu na kumshukuru ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.(picha na Freddy Maro)