Mtunzi
mashuhuri wa vitabu kutoka kampuni ya Mkuki na Nyota, Mzee Walter
Bgoya, akikata utepe pamoja na mtunzi wa kitabu cha ‘Kifo ni Haki
Yangu’, Eric James Shigongo (kulia) wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho
uliofanyika katika duka la vitabu la Tanzania Publishing House lililopo
mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam leo.
Mtunzi
wa kitabu cha ‘Kifo ni Haki Yangu’, Eric James Shigongo, akiongea na
wadau (hawapo pichani) waliofika katika uzinduzi wa kitabu chake katika
duka la vitabu la Tanzania Publishing House lililopo mtaa wa Samora
jijini Dar.
Afisa
wa polisi Patrick Massawe ambaye pia ni mtunzi mashuhuri wa hadithi za
magazeti nchini, akisainiwa kitabu na Shigongo wakati wa uzinduzi.
Eric Shigongo akimsainia kitabu mwanaye, Samwel Shigongo.
Eric Shigongo akisaini kitabu kwa ajili ya mwandishi wa Nipashe, Somoe Ng’itu.
Shigongo akiwasainia vitabu baadhi ya wasomaji waliohudhuria uzinduzi huo.
Afisa wa polisi Patrick Massawe na msomaji mwingine wakipitia baadhi ya kurasa za kitabu cha Eric Shigongo aliyesimama kulia.
Shigongo akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa duka la TPH.
MTUNZI
mahiri wa vitabu nchini, Eric James Shigongo, leo amezindua rasmi
kitabu chake cha ‘KIFO NI HAKI YANGU’ katika duka la vitabu la Tanzania
Publishing House (TPH) lililopo mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam.
Katika uzinduzi huo, wasomaji 50 wa mwanzo walipata fursa ya kupata
zawadi ya kitabu hicho bure kilichosainiwa na mtunzi. Kujipatia nakala
ya kitabu hicho na vinginevyo, wasiliana au fika katika vituo tajwa hapo
chini:
(PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY / GPL)
No comments :
Post a Comment