Mkurugenzi
wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Dk. Aloyce Nzuki akiwa katika mazungumzo
na Rica Rwigamba Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Rwanda wakati
alipokutana katika maonyesho ya dunia ya Utalii ITB yanayofanyika kwenye
jengo la Messe Berlin jijini Berlin Ujerumani, Monyesho hayo
yanahusisha makampuni yenye kutoa huduma mbalimbali za utalii duniani
ambao hukutana na kutangaza utalii wa nchi zao huku wakifanya
makubaliano na kuingia mikataba mbalimbali ya kuuziana bidhaa za
kitalii, Maonyesho hayo yanamalizika rasmi leo. Mkurugenzi wa Kampuni ya ndege ya Flightlink Capt. Munawer Dhirani akizungumza na Ibrahim Mussa Mkurgenzi wa Utalii Wizara ya Maliasili na Utalii katikati ni Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Christopher Mvula akisikiliza
kwa makini wakati Balozi huyo alipotembelea katika banda la Tanzania
kwenye maonyesho ya ITB yanayomalizika leo jijini Berlin Ujerumani kulia
ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Dk. Aloyce Nzuki .(PICHA
NA FULLSHANGWEBLOG) Meneja
Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Geofrey Meena kushoto akitembelea
Banda la Kampuni ya Pongo Safaris katika maonyesho ya Utalii ya ITB,
wengine kutoka kulia ni Marlon Van Hee Meneja Mradi wa kampuni ya ECEAT
PROJECTS ya Uholanzi ,Julias Alexander Pundo Mwakilishi wa kampuni ya
Ramogi Tours & Travel Limited Jumuiya ya Ulaya na Cynthia Ponera
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Pongo Safaris Wadau
wa Ujerumani hawakukosa kutembelea maonyesho hayo hapa walikuwa
wakipata Menyu wakati wa hafla ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Team Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kazi kubwa ya kuuza utalii wa Tanzania kwenye maonyesho hayo. Nami
nikajichanganya kwenye Banda la Pongo Safaris na Ramogi Tours hapa
nikipata picha na Julius wa Ramogi Tours pamoja na Cynthia wa Pongo
Safaris Kaimu
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Christopher Mvula akizungumza jambo
na Mkurugenzi wa Kampuni ya ndege ya Flightlink Capt. Munawer Dhirani
wakati walipokutana katika maonyesho hayo
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment