Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali na kumpa pole Mzee` Yusuf Mzimba,
mmoja wa wazee marufu wa Klabu ya Dar es salaam Young Africans (YANGA) ambaye
amelezwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiuguza majeraha
kufuatia kugongwa na BodaBoda wiki iliyopita Barabara ya Nyerere jijini
Dar es salaam. Mzee Mzimba
amevunjika mguu wa kushoto na kupata majeraha ya usoni na mikononi.
Hadi jana hali yake ilikuwa inaendelea vyema na Rais Kikwete amempa pole
nyingi kwa maumivu aliyoyapata na kumtakia apate nafuu ya haraka. PICHA NA IKULU
RC NYONGO AAGIZA UPANDAJI MICHE MILIONI MBILI YA KOROSHO PWANI
-
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Stanslaus Haroon Nyongo, amezitaka Halmashauri
zote za Mkoa huo kuhakikisha zinapanda miche ya mikorosho milioni mbili kwa ...
3 days ago


No comments :
Post a Comment