Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Saturday, July 6, 2013

SHINYANGA,TABORA,KAGERA NA KILIMANJARO WAPATA MABINGWA WA VILABU SAFARI POOL




Mwakilishi wa Afisa Utamaduni Mkoa wa Shinyanga,Seif Hamadi(kushoto)na Mwenyekiti wa Chama cha Pool Shinyanga, Jastin Shine (wapili kushoto) wakimkabidhi nahodha wa Klabu ya King Palace, Kulwa Peter, fedha taslimu shilingi 700,000 mara bada ya kuibuka mabingwa kwenye fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa Ngazi ya Mkoa yaliyofanyika katika Klabu ya Garden Mkoani Shinyanga

Machezaji wa Klabu ya King Palace wakishangilia na kitita cha shilingi 700,000 mara baada ya kuibuka mabingwa kwenye fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa Ngazi ya Mkoa yaliyofanyika katika Klabu ya Garden Mkoani Shinyanga 



 FAINALI za mashindano ya mchezo wa Pool Taifa ngazi ya Mkoa yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia nchini(TBL) kupitia Bia ya Safari Lager yamemalizika vyema kwa kupata vilabu vitakavyowakilisha mikoa katika mikoa mine ambayo ni Shinyanga,Kilimanjaro,Kagera naTabora.
Mkoa wa Shinyanga,King Palece  klabu wameibuka mabingwa 2013, baada ya kumfunga klabu ya Emerates 13-8.Kwa ubingwa huo walizawadiwa fedha taslimu shilingi 700,000/= na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa Shinyanga kwenye fainali za kitaifa zinazotarajiwa kufanyika Mkoani Morogoro mwezi ujao. Emirates walikamata nafasi ya pili na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 350,000/=,Nafasi ya tatu ni Klabu Veteran ambao walizawadiwa shilingi 200,000/=.
Upande wa wachezaji mmoja mmoja(Singles) wanaume,Paul Silas alitwaa ubingwa kwa kumfunga Siga Agustino 3-0,hivyo kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 350,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa kwenye fainali za kitaifa Mkoani Morogoro ambapo Siga alikamata nafasi ya pili na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 200,000/=.Upande wa wakinadada Sada Tula alitwaa ubingwa na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 250,000/=
Mkoa wa Kilimanjaro, Klabu ya Mbosho imefanikiwa kutetea ubingwa wa Mashindano  hayo kwa kuifunga  Goodhope 16-5 na hivyo kujinyakulia zawadi ya fedha taslimu shilingi 700,000/=  na  Medali ya Dhahabu pamoja na  tiketi ya kuwakilisha Mkoa kwenye  fainali za kitaifa pale Morogoro,na  nafasi ya poli ilichukuliwa na Goodhope ambao walizawadiwa shilingi 350,000/=  na medali ya Fedha.Nafasi ya tatu ilichukuliwa na Highbury na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 200,000.

Katika mchezo wa mchezaji mmoja mmoja (Singles) wanaume mchezaji, Peter George alifanikiwa kutwaa ubingwa  na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 350,000  na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za kitaifa baada ya kufunga  Spider Elisha 2-1ambaye alikamata nafasi ya pili na kuzawadiwa shilingi 200,000.

Upande wa wanawake mchezaji, Mwayamu Mwinyi alitwaa ubingwa na kuzawadiwa shilingi 250,000 na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za kitaifa Mkoani Morogoro baada ya kumfunga, Maya Saburi 2-1 ambapo yeye alishika nafasi ya pili na kuzawadiwa shilingi 150,000.


Mkoa wa Kagera,Klabu ya Bilele ilitwaa ubingwa na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 700,000 na tiketi ya kuwakilisha Mkoa kwenyefainali za kitaifa baada ya kuifunga Klabu ya Bukoba ambayo ilishika nafasi ya pili na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 350,000.Nafasi ya tatu ilichukuliwa na Klabu ya Q Bar  ambao walijinyakulia fedha taslimu shilingi 200,000.
Upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume,Gozbat Kapama alitwaa ubingwa na kuzawadiwa shilingi 350,000 na tiketi ya kuwakilisha Mkoa kwenye fainali za kitaifa na Upande wa wanawake mmoja mmoja Patricea Parick alitwaa ubingwa na kuzawadiwa 250,000 na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za kitaifa.
Mkoa wa Tabora,Kalbu ya Loriondo wameliibuka mabingwa na kuzawadiwa shilingi 700,000 pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za kitaifa wakati nafasi ya pili ilichukiwa na Klabu ya Tiptop ambao walijinyakulia frdha taslimu shilling 350,000.
Upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume,Ernest John alitwaa ubingwa na kuzawadiwa shilingi 350,000 na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za kitaifa wakati upande wa kinadada,Happness Magani alitwaa ubingwa na kuzawadiwa shilingi 250,000 na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za kitaifa Mkoani Morogoro.

No comments :

Post a Comment