Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, May 28, 2010

TIMU ZA TAIFA ZA AFRIKA KATIKA KOMBE LA DUNIA

Kocha wa timu ya taifa ya Misri Hassan Shehata bila shaka amejipatia umaarufu mkubwa kabla na hata wakati huu tukielekea katika kombe la dunia. Hakika sio tu kwa sababu hivi sasa anaogelea katika dimbwi la pongezi nyingi, bali ni kwa sababu makocha maarufu duniani wangependa sana kuchota sehemu ya maarifa na umahiri wake.
Shehata

Hassan Shehata akipongezwa

Shehata mwenye umri wa miaka 60, alifanikiwa ‘kuzitandika’ si chini ya timu nne zinazotarajiwa kuiwakilisha Afrika katika kombe la dunia wakati wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika iliyofanyika mwezi wa kwanza nchini Angola na kutwaa ubingwa. Timu hizo ni Nigeria, Cameroon, Algeria na Ghana. Nigeria wao baada ya kumtimua kocha Shaibu Amodu, wakaamua kufuata hekima ya kutafuta maarifa toka kwa wapinzani wao ( if you can’t beat them, join them”) na kuonesha nia ya kumpa Shehata kazi hiyo yenye changamoto nzito. Hata hivyo inaonekana kuwa jitihada hizo zimekutana na ukuta mgumu wa Chama cha soka cha Misri.

Hakika si mengi tunayoweza kujifunza katika soka dhaifu la Nigeria wakati wa fainali za kombe la mataifa ya Afrika na hatimaye kufukuzwa kwa Amoadu ukilinganisha na timu zingine zitakazoiwakilisha Afrika katika Kombe a Dunia. Ilichapwa na Misri, ikabahatika kwa Benin, ikapata ahueni kwa Msumbiji lakini ikawa dhaifu mbele ya Zambia na kulewa mbele ya Ghana. Hakika hatuwezi sema kuwa Soka la Nigeria wakati wa fainali hizo lilikuwa lenye uwezo wowote wa maana.

Nigeria

Kikosi cha Nigeria kilichoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2010

Picha-caption-Nigeria ilishika nafasi ya tatu lakini ikaamua kumtimua kocha

Nigeria wanaonekana kawaida kuanza vyema lakini hakika wanahitaji sana kuongeza msuli ili mambo yao yaweze kufanikiwa.

Kushindwa kufunga magoli lilikuwa tatizo wakati mwingine. Yakubu na Obafemi Martins walikosa magoli mengi. Lakini tatizo hasa ni kukosekana kwa kwa kiungo mchezeshaji Viungo wengi walioichezea Nigeria katika fainali hizo ni viungo wakabaji; John Obi Mikel, Dickson Etuhu, Sani Kaita na Yussuf Ayila, hali iliyosababisha mshambuliaji Osaze Odemwingie awe na kazi kubwa.

Nigeria wana tatizo jingine la kutocheza kama timu moja iliyoshikamana. Ni kikosi kilichojaa ubinafsi wa mchezaji mmoja mmoja. Hii itakuwa ni changamoto kubwa kwa kocha mpya hasa ukitilia maanani muda mfupi uliobaki kabla ya Fainali za Kombe la Dunia na timu pinzani katika kundi B ambazo ni Argentina, Korea ya Kusini na Ugiriki.

Wachambuzi wa soka kwa muda mrefu wamekuwa wakilisema jambo hilo kuhusu Nigeria lakini si kwa Ivory Coast.

Kama ilivyo kwa ndugu zao hao wa Afrika Magharibi, kikosi cha Ivory Coast nacho kilikosa kiungo mchezeshaji. Japo Yahya Toure na Didier Zokora ni viungo hodari lakini hawakuonesha kuelewana ipasavyo au uwezo wa kubadilisha mchezo. Jukumu hili linaonekana kuwaaangukia Abdulkader Keita na Bakary Kone, lakini kule Angola hawakuonesha la maana sana. Ukimtaja Gervinho, bado hakuweza kuonesha makeke licha ya matarajio makubwa aliyotwishwa.

Drogba

Nahodha wa Ivory Coast, Didier Drogba

Hiyo ni kwa upande wa ubunifu katika kiungo.Lakini udhaifu wake hatuwezi kuulinganisha na udhaifu mkubwa uliojionesha katika nafasi ya ulinzi hasa wakati wa kipigo cha nusu fainali toka kwa Algeria. Mabeki na viungo walipoteza kabisa maelewano, hali iliyojionesha wazi pale beki wa Algeria Madjid Boughera alipotumia vyema udhaifu huo kufunga goli la muhimu la kusawazisha katika dakika ya 92.

“Timu kubwa haziachii ushindi wa 2-1 upotee kirahisi kunapokuwa kumebaki dakika chache mechi kumalizika”, akasema kocha wa Ivory Coast kutoka Bosnia Vahid Halilhodzic. “Tulikuja na matumaini makubwa, lakini kwa mara nyingine Ivory oast imeshindwa kutoa matokeo mazuri. Si tatizo la kimwili ila ni la kisaikolojia”

Lilikuwa ni tatizo la kisaikolojia au ni matokeo ya pumziko refu la siku tisa lililosababishwa na kujiondoa kwa Togo? Wachambuzi wanaweza kusema ni tatizo la kisaikolojia, wakizingatia matokeo mabaya ya miaka ya nyuma. Mwaka 2006 Ivory Coast ilifungwa na Misri katika fainali, ikapoteza nusu fainali mwaka 2008 mbele ya hao hao Misri na mwaka huu ikabanwa mbavu na Algeria.

Inavyoonekana ni kuwa Ivory Coast hupata wakati mgumu ikikumbana timu zilizojipanga vyema. Sifa ambayo timu za Afrika Kaskazini wanayo. Lakini bora wajue kuwa wapinzani wao ndani ya kundi G, Korea ya Kaskazini, Ureno na Brazil, zote zina sifa hiyo hiyo ya kujiandaa na kujipanga vyema. La kutia hofu zaidi ni kwamba mashabiki wa Ivory Coast wanaonekana kupoteza imani yao kwa mshambuliaji Didier Drogba ambaye kiwango chake kule Angola kiliwakasirisha wengi.

Sina hakika kama watu wa Cameroun wana hisia na mawazo hayo hayo juu ya Samuel Eto’o. Lakini naye hakuwa katika kiwango chake kule Angola. Kocha Paul Le Guen alimchezesha nyuma ya washambuliaji wawili mbele katika kipigo cha robo fainali kutoka kwa Misri. Lakini kwa silika ya kiwindaji aliyo nayo Eto’o, inakuwaje achezeshwe katika nafasi hiyo?.

Eto'o

Samuel Eto'o wa Cameroon

Kulikuwa na mengi ya kushangaza hasa ukitilia maanani matarajio mengi yaliyowekwa kwa viungo Stephane Mbia na Jean Makoun.

Lakini Mbia alipewa dakika 45 tu na Makoun akaachwa katika mechi dhidi ya Misri. Nafasi hizo wakachukua Enoh Eyong na George Mandjeck mwenye umri wa miaka 21, ambaye aling’ara katika pambano dhidi ya Misri.

“Niliamua kutia damu changa ili kuleta nguvu mpya” akasema kocha Le Guen. “Mechi yetu na Misri ilionesha nilikuwa sahihi”.

Hatimaye kulifanyika mabadiliko katika ulinzi. Rigobert Song hakuanzishwa na vijana wapya Nicolas N’Koulou na Aurelian Chedjou wakakamata nafasi.

Lakini Cameroun wana tatizo la kufungwa mapema. Misri wakaonesha udhaifu wa golikipa Carlos Kameni, licha ya kwamba kwa kawaida huwa huwa ni kizuizi imara golini lakini si kwa Ahmed Hassan.

Rahim Ayew na Hans Sarpei walicheza vyema Angola licha ya vikwazo kadhaa.

Cha kutia moyo ni kuwa wachezaji wote 19 (outfield players) walionja ladha ya kucheza soka Angola ambako mwinuko kutoka usawa wa bahari katika mji wa Lubango ni mita 1750. Hali hiyo itawaweka katika hali ya kukabili mechi za kundi E. Katika mwinuko wa jiji la Bloemfotein dhidi ya Japan ambao ni mita 1400 na dhidi ya Denmark jijini Petoria mita 1275. Mechi ya mwisho dhidi ya Uholanzi itakuwa ni katika usawa wa bahari.

Lakini kama kuna timu iliyofaidika na michuano ya Angola ni Ghana.Wachezaji wake sita wa kikosi cha kwanza walikosekana, wakiwemo wote wa nafasi ya kiungo na walinzi mahiri wawili. Vijana wachanga wa Ghana waliopata nafasi ya kucheza waliikabili michuano kwa ujasiri kiasi kwamba uzoefu huo unaweza kuwasaidia wakati wa kombe la dunia watakapokuwa wakikabiliana na wapinzani wao wa kundi D, Ujerumani , Australia na Serbia.

Hali ya kisaikolojia ya Ghana ilitiliwa mashaka hapo awali lakini vijana kama Kojo Asamoah, Samuel Inkoom, Agyemang Badu na Opoku Agyemang walionesha ujasiri mkubwa wa kuzikabili mechi ngumu na inaashiria hali nzuri ya siku za baadae kwa soka ya Ghana.

Essien

Nahodha wa Ghana, Michael Essien

Timu ya Ghana imejengwa kutokana na kikosi cha vijana wa chini ya miaka 20 walionyakua kombe la dunia. Vijana sita kati ya walionza katika fainali dhidi ya Misri walikuwa na miaka 22 au chini. Lakini kwa kombe la Dunia inaweza isiwe rahisi kukamata nafasi ya kucheza. Hiyo ni kwa kuwa pia zile tofauti kati ya kocha Milovan Rajevac na Sulley Muntari zimemalizwa.

“Wanahitajika wachezaji wenye uzoefu kwa ajili ya kombe la Dunia.Tunao kama John Mensah, John Pantsil, Laryea Kingston, Michael Essien na Sulley Muntari. Wapo wengine pia” anasema kocha Milovan.

Baada ya michuano ya Angola, Milovan alilaumu ukosefu wa uzoefu kwa wachezaji wake lakini akasema kuwa anafurahia uzoefu waliopata vijana wale na kuamini kuwa utasaidia wakati wa kombe la dunia. Bila kuogopa kufanya maamuzi makubwa, kocha Milovan alionesha ubora wake pale timu ilipoweza kuingia fainali licha ya kuwa na majeruhi na changamoto nyingi.

Mafanikio yake makubwa ni kuweza kuwajenga wachezaji kucheza ki timu zaidi kuliko ilivyokuwa kwa timu zingine zitakazoiwakilisha Afrika katika Kombe a Dunia. Nani anajua mchango ambao ungetolewa na vijana wazoefu kama akina Essien, Muntari, Pantsil na wengine kama wangekuwa katika hali nzuri ya kuweza kucheza?

Kwa wengine wenye majina makubwa kama vile Drogba, Eto’o na Mikel ilikuwa ni hali ya kusikitisha. Je ni kwa sababu shauku ya kucheza katika kombe la mataifa ya Afrika kumezwa na aina ya maisha wanayoishi huko Ulaya? Au majina yao makubwa na hali ya soka Ulaya inaweza kuwa ndiyo sababu?

Kama siyo, je sababu ni nini? Lolote jibu liwalo naamini soka la Afrika katika fainali hizi za kombe la dunia litakuwa tofauti sana.

Tuesday, May 25, 2010

KOMBE LA DUNIA: IWEJE CONGO HAWAPO

Wakati bara la Afrika likiandaa michuano ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza, kuna jambo moja ambalo halijabadilika: wapenzi wa soka katika nchi za mashariki mwa Afrika na eneo la maziwa makuu wataendelea kuwaza na kuwazua waiunge mkono timu ipi, kwani hakuna nchi iliyofuzu kutoka eneo hilo.

Mara ya mwisho eneo hilo lilipowakilishwa katika kombe la dunia ilikuwa ni mwaka 1974 na nchi ya Zaire, ambayo leo ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Zaire ilikuwa nchi ya pili kutoka bara la Afrika kushiriki michuano ya kombe la dunia baada ya Morocco, iliyoshiriki mwaka 1970, lakini Leopards, kama ilivyojulikana timu hiyo ya Zaire, ilikuwa timu ya kwanza kutoka kusini mwa jangwa la Sahara kufuzu kwa kombe la dunia.

Ingawa haijawezekana tena kwa nchi hiyo kufuzu kushiriki kombe la dunia, wachezaji waliokuwa katika timu hiyo ya mwaka wa 74 bado hujivunia hilo mpaka leo.

‘’Kombe la dunia ni kilele cha soka, ndicho kitu ninachojivunia maishani mwangu kwa kushiriki mwaka 74, tulikuwa nchi ya kwanza ya watu weusi kushiriki kombe la dunia, na ni fahari ya kukumbuka siku zote.’’ Mohamed Kalambay, aliyekuwa kipa wa akiba wa Leopards aliambia BBC.

Mohammed Kalambayi

Mohammed Kalambayi anajivunia kuwa mmoja wa wachezaji walioiwakilisha Zaire katika Kombe la Dunia 1974.

Leopards walifungwa mabao 14 katika mechi tatu bila wao kufunga hata moja. Katika mechi yao ya kwanza walifungwa 2-0 na Scotland, kisha wakabugizwa 9-0 na Yugoslavia, na katika mechi yao ya mwisho wakafungwa 3-0 na Brazil.

Mwepu Ilunga alikuwa mlinzi katika timu hiyo, na ijapokuwa anaona fahari kwamba walifuzu kwenda kushiriki kombe la dunia, angali na machungu kuhusu waliokuwa maafisa wa shirikisho la soka Zaire, ambao anawalaumu kwa kuchukua pesa zilizotolewa na shirikisho la FIFA kwa wachezaji, kama mafao ya kushiriki.

‘’ Tulirejea nyumbani bila senti hata moja kama wachezaji. Kabla ya mchuano wetu dhidi ya Yugoslavia tulifahamu kwamba hatutalipwa, licha ya kufahamu kwamba FIFA walikuwa wameshawakabidhi fedha maafisa wetu. Kwanza tulikataa kucheza, na ilipolazimika kucheza, tulitembea tu uwanjani, na ndio sababu tukafungwa mabao 9.’’

Mwepu Ilunga

Mwepu Ilunga anakumbukwa kutoka na kituko cha kuondosha mpira kuepusha free-kick.

Mwepu aanakumbukwa kote duniani kwa kituko alichofanya katika mechi yao iliyofuatia, dhidi ya Brazil. Brazil ilipata free kick hatua chache kutoka lango la Zaire, wachezaji wa Zaire wakaweka ukuta wa ulinzi. Lakini refarii alipopiga kipenga ili Brazil kupiga free kick hiyo, Mwepu aliondoka kutoka ule ukuta wa ulinzi, akaupiga ule mpira na kuuondosha nje.

‘’ Sijuti hata kidogo, nilifanya kwa kusudi. Nilitaka nipewe kadi nyekundu ili niondoke uwanjani. Kwa nini nicheze kwa faida ya maafisa wa chama cha soka cha nchi yetu waliochukua fedha za wachezaji zilizotolewa na FIFA?. Ila sikufaulu , refa hakunipa kadi nyekundu.’’

Bila kufahamika yaliyotokea, lawama nyingi zilielekezwa kwa kocha wa Leopards Blagoj Vidinic kutoka Yugoslavia. Lakini aliyekuwa naibu kocha msaidizi wa timu ya Leopards Kabamba Nicodem aliambia BBC kitendo cha maafisa wa chama cha soka kuwalaghai wachezaji ndicho kilisababisha matokeo mabaya.

Peter Musembi (kushoto) akiwa na Nicodemu Kabamba

Ujuzi na busara za watu kama Kabamba Nicodemu (shati jekundu) unaweza kusaidia kuirejesha Kongo katika mafanikio ya miaka ya 1970.

Kabamba anasema kwa sasa nchi hiyo ina wachezaji wazuri lakini kinachowafanya kushindwa kwenda kushiriki kombe la dunia ni ukosefu wa maandalizi bora.

‘’Ukosefu wa mipango mahsusi ndio umesababisha nchi ya Congo kushindwa kushiriki katika mashindano makubwa kama vile kombe la mataifa ya Afrika na kombe la dunia; bila maandalizi bora huwezi kufanikiwa katika jambo lolote’’. Anasema Kabamba.

Kuna hamasa kubwa ya mpira wa vilabu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo miongoni mwa mashabiki, klabu ya TP Mazembe kutoka mji wa Lubumbashi kusini mwa nchi ndio mabingwa wa sasa wa Afrika, na vilabu vingine kama AS Vita Club na DC Motema Pembe vinavutia wachezaji kutoka nchi zingine.

Timu ya taifa ya nchi hiyo ndiyo mabingwa wa taji la Afrika kwa wachezaji wanaoshiriki ligi za nyumbani.

Haya yote yanaashiria uzito unaopewa soka katika Jamhuri ya Kidemorasia ya Congo, lakini swali linasalia kwa nini hawajaweza kurudi tena katika kombe la dunia tangu mwaka wa 1974?

Rais wa shirikisho la soka nchini Congo Constant Omar Selemani anasema ukosefu wa amani katika nchi, hali mbaya ya kiuchumi na kupuuzwa kwa soka ya vijana kwa kipindi kirefu kulikwamisha maendeleo ya soka katika nchi hiyo.

Constantine Omar Selemani

Constantine Omar Selemani rais wa shirikisho la soka la Congo ana jukumu kubwa la kuirejesha nchi hiyo katika michuano ya Kombe la Dunia.

‘’Maendeleo ya soka yanakwenda kulingana na hali ya nchi, kijamii na kiuchumi. Wakati Zaire ilipofuzu kwa kombe la dunia mwaka wa 74 uchumi wa nchi ulikuwa mzuri, lakini tangu wakati huo kumekuwa na matatizo mengi katika nchi.’’

‘’Pia viongozi wa wakati ule walikosa maono ya kukuza wachezaji wapya. Wale wachezaji walioshiriki kombe la dunia walitaka kwenda kucheza soka ya kulipwa katika nchi za nje, lakini Rais Mobutu akawakataza, akawalazimisha kukaa nyumbani. Wengine waliacha kucheza, na kukawa hakuna mpango wa kukuza vijana wengine’’. Anaelezea Bw Selemani.

Rais huyo wa shirikisho la soka nchini Congo, ameahidi kwamba nchi yao itakuwepo kwenye mashindano ya kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil.

Saturday, May 15, 2010

YANGA YAPOKEA OFA YA NGASA


Yanga SC imeonesha kukomaa baada ya kuipokea ofa ya Azam FC na kwa mujibu wa mwenyekiti wake Imani Madega, “wao kama Yanga hawana mpango wa kumzuia Ngasa na mchezaji yoyote atakayependa kuhama kwani kuhama kwao kutatoa nafasi kwa Yanga kusajiri wachezaji wengine nyota.
Suala la Ngasa kusajiliwa Azam FC limezuka kama filamu, na sasa limekuwa likifuatiliwa na wapenzi wengi wa Mchezo wa mpira wa miguu, awali leo mchana, Azam FC imepeleka barua ya kuomba kumsajili Ngasa ikiwa na ofa ya 25 Milioni. Kiasi hiki ni kikubwa sana kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya usajiri wa wachezaji kwani Ngasa amebakisha mwaka mmoja tuu na sheria za FIFA zinamruhusu mchezaji aliyebakisha mwaka mmoja kuunnua mkataba wake kwa kuilipa klabu aliyokuwa akiichezea mshahara wote uliobaki. Lakini Azam FC licha ya kufahamu sheria hiyo bado imeonesha uungwana na nia njema kwa kuamua kutoa ofa nzuri ambayo ni rekodi nchini.
Juma kaseja ndiye anayeshikiria rekidi ya uhamisho ambapo Uhamishowake kwenda Yanga uliigharimu timu hiyo ya Jangwani Milioni 24 na kama deal hili la Ngasa litafanikiwa basi Yanga na Ngasa watakuwa wakishikilia rekodi ya usajiri wa fedha nyingi kwa wachezaji wa ndani.
Gazeti la Mwanaspoti nalo lina habari kuwa, nanukuu “MAMILIONI ya fedha aliyoahidiwa na klabu ya Azam yamemrudisha nyumbani Mrisho Ngassa na jana alitarajiwa kukutana na uongozi wa Yanga na kuwaelezea nia yake ya kutaka kutosajiliwa tena na klabu hiyo msimu ujao.



Ngassa alisema jana kuwa ameamua kurejea nyumbani baada ya kuona kuwa fedha alizopewa na APR ya Rwanda ni ndogo zikilinganishwa na zile alizoahidiwa na Azam.



'' Kweli tulifanya mazungumzo na APR wiki hii, lakini walikuwa wanasuasua kunipa fedha ambayo niliitaka mimi na nilipofuatwa na Azam wakanieleza dau kubwa zaidi, ndipo nikaona nisipoteze muda bora nije kuzungumza nao, '' alisema Ngassa ambaye amekuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu uliopita.



Alisema kuwa alitarajia kukutana na uongozi wa Yanga ili kuwaeleza nia yake ya kutua Azam na kuwaweka wazi fedha anazopata na kuwaomba wamruhusu kwani mpira ni ajira kwa sasa.


'
' Kwa sasa mimi ndio najitengenezea maisha yangu mpira ukiisha hapa sijafanya kitu chochote kesho na kesho kutwa nitavyokuwa naomba omba watu wananisema sana, hivyo naomba viongozi wa Yanga wanielewe na kuniruhusu kuichezea Azam msimu ujao,'' alisema.



Pia, aliongeza kuwa uamuzi wake anaamini kuwa ni sahihi kutokana na fedha alizoahidiwa kuwa ni nyingi na anaamini kuwa Yanga hawawezi kumsajili kwa fedha hizo hata iweje.

"Ni zaidi ya fedha ambazo walitaka kunipa APR ambao katika maongezi ya mwanzo walikubaliana nami Shilingi 20 na Azam wananipa zaidi ya hapo.



"Ninawaomba mashabiki wa Yanga wakubaliane na uamuzi wangu huo kwa ajili ya maisha yangu na ukizingatia nimeitumikia kwa miaka mingi timu hiyo tena kwa moyo mmoja hivyo wasiupokee vibaya uamuzi wangu huo," alisema.



Alisema hana shida na viongozi wake anaamini pindi watakapokutana na wenzao wa Azam watafika muafaka na kumruhusu kwa moyo mmoja kuichezea timu hiyo ambayo imekuwa na upinzani kwenye ligi msimu uliopita.



Hata hivyo, mchezaji huyo alitangaza dau lake kupitia gazeti la Mwanaspoti kuwa yupo tayari kuondoka Yanga endapo klabu inayomtaka iko tayari kutoa Shilingi 40 milioni.

SENYONJO ATUA AZAM FC


AZAM FC ya Dar es Salaam imefanikiwa kumsajiri nyota wa kimataifa wa Uganda ambaye ni mshambuliaji hatari wa timu ya ya Polisi ya Uganda, Peter Senyonjo ambaye alikuwa akihusishwa na Yanga kwa misimu miwili mfululizo iliyopita.
Senyonjo ambaye anatisha kwa kuzifumania nyavu za timu pinzani anatarajiwa kutengeneza partnership ya hatari na John Raphael Boko Adebagoals amabye kama siyo kukosa baadhi ya mechi kutokana na kuwa Israel kwa majaribio basi angekuwa mfungaji bora msimu huu.

kwa mujibu wa gazeti la mwanaspoti, Yanga walikuwa wamepania kumsajili mchezaji huyo msimu wa 2007 na 2008 lakini wakashindwa kutokana na kutokuwa makini kwenye ufuatiliaji lakini wikiendi iliyopita timu ya Azam imemshusha Dar es Salaam na kumsainisha mkataba wa mwaka mmoja.

Mchezaji huyo mzoefu na tegemeo kwenye timu ya Taifa ya Uganda, alikuwa jijini Dar es Salaam wikiendi iliyopita kukamilisha uhamisho wake na ameshakwea pipa kurejea Kampala.

Meneja wa Azam, Ibrahim Jeshi amesema kuwa kila kitu kimekwenda vizuri na mchezaji huyo amerejea kwao kukamilisha mambo mengine.

Senyonjo amejijengea umahiri mkubwa akiwa na timu hiyo ya Police kwenye michuano ya kombe la kagame na timu ya Taifa katika chalenji.
Wakati huo huo, beki mahiri wa timu ya Taifa Stars Nadir Haroub Canavaro yupo katika hatua za mwisho za kujiunga za Azam FC, Canavaro mwenyewe ameshatamka wazi kuwa dhamira yake ni kuichezea Azam FC msimu ujao

CHELSEA MABINGWA KOMBE LA FA


Carlo Ancelotti ameweka rekodi wakati Didier Drogba alipopachika bao kipindi cha pili na kuizamisha Portsmouth hali iliyoifanya Chelsea kuweka kibindoni makombe mawili, ubingwa wa Ligi ya England na Kombe la FA.

Shuti la Drogba la adhabu ya moja kwa moja alilopiga kiufundi ndio liliamua ushindi kwa Chelsea katika mchezo ambao Chelsea walikosa mabao mengi kipindi cha kwanza ambapo mpira ulikuwa ukigonga nguzo ya goli mara kwa mara ambapo pia timu zote zikikosa kufunga mikwaju ya penalti.

Chelsea ambayo inakuwa klabu ya saba kushinda makombe mawili katika msimu mmoja, kwa mara nyingine ilikuwa na kila jambo la kumshukuru mshambuliaji wao hatari Drogba, ambaye amezidi kuweka rekodi ya kufunga katika michezo sita iliyopia kwenye uwanja wa Wembely huku msimu huu akiwa amefunga mabao 37.

Alifunga dakika chache tu baada ya Portsmouth kukosa mkwaju wa penalti ambapo Kevin-Prince Boateng alipiga mkwaju usio wa kiufundi na kuokolewa na mlinda mlango wa Chelsea Petr Cech na ule wakati ambapo Pompey ilionekana kurejea kile ilichofanya miaka miwili iliyopita ukipotea.

Chelsea nayo ilikosa kufunga bao la pili kwa kwaju wa penalti baada ya Frank Lampard kuangushwa na Michael Brown na mkwaju wake kwenda nje.

SERENGETI BREWERIERS YAZINDUA BIA MPYA (UHURU PEAK LAGER)




Mwenyekiti wa kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers Jaji Mark Bomani kulia pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo Shantanu Chitgopkar wakionyesha mfano wa bia ya Uhuru Peak Lager jana mara baada ya kuzinduliwa rasmi jijini Dar es salaam kwenye Hoteli ya Movenpick, bia hiyo kwa sasa inapatikana kwenye baa mbalimbali na ina kilevi asilimia 5.8 haya kazi kwenu watumiaji wa kilaji endeleeni kujimwaga na Uhuru Peak Lager
Kocha wa timu ya taifa Taifa Stars Marcio Maximo akiwa na maiwaifu wake.


WADAU KAMA TULIKUWA CHIMBO HIVI!!!

WADAU WA VIWANJANI KAMA TULIKUWA CHIMBO HIVI KWA MAJUMA KADHAA SASA TUNAREJEA TENA

TUMEREJE TENA

NI MAHABARI YA MICHEZO ZAIDI

KARIBU

Saturday, April 24, 2010

WASHINDI 21 WAPATIKANA ZAIN AFRCAN CHALLENGE

Afisa mawasiliano ya ndani wa Zain Tanzania Dangio Kaniki (kushoto) akimkabidhi simu ya mkononi mshindi katika shindano la kujibu maswali kwa njia ya SMS wakati wa kipindi cha Zain Africa Challenge, Juma Mustafa wa Dar es Salaam baada ya kuibuka mshindi. Shindano hilo limeapata jumla ya washindi 23 kutoka sehemu mbalimbali nchini. Kulia ni meneja wa huduma za jamii wa Zain,Washindi katika shindano la kujibu maswali kwa njia SMS wakati wa shindano la Zain Africa Challenge yanayoonyeshwa katika luninga ya TBC 1 wakiwa katika picha ya pamoja bada ya kukabidhiwa zawadi zao katika makao makuu ya ofisi za Zain jijini Dar es Salaam. Kushoto afisa mawasilano ya ndani wa Zain Dangio Kaniki na kulia ni meneja wa huduma za jamii wa Zain, Tunu Kavishe.Afisa mawasiliano ya ndani wa Zain Tanzania Dangio Kaniki (kushoto) akimkabidhi simu ya mkononi mshindi katika shindano la kujibu maswali kwa njia ya SMS wakati wa kipindi cha Zain Africa Challenge, Salvatory Mkami wa Dar es Salaam baada ya kuibuka mshindi. Shindano hilo limeapata jumla ya washindi 23 kutoka sehemu mbalimbali nchini. Kulia ni meneja wa huduma za jamii wa Zain.

Wednesday, April 21, 2010

MAXIMO ATANGAZA KIKOSI KITAKACHOIVAA RWANDA

kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania TFF Marcio Basilio Maximo (katikati) akitangaza majina ya timu ya Taifa itakayoingia kambini kujiandaa na mchezo wa kufuzu michuano ya CHAN ambayo inajumuisha wachezaji wa ndani, timu ya Tanzania inataraji kukutana na Rwanda.

wachezaji waliyoitwa ni pamoja na.

Golikipa
Shabani Kado Mtibwa
Jackson Chove JKT

FULLBACKS
Shadrack Nsajigwa Yanga
Salum Kanoni Simba
Juma Jabu Simba
Stephano Mwasika Moro UTD

CENTER BACKS
Nadir Haroub (Canavaro) Yanga
Kevin Yondani Simba
Aggrey Morris Azam Fc
David Naftal Simba
Dickson Daudi Mtibwa

MIDFIELDERS
Erasto Nyoni Azam
Nurdin Bakari Yanga
Jabir Aziz Simba
Ibrahim Mwaipopo Azam
Kigi Makasi Yanga
Shaban Nditi Mtibwa
Abdi Kassim Yanga
Uhuru Suleiman Simba
Selemani Kassim Azam

FORWARDS
Mrisho Ngassa Yanga
John BOcco Azam
Mussa Mgosi Simba
Jerson Tegete Yanga
MIchael Mgimwa Moro UTD U-20
Yusuf Abbas Soka African Lyon U-20
Joanas Kajuna African Lyon U-20

SOKA KJUTUMIKA KUPAMBANA NA MALERIA TANZANIA

Raisi wa shirikisho la kandanda Tanzania Leodga Chilla Tenga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari za michezo wakati wa ufunguzi wa Semina ya MALERIA HAIKUBALIKI, kushoto ni katibu mkuu wa TFF Fredrick Mwakalebela, na kulia ni Anne mratibu wa Marelia Haikubaliki.

Tenga amesema michezo inanafasi kubwa ya kupambana na Maleria kufuatia kuhusisha watu wengi, lakini mchezo wa mpira licha ya kuchezwa dakika 90 hutajwa na kuzungumzwa zaidi ya dakika 90.
Tenga ametolea mfano mchezo wa Simba na Yanga licha ya kuchezwa Jumapili ya tarehe 18 lakini hadi leo bado unajadiliwa, hivyo kupambana na Maleria kupitia michezo itakuwa ni rahisi zaidi kuwafikia watu wengi zaidi pengine kuliko njia yeyote.
Amesema Tayari wamekwishaanza kutoa mafunzo kwa wachezaji wa timu ya taifa TAIFA STARS na wamewateua kuwa mabalozi wa MALERIA HAIKUBALIKI lakini pia wamewagawia vyandarua, wamefanya hivyo pia kwa timu ya U-20 pamoja na timu tisa zilizoshiriki ligi daraja la kwanza dhidi ya matumizi ya chandarua ikiwa ni kinga ya kwanza.

UZINDUZI WA "UHURU WA KUONGEA" WA ZAIN WAFANA J-MARTIN AFANYA KWELI

Huyu ni J-Martin akitoa burudani wakati wa uzinduzi wa UHURU WA KUONGEA katika jengo jipya la Zain, kiukweli jukwaa lilipendeza sana, watu nyomi, full kujiachia na ZAIN

Hapa Brother J-Martin akikamua kitu cha OYOYO wacha Bwana

Kama vipi tucheze pamoja jamani.....




Chidi Benzi kutoka Ilala aliwakilisha vema kwa upande wa wasanii wa Tanzania, jambo la kupongezwa ni kuweza kupiga bonge la shoo akiwa na bendi yake LIVE.Dar es Salaam Stand up, put yo hands up heya heee Dar es Salaam Stand up put yo hands up chichichichi chidi Benziii yoooooo
Sumu ya penzi ukishailambaa hata kwa maziwa huwezi kukuna" ndivyo anavyoimba Belle 9 wakati wa uzinduzi wa UHURU WA KUONGEA wa ZAIN.

Tuesday, April 20, 2010

RATIBA KILI TAIFA CUP 2010 HII HAPA

Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,David Minja akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufanyika kwa droo ya mashindano ya Kili Taifa Cup katika ukumbi wa mikutano wa TFF leo,wengine ni Salim Madadi (kulia) na Iddy Mshangama wote ni Maafisa wa TFF.

FIXTURE KILI TAIFA CUP - 2010

GROUP 'A' - DODOMA
(a) Dodoma
(b) Kigoma
(c) Singida
(d) U - 20

SN - DATE - CODE - TEAMS - TIME - GROUND
1. 5/8/2010 A/B Singida V/S U-20 14:00 HRS JAMHURI ST.
2. 5/8/2010 C/D Dodoma V/S Kigoma 16:00 HRS JAMHURI ST.
5/9/2010 REST DAY

3. 5/10/2010 B/C U-20 V/S Dodoma 14:00 HRS JAMHURI ST.
4. 5/10/2010 D/A Kigoma V/S Singida16:00 HRS JAMHURI ST.

5/11/2010 REST DAY

5. 12-May A/C Singida V/S Dodma 14:00 HRS JAMHURI ST.
6. 12-May-10 D/B Kigoma V/S U-20 16:00 HRS JAMHURI ST.

GROUP 'B' - TANGA
(a) Tanga
(b) Morogoro
(c) Pwani
(d) Temeke

SN - DATE - CODE - TEAMS - TIME - GROUND
1. 5/8/2010 A/B Tanga V/S Morogoro 14:00 HRS MKWAKWANI
2. 5/8/2010 C/D Pwani V/S Temeke 16:00 HRS MKWAKWANI

5/9/2010 REST DAY

3. 5/10/2010 B/C Morogoro V/S Pwani 14:00 HRS MKWAKWANI
4. 5/10/2010 D/A Temeke V/S Tanga 16:00 HRS MKWAKWANI

5/11/2010 REST DAY

5. 12-May A/C Tanga V/S Pwani 14:00 HRS MKWAKWANI
6. 12-May-10 D/B Temeke V/S Morogoro 16:00 HRS MKWAKWANI

GROUP 'C' - MWANZA
(a) Mwanza
(b) Kagera
(c) Shinyanga
(d) Tabora

SN - DATE - CODE - TEAMS - TIME - GROUND
1. 5/8/2010 A/B Shinyanga V/S Kagera 14:00 HRS C.C.M. KIRUMBA
2. 5/8/2010 C/D Mwanza V/S Tabora 16:00 HRS C.C.M. KIRUMBA

5/9/2010 REST DAY

3. 5/10/2010 B/C Kagera vs Mwanza 14:00 HRS C.C.M. KIRUMBA
4. 5/10/2010 D/A Tabora vs Shinyanga 16:00 HRS C.C.M. KIRUMBA

5/11/2010 REST DAY

5. 12-May A/C Shinyanga vs Mwanza 14:00 HRS C.C.M. KIRUMBA
6. 12-May-10 D/B Tabora V/S Kagera 16:00 HRS C.C.M. KIRUMBA


GROUP 'D' - ARUSHA
(a) Arusha
(b) Mara
(c) Manyara
(d) Kilimanjaro



SN - DATE - CODE - TEAMS - TIME - GROUND
1. 5/8/2010 A/B Mara V/S Kilimanjaro 14:00 HRS SHEKH AMRI ABED
2. 5/8/2010 C/D Manyara V/S Arusha 16:00 HRS SHEKH AMRI ABED

5/9/2010 REST DAY

3. 5/10/2010 B/C Kilimanjaro V/S Manyara 14:00 HRS SHEKH AMRI ABED
4. 5/10/2010 D/A Arusha V/S Mara 16:00 HRS SHEKH AMRI ABED

5/11/2010 REST DAY

5. 12-May A/C Mara V/S Manyara 14:00 HRS SHEKH AMRI ABED
6. 12-May-10 D/B Arusha V/S Kilimanjaro 16:00 HRS SHEKH AMRI ABED

GROUP 'E' - IRINGA
(a) Iringa
(b) Mbeya
(c) Rukwa
(d) Kinondoni

SN - DATE - CODE - TEAMS - TIME - GROUND
1. 5/8/2010 A/B Rukwa V/S Mbeya 14:00 HRS SAMORA ST.
2. 5/8/2010 C/D Iringa V/S Kinondoni 16:00 HRS SAMORA ST.

5/9/2010 REST DAY

3. 5/10/2010 B/C Mbeya V/S Iringa 14:00 HRS SAMORA ST.
4. 5/10/2010 D/A Kinondoni V/S Rukwa 16:00 HRS SAMORA ST.

5/11/2010 REST DAY

5. 12-May A/C Rukwa V/S Iringa 14:00 HRS SAMORA ST.
6. 12-May-10 D/B Kinondoni V/S Mbeya 16:00 HRS SAMORA ST.


GROUP 'F' - MTWARA
(a) Mtwara
(b) Lindi
(c) Ruvuma
(d) Ilala

SN - DATE - CODE - TEAMS - TIME - GROUND
1. 5/8/2010 A/B Lindi V/S Ruvuma 14:00 HRS NANGWANA ST.
2. 5/8/2010 C/D Mtwara V/S Ilala 16:00 HRS NANGWANA ST.

5/9/2010 REST DAY

3. 5/10/2010 B/C Ruvuma V/S Mtwara 14:00 HRS NANGWANA ST.
4. 5/10/2010 D/A Ilala V/S Lindi 16:00 HRS NANGWANA ST.

5/11/2010 REST DAY

5. 12-May A/C Lindi VS Mtwara 14:00 HRS NANGWANA ST.
6. 12-May-10 D/B Ilala VS Ruvuma 16:00 HRS NANGWANA ST.



FIXTURE KILI TAIFA CUP - 2010
QUARTER, SEMI FAINAL AND FAINAL
KILIMANJARO TAIFA CUP 2010
FROM 23 MAY, 2010 TO 29 MAY, 2010
UHURU STADIUM - DAR ES SALAAM

SN - DATE - TEAMS - TIME - GROUND
QUARTER FINAL

1. 23 May, 2010 WINNER GROUP 'A' V/s WINNER GROUP 'B' 14:00 HRS UHURU ST - DSM
2. 23 May, 2010 WINNER GROUP 'C' V/s WINNER GROUP 'D' 16:00 HRS UHURU ST - DSM
3. 24 May, 2010 WINNER GROUP 'E' V/s WINNER GROUP 'F' 14:00 HRS UHURU ST - DSM
4. 24 May, 2010 WINNER GROUP 'G' V/s WINNER GROUP 'H' 16:00 HRS UHURU ST - DSM

SEMI FAINAL

5. 25 May, 2010 WINNER GROUP 'A' V/s WINNER GROUP 'B' 16:00 HRS UHURU ST - DSM
6. 26 May, 2010 WINNER GROUP 'C' V/s WINNER GROUP 'D' 16:00 HRS UHURU ST - DSM

27 May, 2010 REST DAY

7. 28 May, 2010 LOOSER No. '5' V/s LOOSER No. '6' 16:00 HRS UHURU ST - DSM
8. 29 May, 2010 WINNER GROUP '5' V/s WINNER GROUP '6' 16:00 HRS UHURU ST - DSM

OKINAWA GOJU RYU KARATE - DO - JUNDOKAN KURO OBI KAI DOJO WAADHIMISHA MIAKA 37 TANZANIA

OKINAWA GOJU RYU KARATE - DO - JUNDOKAN KURO OBI KAI DOJO waadhimisha miaka 37 tangu kuanzishwa kwa dojo hilo mwaka 1973 na Sensei Nantambu Camara Bomani.Hii ni picha ya muasisi wa mchezo huu hapa Tanzania Sensei Nantambu Camara Bomani.Hawa ndiyo wanaoendeleza mchezo huu wa GOJU RYU katika dojo ambalo Sensei Bomani alianzisha mchezo huu nchini Tanzania katika shule ya msingi ya Zanaki ya Jijini Dar es Salaam.Hawa ni wale ambao wanamikanda myeusi wakionyesha namna ambavyo mtu anaweza kupambana na mtu mwenye kisu na ukamshinda, aliyelala chini ndiye mwenye kisu.Hawa ni wale wenye mikanda ya Kijani wakionyesha umahiri wao katika mchezo wa Goju Ryu ama unaweza ukaiata sanaa ya mipigano.Hawa ni wale ambao wanakaribia kuwa na mkanda Mweusi wakionyesha umahiri wao katika sanaa ya mapigano.Huyu ni Japhet Kaseba Bingwa wa Kick Boxing wa WK1 Dunia naye akifuatilia kwa makini.Mdau mwenzangu huyu Ankal Michuzi naye akifuatilia kwa ukaribu namna mtu anavyoweza kupigana kwa ustadi bila kutumia silaha, au siyo Brother Michuzi...???Waliyo kaa chini ndiyo ambao walitunukiwa mikanda ikiwa ni ishara ya kupandishwa ngazi katika mchezo huo, huku mmoja akipewa mkanda mweusi, aliyesimama kulia ni Sensei Rashid Almasi na aliyening`iniza mewani watano toka kulia ni Sensei Wilfred Malekiu.

J-MARTIN AWASILI BONGO TAYARI KWA BURUDANI YA ZAIN

Mwanamuziki kutoka Nigeria J-Martins kulia akiongea wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere. Msanii huyo ambaye yuko nchini kwa mwaliko wa Kampuni ya simu za mkononi ya Zain alitarajia kufanya onyesho jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja uhusiano wa Zain Muganyizi Mutta.

Monday, April 19, 2010

ZAIN YASAIDIA ELIMU, YATOA VITABU VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 4 TANGA

Mkuuu wa wilaya ya Lushoto Sophia Mjema (katikati) akimkabidhi Frank Glibety mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Kisaba iliyopo wilayani humo vitabu vyenye thamani ya Shilingi milioni 2 ambavyo vimetolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Zain kupitia mradi wake wa “Build Our Nation”. Kwa ajili ya shule hiyo ya Kisaba na shule ya sekondari ya Vugabazo mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Zain, Muganyizi Mutta.

Mkuu wa wilaya ya Lushoto Sophia Mjema (katikati) akimkabidhi Juma kibwana mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Vugabazo iliyopo wilayani humo wiki hii. Vitabu vyenye thamani ya Shilingi milioni 2 ambavyo vimetolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Zain kupitia mradi wake wa “Build Our Nation”. Kwa ajili ya shule hiyo ya Vugabazo na shule ya sekondari ya Kisaba mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Zain, Muganyizi Mutta.

SIMBA OYEEEEEEEEEEE.......



Nahodha wa Simba Nicodemus Nyagawa (kushoto ) na mlinzi wa timu hiyoJuma Jabu wakishangilia huku wakiwa wambeba Kombe la Ubingwa wa LigiKuu ya Bara mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaamjana.Katika mchezo huo Simba iliicharaza Yanga mabao 4-3. (Picha naMohamed Mambo)
Mbali na ushindi huo Simba ilikuwa inakabidhiwa kombe lake mara baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi kuu ya Vodacom msimu huu bila kufungwa hata mchezo mmoja ambapo imeshinda michezo 19 imedroo miwili na bado ina mchezo mmoja mkononi wa kukamilisha ratiba dhidi ya Mtibwa Sugar ya Manungu Mkoani Morogoro.
Katika mchezo wa jana wachezaji watatu walipewa kadi nyekundu ambao ni Wisdom Ndlovu na Amir Maftaha wa Yanga baada ya kucheza mchezo mbaya dhidi ya wachezaji wa Simba Salm Kanoni na Juma Kaseja wakati Hilary Echesa wa Simba alipewa kadi nyekundu baada ya kuvua jezi alipokuwa akishangilia goli la nne alilofunga dhidi ya Yanga.

Thursday, April 15, 2010

ULINZI YASHIKILIA USUKANI LIGI KUU YA KENYA

Klabu ya ligi kuu ya Kenya Ulinzi Stars na Mathare United ndiyo klabu pekee ambazo hazijapoteza mchezo tangu kuanza kwa msimu wa ligi mapema mwezi Februari.

Hata hivyo klabu hizi mbili zimeachana kwa tofauti kubwa ya pointi ambapo klabu ya Ulinzi inashikilia usukani wa ligi huku Mathare ikishika nafasi ya 5.

IKiwa tayari imechezwa michezo nane hadi sasa katika ligi kuu ya Kenya, Ulinzi Stars inaongoza ikiwa na jumla ya pointi 18, ikiwa ni pointi mbele dhidi ya Tusker FC inayoshika nafsi ya pili.Sofapaka inashika nafasi ya 3 ikiwa na jumla ya pointi 14. Sony Sugar inashika nafasi ya 4 huku ikiwa na point 13 wakati Mathare United ikiwa na pointi 12 ikilala nafasi ya 5 katika msimamo wa ligi.

Gor Mahia inashika nafasi ya 6 ikilingana pointi na klabu ya Mathare United lakini wakitofautiana magoli ya kufunga wakati Nairobi City stars, Western Stima na Sher Karuturi Sports zinashika nafasi ya 7, 8 na 9 zikiwa na pointi 11 kila moja. klabu ya KCB maarufu kwa jina la The Bankers wanahitimisha kumi bora wakishika nafasi ya kumi katika msimamo ikiwa na pointi kumi baada ya michezo ya wikiendi.

Wakati huo huo, Kongowea imefanikiwa kutwaa ubingwa wa kanda ya Pwani katika michuano ya Copa Coca Cola (Coast Province 2010 COPA Coca-Cola) baada ya kuichapa Gede FC 5-4 kwa mikwaju ya penati katika mchezo uliyopigwa katika dimba la Manispaa ya Mombasa.

Kwa upande wasichana, Furaha Ladies inashika nafasi ya kwanza, baada ya kuichapa Mwakitawa Ladies 1-0.

Jijini Nairobi, kipute kilipigwa Posta Grounds ambapo Indomitable FC ilitwa ubingwa wa jumla baada ya kuichapa Korogocho Youth 3-2 kwa mikwaju ya penati wakati wasichana, Dhapks United walitawazwa mabingwa baada ya kuitoa Pioneer Girls kwa goli la ugenini.

mabingwa waliondoka na kitita cha Shilingi za Kenya 30,000 na kila mshindi wa pili aliweka kibindoni Shilingi za Kenya 20,000.

RENARD AWEKA MIPANGO YA 2012 MATAIFA YA AFRIKA

Kocha mpya wa timu ya taifa ya Angola Herve Renard amejiwekea malengo ya kutaka kufuzu kucheza mataiafa ya Afrika mwaka 2012 kuwa ni kiwango cha kati katika malengo ya mafunzo kwa Palancas Negras.

katika mahijiano yaliyofanyika nyumbani kwake mjini Luanda, Mfaransa huyo amewaomba wananchi wa Angolan kuwa na subira katika kipindi hiki, na kusema "much work to be done" kuijenga upya timu ya taifa ya Angola.

Kocha huyo wa zamani wa Zambia wiki iliyopita alitajwa kuchukua nafasi ya kocha Manuel Jose, Mreno ambaye aliiongoza Angola katika fainali za mataifa ya Afrika mwezi januari.

Jose aliondoka baada ya tumaini la Angola la kutwaa uchampion wa mataifa ya Afrika kutoweka huku michuano ikipigwa katika ardhi ya nyumbani, walitolewa katika hatua ya robo fainali na timu ya taifa ya Ghana.

CARLOS TEVEZ, WAYNE ROONEY, CESC FABREGAS NA DIDIER DROGBA KUWANIA TUZO YA MWANASOKA BORA WA MWAKA

Carlos Tevez, Wayne Rooney, Cesc Fabregas na Didier Drogba wametajwa kuwania tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka inayotolewa na na chama cha wachezaji wa kulipwa (PFA Player of the Year award).

Rooney ndiye anayepewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo.

Nyota huyo wa Manchester United amekuwa na wakati mzuri msimu huu, ingawa inaonekana kanakwamba mafanikio ya kusonga mbele katika michuano ya Carling Cup kudoda. Rooney amefunga jumla ya magoli 34 akiwa na klabu yake ya Man United msimu huu katika michuano yote na yeye mwenyewe kkujitaja kuwa ni moja ya wachezaji wenye kipaji Duniani.

Klabu ambayo msimu huu imekuwa tishio katika ligi kuu ya England, Manchester City inawakilishwa na Carlos Tevez, ambaye naye tangu ajiunge na klabu hiyo ni mwenye mafanikio na kufanikiwa kufunga jumla ya magoli 28 katika michuano yote.

Kama Rooney, Nyota wa klabu ya Arsenal Cesc Fabregas amechaguliwa kuwania tuzo mbili ikiwa ni tuzo kuu ya mwanasoka bora na tuzo ya mwanasoka chipukizi wa mwaka.

Ingawa amekuwa akikalia benchi muda mwingi msimu huu akiuguza maumivu, Fabregas amekuwa chachu ya ushindi katika michezo mingi ya klabu hiyo ya washika bunduki.

Wakipewa jina la muda, yaani Mabingwa wateule, Chelsea inawakilishwa na Didier Drogba licha kutofanya vizuri sana kama ilivyokuwa mwaka uliyopita, lakini bado anatajwa kuwa ni mwiba katika lango la wapinzani.

Aston Villa inawakilishwa na James Milner na Birmingham City inawakilishwa Joe Hart ambao wanawania tuzo mwnasoka mdogo pamoja na Rooney na Fabregas

Wednesday, April 14, 2010

SBL YAIKABIDHI NGORONGORO HEROES MILIONI 83/


Meneja uhusiano Habari na Mawasiliano wa Serengeti SBL Teddy Mapunda kulia akimkabidhi vifaa mbalimbali vya michezo Kapteni wa timu ya Vijana Ngorongoro Heroes Himid Mao kwenye ofisi za shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF leo, katikati ni kocha mkuu wa timu hiyo Rodrigo Stokla na mwisho kushoto ni Matadi Yasoda Kaimu mkurugenzi Idara ya Michezo Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo.


Kampuni ya bia ya Serengeti SBL leo imetoa jumla ya shilingi milioni 83 kwa shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF ili kufanikisha maandalizi ya timu ya taifa ya vijana Ngorongoro Heroes chini ya Umri wa miaka 20 katika maandalizi ya safari yao kwa ajili ya mchezo wake na timu ya vijana ya nchini Malawi.

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja uhusiano habari na Mawasiliano wa kampuni hiyo Tedd Mapunda amesema katika fedha hizo shilingi milioni 50 ni fedsha taslimu kwa ajili ya masuala ya utawala na shilingi milioni 25 kwa ajili ya kulipia tiketi na shilingi milioni 8 zimetumika kwa ajili ya vifaa vya michezo kwa timu hiyo.

"Kama ambavyo tumekuwa tukisaidia michezo tumeona tuisaidie timu hii ya vijana chini ya miaka 20 kwani tunaamini msaada huu utasaidia kujenga na kuimarisha kikosi bora cha timu ya taifa miaka michache ijayo" amesema Tedy Mapunda.

Ameongeza kuwa tunawatakia Ngorongoro Heroes mafanikio katika mchezo wao huo utakaofanyika katika jiji la Blantyre nchini Malawi na tuna imani kuwa watarudi na ushindi hivyo kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania, Ngorongoro Heroes inatafuta tiketi ya kushiriki kombe la mataifa ya afrika kwa timu za vijana chini ya umri wa miaka 20 katika fainali zinazotarajiwa kupigwa nchini Misri mwaka 2011.

Kampuni ya bia ya Serengeti SBL ni mdhamini mkuu wa timu ya taifa ya mpira wa miguu Taifa Stars kwa miaka kadhaa sasa na chini ya udhamini huo mafanikio ya timu ya taifa yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka hivyo SBL wanastahili kupongezwa kwa udhamini huo.

TIMU YA TAIFA YA VIJANA U-20 KUONDOKA KESHO

TIMU ya Taifa ya vijana chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroez leo imekabidhiwa bendera ya taifa na Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya michezo Juliana Matagi Yasoda ikiwa ni ishara ya kikosi hicho kwenda kuiwakilisha nchi kwenye mchezo wa awali wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Africa kwa vijana dhidi ya Malawi,mchezo utakaopigwa Jumamosi huko Malawi.

Ngorongoro Heroes itaondoka kesho ikiwa na jumla ya wachezaji 20 na viongozi saba msafara utakaoongozwa na mwenyekiti wa maendeleo ya soka la Vijana Alhaji Ahmed Msafiri Mgoyi.

Akizungumza baada ya kukabidhi bendera Matagi Yasoda amewataka vijana hao kurudi na ushindi.

Rais wa Shirikisho la soka nchini TFF Leodger Tenga amesema kikosi hicho ndio Taifa Starz ya baadaye.

WACHEZAJI WATAKAOONGOKA KESHO NI
1. KHOMEINY ABUBAKARI
2. AMANI KYATA
3. LEORNAD MUYINGA
4. TUMBA SWEDI
5. KIBANDA JUKUMU JOAKIM
6. HIMID MAO
7. ISSA RASHID ISSA
8. JOHANES SALVATORY
9. ABUU UBWA ZUBERI
10. FURAHA YAHAYA TEMBO
11. THOMAS ULIMWENGU
12. SALUM ABDULL TELELA
13. ABDALLAH BUNU
14. MBWANA SAMATA
15. YUSUPH SOKA
16. RAJABU ISIHAKA ABDALLA
17. MOHAMMED HAMIS THABIT
18. OMEGA SEME
19. SALUM ABUBAKARI
20. SWALEHE KABARI FARAJI

KILA LA KHERI U-20

MECHI YA SIMBA NA YANGA PRESHA TUPU

Watoto wa Jangwani Yanga wametamba wako kwenye morali ya juu kuua mnyama hapo Jumapili kwenye uwanja wa Taifa mchezo utakaopigwa usiku saa 2.

Afisa habari wa Yanga Luis Sendeu amesema kikosi kiko imara na kinaendelea na maandalizi yake vizuri huku leo wakipokea wachezaji wawili wa kigeni wanaotokea nchini Ghana waliokuja kufanya majaribio.

Wakati Watoto hao wa Jangwani wakijinadi hivyo huko Msimbazi nao wanasema wako tayari kuwatia kitanzini watoto hao wa Jangwani.

Meneja wa Simba Innocent Njovu anasema wako kamili na kocha Patrick Phiri anarejea kesho kuwaongezea nguvu zaidi.

TUFANYE MAZOEZI KUJENGA AFYA

Watanzania wameombwa kujitokeza kwa wingi kushiriki mbio za hisani zinazotarajia kufanyika April 17 mwaka huu.

Kiongozi katika mbio hizo Meritus Magungu amesema mbio hizo ambazo zitakuwa ni matembezi mafupi zitafanyika mara kwa mara ili kujenga afya za vijana.

Matembezi hayo yataanzia tabata segerea na kumalizikia tabata Relini.

SHINYANGA KUJENGA SHULE YA MICHEZO

Mdau wa soka na mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Hamis Mgeja ameamua kujikita na kuwekeza kwenye sekta ya michezo nchini.

Mgeja amesema sasa ameamua kuwekeza kwenye sekta ya michezo akiwa na malengo ya kuanzisha kituo cha michezo kitakachoanza kujengwa mwezi ujao huko Shinyanga huku hii leo akikabidhi mipira kwa timu mbalimbali zikiwemo za Wilayani Maswa kwenye kata ya Kadoto.

TFF LAWAFUNGIA VIONGOZI, WACHEZAJI LIGI DARAJA LA KWANZA


KAMATI ya Mashindano ya Shirikisho la Soka Tanzania TFF,limewaangushia rungu baadhi ya viongozi na wachezaji wa timu za Daraja la Kwanza kwa utovu wa nidhamu akiwemo Meneja wa Mwanza United, Evarist Hagira ambaye ametozwa faini ya sh. milioni 1 na ushee huku pia akifungiwa miezi sita kujihusisha na michezo.

Kamati hiyo ilikutana Jumamosi jijini Dar es Salaam kujadili mambo mbalimbali yanayohusu ligi daraja la kwanza.

Afisa Habari wa TFF, Frolian Kaijage, amesema baada ya kuitathimini ligi daraja la kwanza waligundua kuna kasoro zilizojitokeza katika baadhi ya michezo ya ligi daraja la kwanza.

Amesema katika mchezo namba 31, kati ya TMK United na Mwanza United, Kocha wa Mwanza United,John Tegete aliwashawishi wachezaji wake kugomea mchezo na kamati imeamua kumfungia miezi mitatu kujihusisha na masuala ya soka.

Amewataja baadhi ya wachezaji wa timu hiyo ambao pia wamekumbwa na rungu hilo la kufungiwa miezi mitatu kujihusisha na soka, kuwa ni pamoja na Hamis Ally, Paulo Joseph, Naftari Matari, Emmanuel Sitta na Othman Othman.

Kaijage amesema mchezo namba tano kati ya Watoto wa A town AFC ya Arusha dhidi ya Mwanza United, mashabiki wa AFC walimfanyia fujo mwamuzi baada ya mpira kumalizika, hivyo nayo AFC imetozwa faini ya Shilingi 150,000.

Ameongeza kuwa mchezo namba 12 kati ya Ruvu Shooting ya Pwani na Coastal Union ya Tanga, waamuzi wa mchezo huo Bamy Bahisha na Mustapha Abdi walichezesha chini ya kiwango, hivyo wamefungiwa miezi mitatu kujihusisha na masuala ya soka.

WATANO MBEYA WASHINDA TIKETI Coca-Cola KWENDA KOMBE LA DUNIA AFRIKA KUSINI


Mbeya Aprili 13, 2010... Promosheni ya Kwea Pipa na Coca-Cola inazidi kupamba moto ambapo wateja watano wa Coca-Cola mkoani Mbeya wamebahatika kushinda tiketi kwenda kushuhudia mechi ya fainali ya Kombe la FIFA la Dunia kati ya Brazil na Ureno itakayochezwa kwenye uwanja wa kisasa wa Moses Mabhida jijini Durban Juni 25, 2010.

Fainali za Kombe la FIFA la Dunia zimebeba uzito wa pekee barani Afrika mwaka huu kwa kuwa tamasha hili linalovuta hisia za mamilioni ya wapenzi wa mpira wa miguu duniani linafanyika kwa mara ya kwanza kwenye ardhi ya Afrika tangu kuanzishwa kwake 1930.

Washindi waliotangazwa jijini Mbeya hivi leo ni sehemu ya wateja wa Coca-Cola 200 ambao kampuni hiyo ya vinywaji baridi itawapeleka Afrika kusini kwenda kuungana na maelfu ya wapenzi wengine wa soka kutoka sehemu mbali mbali duniani kusherehekea kombe la dunia.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza washindi hao, Meneja Mauzo wa Coca-Cola Kwanza, Mkoani Mbeya, Bw.Francis Mroso aliwataja washindi hao kuwa ni Deogras L. Kapesa (43) mfanyabiashara wa Mlowo, Mbozi, Tujelimpoki Frank (24), mfanyabiashara kutoka Kyela, Raphael Paul Ngungwi (33), pia mfanyabiashara wa Makunguru, Mbeya.

Wengine in Ally David Kaisi (23) wa Nzovwe, Mbeya ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini na Kelvin Mallya (36) ofisa kutoka Ofisi ya Uhamiaji Tunduma, Mbeya. Waliobahatika kushinda TV aina ya Sony zenye muundo wa kisasa (flat screen) inchi 32 ni Benedicto George, Daniel Kisunga na Petrol Sanga wote wafanyabiashara.

“Tunafurahi kwamba watu wengi wemejitokeza kushiriki promosheni yetu ya Kwea Pipa na Coca-Cola: Shinda tiketi ukasherehekee Kombe la FIFA la Dunia ambayo inawapa fursa adimu Watanzania 200 watakaobahatika kushinda tiketi kwenda kutazama mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia”, alisema Mroso.

Mbali na tiketi za kwenda Afrika Kusini Coca-Cola pia itatoa zawadi mbali mbali kwa wateja 1,200,000 ikiwa ni pamoja na Televisheni ya muundo mpya (flat screen) aina ya Sony, fulana, kofia na soda za bure.

Ili kushiriki, wateja wanatakiwa kununua chupa zenye ujazo wa 300ml au 350ml za Coca-Cola, Sprite au Fanta na kuangalia chini ya kizibo kuona zawadi walizoshinda. Promosheni hii inafanyika katika mikoa yote ya nchi Tanzania hadi Mei 31 na washindi wataendelea kuchukua zawadi zao hadi Juni 15, 2010.

“Napenda kutoa wito kwa Watanzania wote kuendelea kuburudika na vinywaji vya jamii ya Coca-Cola: Coca-Cola, Fanta au Sprite na kuweka hai matumaini ya kujishindia tiketi za kwenda kutazama mechi ya kusisimua ya kombe la dunia kati ya Brazil na Ureno”,
Alisema Mroso.

Coca-Cola imekuwa mstari wa mbele katika kuwawezesha Watanzania kushuhudia matukio makubwa ya kimichezo. Mwaka jana Coca-Cola iliwawezesha Watanzania kuliona Kombe halisi la FIFA la Dunia kwa mara ya pili baada ya kuliona mara ya kwanza 2006. Coca-Cola pia iliwawezesha Watanzania kuuona laivu Mwenge wa Olympiki 2008 pamoja na kuwa sehemu ya shamra shamra ya Mbio za Mwenge wa Olimpiki ambazo hutangulia michezo ya Olimpiki, ambayo pia ni michezo inayotambaa ulimwenguni kwa umaarufu.

Tuesday, April 13, 2010

ZAIN YAZINDUA MALIPO YA TSHS 1 SAA 24 - "UHURU WA KUONGEA"

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Zain yazindua Malipo ya Tshs 1 saa 24 - "Uhuru wa Kuongea"
.Ongea kwa Tsh 1 kwa sekunde siku nzima.
.Ongea kwa Tsh 1 kwa sekunde kwa dakika usiku kucha.
.Hakuna kujisajili, Hakuna kikomo cha muda, Hakuna Malipo yaliyofichwa, Hakuna kukatika simu hovyo, Hakuna Msongamano wa simu.

Zain, Kampuni inayoheshimika zaidi Tanzani na inayoongoza kwa ubunifu wa bidhaa na huduma, leo imezidi kudhihirisha umahiri wake katika soko kwa kuzindua mpango mpya wa malipo ya kupiga simu yenye viwango vya chini kuliko vyote nchini wa Tsh 1 kwa sekunde unaojulikana kama " Uhuru wa Kuongea".

"Ninayo fuaraha kubwa kuwatangazia kwmaba kuanzia leo wateja wetu waliyopo na wapya katika mpango wa malipo kabla, moja kwa moja watajiunga na mpango wa Ths 1 kwa sekunde saa 24 ikiwa ni pamoja na kuweza kupiga simu kwa kiwango nafuu kuliko vyote cha Tsh 1 kwa dakika baada ya dakika ya kwanza ya Uhuru wa Kuongea wakati wa usikku. Mbali na kutoa ubunifu wa kisasa wa kiteknolojia pamoja na kuwa na huduma bora zenye kuambatana na mtandao kuenea nchi nzima, Zain imejidhatiti kuongoza katika sekta ya mawasiliano kwa kuzidi kutoa viwango nafuu zaidi kwa wateja wetu, na ndiyo maana tumezindua Uhuru wa Kuongea ikiwa ni kutambua mahitaji ya soko la huduma ya simu na kuzingatia unafuu. Hakuna kujisajili, wala gharama za kuhama kutoka mpango mmoja kwenda mwingine, tunaposema "Uhuru wa kuongea" tunamaanisha hicho hicho," Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Zain Tanzania Khaled Muhtadi.

Zain imeamua kuwa wazi na bayana, hakuna haja ya kujiunga, wasiwasi wa muda, malipo yaliyofichwa wala simu kukatika katika kutokana na msongamano. Wateja wa Zain wataweza kujivunia Uhuru wa Kuongea kwa urahisi kabisa saa 24 siku zote za wili wakiwa na uhakika wa mtandao madhubuti na ulioenea nchi nzima.

Akiongea na waandishi wa habari wakati wa usinduzi wa mpango huo mpya wa malipo Jijini dar es Salaam, Mkurugenzi wa masoko wa Zain Tanzania Ahsan Syed alisema, "Zain imewekza zaidi ya dola za Marekani milioni 500 katika miundo mbinu ya mawasiliano katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kuhakikisha tunawapa wateja wetu huduma bora ya viwango nafuu popote pale walipo nchini. Mpango wetu wa malipo ya Ths 1 ni rahisi na hauna mkanganyiko wowote na ni kwa saa 24 kwa siku. Muda wa usiku kati ya saa tano usiku hadi saa moja Alfajiri, wateja wa Zain watapiga simu kwa viwango vya chini kabisa kwa Tsh 1 kwa dakika baada ya dakika moja ya kwanza. Wateja wa Zain hawatalazimika kuangalia saa zao za mkononi au ukutani kujua kama wako katika muda wa viwango vya malipo ya Tsh 1, na hii ndiyo inatutofautisha na makampuni mengine."

"Tunatambua kwamba kufanikisha kupatika mawasiliano ni eneo ambalo tunatoa mchango mkubwa kwa jamii na kuchangia kushamiri kwa uchumi wa Tanzania. Simu za mkononi zina mchango mkubwa katika uchumi wetu na ndiyo sababu siyo tu kwamba tunaleta bidhaa zenye ubunifu mkubwa lakini pia tunahakikisha mtandao wetu ni wa kutegemewa na uliyosambaa maeneo mengi zaidi nchini Tanzania. Pia tumesambaza mtandao wetu na bidhaa zetu nchi maeneo mengi vijijini ili kuwawezesha mamilioni ya watu wanaoishi maeneo ya vijijini kuwasiliana na ndugu zao wanaoishi mjini na kuwapunguzia adha mbali mbali zinazosababishwa na umbali. kupitia Uhuru wa Kuongea, Zain inazidi kuwathibitishia wa Tanzania maana halizi ya Ulimwengu maridhawa" Mkurugenzi wa Mtandao wa Zain tanzania Thierry Diasonama alisema.