
OKINAWA GOJU RYU KARATE - DO - JUNDOKAN KURO OBI KAI DOJO waadhimisha miaka 37 tangu kuanzishwa kwa dojo hilo mwaka 1973 na Sensei Nantambu Camara Bomani.

Hii ni picha ya muasisi wa mchezo huu hapa Tanzania Sensei Nantambu Camara Bomani.

Hawa ndiyo wanaoendeleza mchezo huu wa GOJU RYU katika dojo ambalo Sensei Bomani alianzisha mchezo huu nchini Tanzania katika shule ya msingi ya Zanaki ya Jijini Dar es Salaam.

Hawa ni wale ambao wanamikanda myeusi wakionyesha namna ambavyo mtu anaweza kupambana na mtu mwenye kisu na ukamshinda, aliyelala chini ndiye mwenye kisu.

Hawa ni wale wenye mikanda ya Kijani wakionyesha umahiri wao katika mchezo wa Goju Ryu ama unaweza ukaiata sanaa ya mipigano.

Hawa ni wale ambao wanakaribia kuwa na mkanda Mweusi wakionyesha umahiri wao katika sanaa ya mapigano.

Huyu ni Japhet Kaseba Bingwa wa Kick Boxing wa WK1 Dunia naye akifuatilia kwa makini.

Mdau mwenzangu huyu Ankal Michuzi naye akifuatilia kwa ukaribu namna mtu anavyoweza kupigana kwa ustadi bila kutumia silaha, au siyo Brother Michuzi...???

Waliyo kaa chini ndiyo ambao walitunukiwa mikanda ikiwa ni ishara ya kupandishwa ngazi katika mchezo huo, huku mmoja akipewa mkanda mweusi, aliyesimama kulia ni Sensei Rashid Almasi na aliyening`iniza mewani watano toka kulia ni Sensei Wilfred Malekiu.
No comments :
Post a Comment