UONGOZI wa Dar es Salaam Young African maarufu Yanga umesema hauna mpango wa kumbania Mshambuliwa wao Jerrson Jerry Tegete kusukuma gozi la kulipwa nchini Sweden kwenye klabu ya DULKUD FF ya Sweden.
Afisa habari wa Yanga Luis Sendeu amesema wanataka mchezaji wao arudi kwanza halafu ndio mambo mengine yatafuata baadaye.
Amesema wao ndiyo waliyomruhusu kwenda kufanya majaribio wakiwa wanaamini atafanikiwa kutokana na kiwango chake lakini makubaliano yalikuwa ni lazima arejee baada ya kumaliza majaribio awe amefanikiwa ama la.
Sendeu amesema kumtaka arejee nchini kwanza inatokana na wao kutaka kujua aina ya mkataba ambao wataingia na klabu hiyo kwa mkopo lakini pia kufahamu klabu ya Yanga itafaidika vipi na mchezaji huyo ikiwa na maslahi ya mchezaji mwenyewe.
Wakala wa wachezaji Mzalendo Damas Ndumbaro aliweka bayana kuwa watoto hao wa Jangwani wamekataa Tegete kucheza kwa mkopo kwenye klabu hiyo ya Dalkud FF kiasi cha nafasi yake kupewa Uhuru Suleiamn wa Simba.

No comments :
Post a Comment