Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, April 13, 2010

JULIUS MBILINYI ANG`ARA GOFU YA ZAIN


Julias Mbilinyi ameng’ara katika mashindano ya mchezo wa gofu yanayodhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Lugalo jijini Dar es Salaam baada ya kupata pointi 39.

Jualias alifuatiwa na Ali Mufuruki ambaye naye pia alijikusanyia pointi 39 lakini Julias alimzidi mpinzani wake katika tofauti ya viwango vya uchezaji.

Kufuatia ushindi huo Julias na Mufuruki walijinyakulia zawadi mbalimbali ikiwemo mwavuli na kalamu, Vyote vikiwa na nembo ya Zain kutoka kampuni ya Zain ambao ndiyo wadhamini wakuu wa mashindano hayo.

Mashindano hayo ambayo uchezwa katika makundi tofauti yalishuhudia washindi wengine kutoka katika kundi la akina mama pamoja na kundi la vijana wa kike na wa kiume.

Kundi la akina mama liliongozwa na Lina Nkya aliyepata pointi 17, kundi la vijana wa kike liliongozwa na Sara Denis aliyepata pointi 31. Akina mama na vijana wa kike walijishindia khanga za Zain.

Kundi la vijana wa kiume liliongozwa na Joshua Amoni aliyepata pointi 37 akifuatiwa na Baraka Masari aliyepata pointi 37, lakini wakatofautiana katika viwango vya uchezaji. Washindi hawa walizawadiwa kalamu za Zain pamoja na miavuli ya Zain.

Kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania ina mkakati maalum kwa kushirikiana na klabu ya mchezo wa gofu ya Lugalo ya jijini Dar es Salaam wenye lengo la kukuza mchezo wa gofu kuanzia kwa vijana wadogo ili kukuza vipaji.

No comments :

Post a Comment