Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mh,
Mwantumu Mahiza siku ya jumamosi wiki hii anatarajia kuongoza Bonanza la
Wanavyuo linaloendea sehemu mbali mbali na ikiwa ni sehemu ya tatu kwa kanda ya
kaskazini inayoendelea lwemye viwanja mbali mbali chini ya Kampuni ya Miss
Demokrasia Tanzania & Entertainment C.o Ltd kwa kushirikiana na kituo
bora cha Matangazo TIMES FM 100.5.
Bonanza hilo ambalo ni kwa ajili
ya kupata timu zitakazoshiriki michuano ya NACTE linatarajiwa kuwa gumzo kwa
mkoa wa Pwani kutokana na mfumo wake uliobuniwa kiufundi na waandaaji ambapo
timu mbali mbali za Viongozi wa Serikali na zile za mkoa upata fulsa ya
kushiriki pamoja kwa kufanya michezo ya soka, kikapu,netball pamoja na
Voleyball.
Akizungumzia bonanza la jumamosi
Mratibu wa Michezo Vyuoni, Mpalule Shaaban alisema kuwa Mh, Mwantumu anatarajia
kufanya Uzinduzi wa Michezo hiyo kwa Mkoa wa Pwani kutokana na kwamba sasa
Michezo hiyo itafanyika kila mwaka Sehemu mbali mbali za Tanzania.
"Ni heshima ya pekee ambayo
Serikali imetoa kwa Vijana wetu wa vyuo vya elimu ya kati kushiriki michezo,
kumbuka kwamba michezo hii aijawahi kuwepo tangu NACTE imeanzishwa hivyo hii ni
fulsa ya pekee tuliyonayo katika kuhakikisha kwamba tunahamasisha michezo hii
wakati wote ili vijana wanaojiunga na Vyuo vya Elimu ya Ufundi, Veta, na wale
wa ngazi ya Diploma kushiriki michezo vyuoni"alisema Mpalule.
Sehemu ya pili imefanyika
mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya ustawi wa jamii kijitonyama tarehe
29/11/2014, ambako Vyuo mbalimbali vya NACTE mkoa wa dar es salaam, vilicheza
katika michezo ya soka, Basketball, Voleyball na netball,katika kutafuta timu
zitakazoshiriki ligi ya NACTE Tanzania katika msimu wa 2014/2015.
sehemu ya kwanza Ilizinduliwa
kwenye chuo cha DIT tarehe 22/11/2014 mwezi huu na kusisimua wengi
katika Michuano lutokana na kuwa na mfumo wa mtoano kuwa kivutio kwa
Wachezaji na Mashabiki ambao wengi wao ni wanafunzi kutoka vyuo mbali mbali
wanaofika kushuhudia michuano hiyo inayoendeshwa kwa ubunifu wa hali ya juu.
Vyuo vilivyokwisha cheza ni Institute of Adult Education, Institute of Social Work (ISW) - DSM, Lugalo Military Medical School - Dsm, St. Joseph College (University), Dar es salaam City College (DACICO, Dar-es-Salaam School of Journalism (DSJ) - DSM, National Institute of Transport (NIT) - DSM, Bandari College - DSM,huku
timu mwalikwa ikiwa ni Timu ya wafanyakazi wa PPF Dsm.
Vyuo
vingine ambavyo tayari vimemaliza michezo yao ya awali ni pamoja na IFM ,DIT, CBE, Muhimbili,TRA, Mlimani Profesianal,na Royal College,
waliokuwa kundi la kwanza lililofanyika viwanja vya chuo cha DIT akiba Posta.
Aidha
vyuo vyote vinavyohusika na michezo ya wiki hii zimetakiwa kuwahi Viwanjani ili
kukamilisha taratibu za ukaguzi kabla ya michuano hiyo ya mtoano kuanza na
ikumbukwe kwamba michuano hiyo inaendeshwa kwa mfumo wa Bonanza na inafanyika
kila siku za jumamosi kutokana na wanafunzi kuwa masomoni katika siku za
kawaida.
kila mwaka michuano hii itakuwa
ikifanyika kwa kushirikisha vyuo mbali mbali vya elimu ya kati hapa
nchini Tanzania na vilivyopata usajili wa kudumu wa NACTE ambapo Kanda mbali
mbali za Tanzania kupitia vyuo vyao vitashindana katika michezo mbali mbali kwa
wavulana na wasichana ni vyuo 32 tu vitakavyokuwa vikishiriki baada ya kufanya
mchujo wa awali kwa njia ya Bonanza na Timu mbili za juu kila BONANZA ndizo
zitakazokuwa zikiingia katika idadi ya vyuo 32 vya NACTE ITER COLLEGE DAR ES
SALAAM.
Ukiachilia mbali michezo hiyo, michezo mingine
itakayokuwa ikifanyika kati ya wanafunzi na wanafunzi ni DEBATE, Marathon,
Modoling, Mashindano ya Vipaji kwa viongozi wanaosimamia serikali za
wanafunzi kwa nafasi za Rais na Makamu, Waziri Mkuu, Mawaziri wa
Michezo,Fedha, na Spika , watakaokuwa wakichuana katika kujielezea,
kujibu maswali, na kuelezea Mada katika nafasi zao na changamoto
wanazokabiliana nazo na washindi watakuwa wakipata tuzo mbali mbali kulingana
na ushindi wa kila mmoja.
Wadhamini
aliojitokeza mpaka sasa na kuonyesha nia ya kusaidia mashindano hayo ni pamoja
na Coca Cola, Vodacom, MLONGE BY MAKAI, CXC –Tours,Bonga Resort &
Hoteli, Ikondolelo Hoteli, na 100.5 Times Fm.
lakini
hata hivyo dirisha la wadhamini bado liko wazi kwa maana bado gharama ni kubwa
za uendeshaji ambapo wajitokeze waweze kusaidia michezo hii iliyoanza kwa
shamrashamra nyingi na kuwa na mvuto kwa watazamaji ususani wanafunzi wa vyuo
mbalimbali waliojitokeza.
No comments :
Post a Comment