Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, July 3, 2014

OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO YAKAGUA MRADI WA MAKAA YA MAWE NGAKA




Viongozi na maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na wale wa NDC wakipata maelezo kuhusu mradi wa makaa ya mawe Ngaka kutoka kwa Mtaalam wa Kudhibiti Ubora (Quality Control Superintendent) Bw. Boscow R. Mabena.
Timu kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na NDC wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kikundi cha Wanawake cha Mbalawala, Bi. Joyce Haule juu ya matumizi ya makaa ya mawe majumbani. Makaa hayo hutumika majumbani kwa kutumia majiko maalum baada ya kubadilishwa kitaalam na kuwa rafiki kwa matumizi ya majumbani. Mbalawala kinajihusisha na shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwa ni jitihada za kumkwamua mwanamke kiuchumi.
Majiko maalum yanayotumia mkaa uliotokana na makaa ya mawe kwa ajili ya kupikia majumbani.
Mtaalam wa Kudhibiti Ubora, Bw. Boscow R. Mabena akitoa maelezo namna ambavyo Coal Briquett Machine (Pichani) hutumika kubadili makaa ya mawe kutoka hali yake ya mwanzo baada ya kuchimbwa na kutengenezwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (ORTM), Dkt. Philip I. Mpango, (wa tano kutoka kushoto) akikagua Mradi wa Makaa ya Mawe Ngaka. Wengine ni viongozi na maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na Shirika la Maendeleo la Taifa – NDC pamoja na wataalam wa kampuni ya TANCOAL inayojishughulisha na uchimbaji wa makaa ya mawe. 
Viongozi na Maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na NDC wakiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa Kampuni ya TANCOAL ndani ya mgodi wa makaa ya mawe. Kampuni ya TANCOAL ndiyo inayohusika nauchimbaji wa makaa ya mawe katika Mradi wa Mkaa ya Mawe Ngaka. Picha na: Thomas Nyindo, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MABALOZI WA OMAN NA SYRIA NCHINI TANZANIA. IKULU DAR





 Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi wa Oman nchini Tanzania, Saoud Ali Mohammed Al-Ruqaish, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 3, 2014 kwa mazungumzo.
 Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Oman nchini Tanzania, Saoud Ali Mohammed Al-Ruqaish, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa mazungumzo.
 Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi wa Syria nchini Tanzania, Abdulmonem Annan,  wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa mazungumzo.
Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Syria nchini Tanzania, Abdulmonem Annan, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa mazungumzo. 
********************************************
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AKUTANA NA MABALOZI WA OMAN NA SYRIA

Ikulu jijini Dar es Salaam, Julai 03, 2014
Makamu wa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal leo Alhamisi Julai 03, 2014 amekutana na Waheshimiwa Mabalozi wa nchi za Oman na Syria wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania. Mheshimiwa Makamu wa Rais amekutana na Mabalozi hao ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.

Awali alikuwa ni Balozi wa Oman, Mheshimiwa Saoud Ali Mohammed Al-Ruqaish aliyefika kukutana na Mheshimiwa Makamu na kufafanua kuwa uhusiano baina ya Tanzania na Oman unazidi kuimarika na kwamba wawekezaji kutoka Oman wamekuwa wakija kwa wingi kuwekeza Tanzania tofauti na siku za nyuma huku pia Tanzania ikionesha kufungua milango yake kwa uwekezaji mkubwa wa kati nchini Tanzania.

Kwa upande wa Balozi wa Syria Mheshimiwa Abdulmonem Annan yeye alimueleza Mheshimiwa Makamu wa Rais kuwa Syria iko katika kipindi kigumu na kwamba nchi hiyo kwa sasa inatafuta kila linalowezekana kurejesha amani. Balozi huyo alifafanua kuwa nchi yake inahitaji msaada wa nchi za Kimataifa ili kusaidia kuweka pande zote zinazokinzana mezani kwa lengo la kufikia maazimio yatakayoifanya nchi hiyo isiparanganyike.
Mheshimiwa Makamu wa Rais alimueleza Balozi za Syria kuwa, Tanzania inatamani sana kuona hali ya utulivu inarejea Syria na kwamba nchi hiyo inaendelea kujenga uchumi uliobomoka tayari. Pia alisema kuwa msimamo wa Tanzania unabakia katika kutaka pande zinazohusika katika mgogoro huo zinafuikia suluhu kwa amani ili wananchi wengi wasipoteze maisha.
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Ikulu Dar es Salaam

ENZOY DAWA YA NGUVU YA KIUME INARETA HESHIMA






TIBA YA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME NA KIKE UVUMBUZI WAKE KITABU HIKI HAPA




KITABU AMBACHO KINATOA TIBA ZA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME NA KIKE KWA KUTUMIA VYAKULA VYA ASILI IKIWEMO MATUNDA NA MBOGA MBOGA ZA MAJANI SASA KIPO MITAANI KINAPATIKANA MITAA YA UHURU NA MSIMBAZI KWA MAITAJI YA KITABU HIKI NA DAWA MBALIMBALI ZA KUTIBU MARADHI PAMOJA NA MATATIZO PIGA SIMU  0787406938

TANGAZO LA DAWA YENYE NGUVU ENZOY





DAWA YA NGUVU ZA KIUME NA MSIMKO KWA WANAWAKE WASIO NA HAMU YA TENDO LA NDOA AMBAYO HULETA MSISIMKO KWA WANAUME NA WAKE WAKUTANAPO.KWA SASA INAPATIKANA KWA BEI NAFUU HAPA JIJINI DAR ES SALAAM MAKUTANO YA MTAA WA KIPATA NA BARABARA YA MSIMBAZI
ALLY WA YANGA BOMBA UHURU NA MSIMBAZI 0787230551 AU 0652755838




PIGA SIMU KWA MR.MKUNJE O713827689, 0755074505 , au 0719 541366
,0652755838 UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM


BUGURUNI LOZANA STENDI YA TAX ULIZIA ADAMU KIBANDANI 0755875884
SHULE YA UHURU FIKA JENGO LA AZAM BAKHRESA ULIZA NGAEJE 0713873412
MWANANYAMALA FIKA JABA KLABU  ULIZA MACHELLAH 0713470492
ENZOY INALETA HESHIMA
Photo: whatsapp 0713406938
whatsapp 0713406938

BUJINGA TRADERS WATENGENEZAJI WA FLIERS,POSTERS,CARDS & CARENDER






BUJINGA TRADERS WATENGENEZAJI WA  FLIERS,POSTERS,CARDS & CARENDER WAPO MACHINGA COMPLEX  4TH FLOOR E4, EAST WING
Email; johnson@bujingatradere.com,info@bujingatraders.com
www.bujingatraders.com
P.O. BOX 43064
Dar es Salaam Tanzania 
Cell+255765224522 Tel;+255773623320
Tanzania East Africa


BUJINGA TRADERS WATENGENEZAJI WA  FLIERS,POSTERS,CARDS & CARENDER WAPO MACHINGA COMPLEX  4TH FLOOR E4, EAST WING
Email; johnson@bujingatradere.com,info@bujingatraders.com
www.bujingatraders.com
P.O. BOX 43064
Dar es Salaam Tanzania 
Cell+255765224522 Tel;+255773623320
Tanzania East Africa

TANGAZO LA UTAFITI NA MGANGA WA TIBA ZA JADI TANZANIA DR,CHIFU UWEZO MOTO WA RADI


DR. CHIFU UWEZO
DR. CHIFU UWEZO MOTO WA RADI KUTOKA KIGOMA SASA YUPO DAR ES SALAAM MAENEO YA GONGOLAMBOTO
ANARUDISHA MALI ILIYOPOTEA KAMA GARI,MIFUGO UWANJA,SHAMBA ,NYUMBA ILIYO DHULUMIWA PESA ZILIZOPOTEA
ANAIFANYA BIASHARA YAKO INUNULIKE NA KUFANYIA MAOMBI YA KUKUBALIKA

ANAFANYA MAZINDIKO MBALIMBALI KAMA VILE NYUMBA SHAMBA MALI NA KADHA WA KAZA 

WANAOWAI KUFIKA KILELENI WAKATI WA TENDO LA NDOA NA MIGUU INAYOWAKA MOTTO KUVIMBA MIGUU 

DAWA YA KUKUZA KIUNGO CHOCHOTE MWILINI MAKALIO ,UUME NA KUPUNGUZA MATITI TUMBO

DAWA ZA NGUVU ZA KIUMA AMBAZO ZINASAIDIA KUSHILIKI TENDO LA NDOA KIKAMILIFU PAMOJA NA DAWA ZA NGUVU ZA KIUME
YOTE YANAWEZEKANA KWA UWEZO WA MUNGU
WOTE MNAKARIBISHWA KWA DR,CHIFU UWEZO MOTO WA RADI KWA MAELEZO ZAIDI
PIGA SIMU NAMBA
0719272582
0688000893
0756095435
NB TIBA KWA WATOTO WADOGO NA WAZEE NI BURE KWA WATU WAZIMA MALIPO MPAKA MAFANIKIO YAONEKANE

Wednesday, July 2, 2014

MFARANSA SEAN GARNIER AJA TANZANIA KUONYESHA UMAHIRI WA KUCHEZA MPIRA WA MTAANI HUKU AKIBINUKA SARAKASI NA KUCHEZA DANSI


 Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier (katikati) ambaye yuko nchini Tanzania kwa ziara maalum ya kimichezo akifafanua machache mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kutambulishwa. Pembeni yake kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Mohn's John Ntuli na Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya Mohan’s Vijay Joshi.

 
 Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier akionyesha staili mbali mbali za kucheza mpira mbele ya waandishi wa habari.
 Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier akionyesha jinsi ambavyo unaweza kupiga danadana huku ukiwa unacheza mziki staili mbali mbali.
  Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier akionyesha jinsi ambavyo unaweza kupiga danadana na kupita katika tundu dogo huku ukiendelea na mchezo. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa leo anatarajiwa kuonyesha shoo ya bure ambapo ataonesha umahiri wa kucheza mpira wa mitaani, sarakasi na kucheza dansi.
Mfaransa huyo Sean Garnier ambaye yuko nchini kwa ziara maalum ya kimichezo jana usiku alianza ziara hiyo kwa kuonesha umahiri wake wa kucheza mpira wa mtaani katika viwanja vya ufukwe wa Coco (Coco Beach) jijini Dar es Salaam.
Garnier ambaye anakipaji cha kupiga danadana mpira huku akiweka mapozi mbalimbali alionekana kuwa kivutio mbele ya mkutano na waandishi wa habari ambao walikuwepo kwenye mkutano huo huku akionesha umahiri wake wa kupiga danadana na kucheza na mpira katika barabara ya Alli Hassan Mwinyi baada ya mkutano huo.
Mwenyeji wa ziara ya Garnier, Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya Mohan’s Vijay Joshi alisema kwamba huyu ni mwanamichezo mwenye kushikilia taji la kipaji cha kucheza ‘Free Style’ duniani.
“Ameletwa kwa udhamini wa ‘Redbull Street Sytle’ na atakuwa nchini kwa siku tano ambapo ni kati ya Julai 2 hadi Julai 7 ataondoka.
Aidha mbali ya kumudu kucheza na mpira pia nacheza sarakasi katika mitindo mbalimbali huku akiwataka watanzania kuiga baadhi ya michezo ambayo ataionyesha akiwa atakapokuwa mtaani.
Baadhi ya mitaa atakayo pita ni Kariakoo, Mlimani City, Posta, Viwanja vua Sabasaba, Chuo Cha Biashara (CBE) na Sea Clif Jijini Dar es Salaam.

MCHUJO WA WASHIRIKI WA SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) KUANZA RASMI



 Jukwaa likitengenezwa kwaajili ya Washiriki Wa fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kupanda jukwaani na kuanza kuonyesha vipaji vyao, Onyesho hili ni onyesho la kwanza la kuelekea Kwenye Mchujo wa kumpata mshiriki Mmoja atakayejinyakulia kitita cha Shilingi Milioni 50 katika fainali kubwa itakayofanyika mwishoni mwa Mwezi wa Nane.
Mahost wa Show ya Tanzania Movie Talents (TMT) Joti na Lulu wakiwa kwa Steji tayari kwa Show kuanza
Timu ya Tanzania Movie Talents (TMT) ikiwa katika maandalizi ya mwisho mwisho kabla ya Show ya Tanzania Movie Talents katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa usiku huu
 Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar waliohudhuria kwaajili ya kutazama onyesho la washiriki wa fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) linaloendelea kufanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
 Wadau waliojitokeza kwaajili ya Kushuhudia onyesho la Tanzania Movie Talents.Picha na Josephat Lukaza
***************************************************
Na Josephat Lukaza, Dar Es Salaam.
Washiriki 20 wa Shindano la Tanzania Movie Talents ambao ni washindi kutoka kanda 6 za Tanzania wamepanda kwa steji katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa kwaajili ya kuanza kuonyesha vipaji vyao vya kuigiza.  Sasa ni safari kwa washiriki kuelekea kwenye kinyanganyiro cha kuwania Milioni 50 za Kitanzania katika fainali kubwa itakayofanyika Mwisho wa Mwezi wa Nane.
Katika Onyesho hili litakalorushwa katika Runinga ya ITV siku ya Jumamosi saa 4 usiku kitakuwa kipindi cha kwanza kwa watanzania kuanza kuangalia na kuwapigia kura washiriki ambao watakuwa wamewavutia na kukonga nyoyo zao na hatimaye kuwawezesha kushiriki katika fainali kubwa Mwishoni mwa Mwezi wa Nane.
Watanzania wanatakiwa kuendelea kutazama muendelezo wa vipindi vya TMT kupitia Kituo cha Runinga cha ITV saa nne Usiku siku ya Jumamosi na hatimaye kuanza kuwapigia kura washiriki. Ili kuweza kupata Taarifa za TMT unaweza kutuma neno "TMT" kwenda namba 15678
Mchujo kwa washiriki sasa waanza rasmi ili kuweza kumpigia kura mshiriki umpendae unatakiwa kutuma neno "TMT ikifuatiwa na namba ya Mshiriki" kwenda namba 15678

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AIWAKILISHA TANZANIA KWENYE MADHIMISHO YA MIAKA 52 YA UHURU WA BURUNDI



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano mwa Tanzania Mhe. Dkt Mohammed Gharib Bilal, Mkewe Mama Zakhia Bilal, Rais wa Burundi Mhe. Piere. Nkurunzinza, na baadhi ya viongozi wa meza kuu, wakisimama kupokea maandamano ya maadhimisho ya Miaka 52 wa Uhuru wa Nchi hiyo yaliyofanyika jana katika uwanja wa Prince Louis Rwegasore jijini Bujumbura Burundi. 
Rais wa Burundi Mhe. P. Nkurunziza akikagua gwaride rasmi kwa ajili ya maadhimisho ya Miaka 52 wa Uhuru wa Nchi hiyo yaliyofanyika katika uwanja wa Prince Louis Rwegasore jijini Bujumbura Burundi. 
 Rais wa Burundi Mhe. P. Nkurunziza, akisalimiana na mke wa Makamu wa Rais wa Tanzania, Mama Zakhia Bilal, walipokutana kwenye Uwanja wa Prince Louis Rwegasore jijini Bujumbura Burundi wakati wa maadhimisho ya Miaka 52 wa Uhuru wa Nchi hiyo yaliyofanyika jana.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais wa Burundi Mhe. P. Nkurunziza walipokutana kwenye Uwanja wa Prince Louis Rwegasore jijini Bujumbura Burundi wakati wa maadhimisho ya Miaka 52 wa Uhuru wa Nchi hiyo yaliyofanyika jana.
 Burudani kutoka kwa vikundi vya Burundi.....
Ujumbe wa Tanzania uliofuatana na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal kwenye maadhimisho ya Miaka 52 wa Uhuru wa Nchi hiyo yaliyofanyika leo Julai 1-2014 katika uwanja wa Prince Louis Rwegasore jijini Bujumbura Burundi.  Picha na OMR
****************************************
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA SIKU YA UHURU WA BURUNDI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo Jumanne Julai Mosi, 2014 ameiwakilisha Tanzania katika sherehe za kilele cha miaka 52 ya Uhuru wa Burundi, sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Prince Louis Rwagasore.
Katika sherehe hizo pamoja na Makamu wa Rais wa Tanzania, pia kulikuwa na Makamu wa Rais wa Somalia, Waziri Mkuu wa Chad na viongozi mbalimbali waliowakilisha nchi kutoka Afrika. Sherehe hizo zilianza kwa Rais Pierre Nkurunzinza kuweka silaha katika eneo  maalum la Uhuru na kufuatiwa na maadhimisho yaliyoshirikisha wananchi mbalimbali katika uwanja wa Rwagasore.
Akizungumza baada ya kutoa tuzo mbalimbali za heshima, Rais Nkurunzinza aliwashukuru wageni wote waliofika katika sherehe hizo na akabainisha kuwa Tanzania ni rafiki wa Burundi hivyo anafurahishwa sana kuona ikiwa imewakilishwa na uongozi wa ngazi za juu katika sherehe hizo.
Burundi ambayo inategemea sana bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania na hasa uwepo wa Ziwa Tanganyika ambalo linaiunganisha na Tanzania, inaadhimisha miaka 52 ya uhuru huku ikiwa imepiga hatua mbalimbali kiuchumi sambamba na kisiasa kufuatia kuwa na miongo kadhaa ya mauaji ya wenyewe kwa wenyewe. Kwa sasa Burundi licha ya kukua kimaendeleo pia inaongezeka idadi ambapo inakadiriwa kuwa na watu milioni 6. Uhusiano baina ya Tanzania na Burundi unabaki kuwa wa damu ambapo pia redio za nchi hii hutangaza vipindi kadhaa kwa kutimia Kiswahili sambamba na nyimbo za muziki za wasanii wa Tanzania hupata nafasi kubwa katika redio za Burundi.
Katika sherehe hizo Mheshimiwa Makamu wa Rais pia alifuatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar, Mheshimiwa Haroun Ali Suleiman na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Mahadhi Juma Maalim.
 Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Julai Mosi, 2014 Bujumbura: Burundi