Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean
Garnier (katikati) ambaye yuko nchini Tanzania kwa ziara maalum ya
kimichezo akifafanua machache mbele ya waandishi wa habari mara baada ya
kutambulishwa. Pembeni yake kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Mohn's John Ntuli na Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya Mohan’s Vijay Joshi.
Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier akionyesha staili mbali mbali za kucheza mpira mbele ya waandishi wa habari.
Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier akionyesha jinsi ambavyo unaweza kupiga danadana huku ukiwa unacheza mziki staili mbali mbali.
Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean
Garnier akionyesha jinsi ambavyo unaweza kupiga danadana na kupita
katika tundu dogo huku ukiendelea na mchezo. Picha zote na Cathbert
Kajuna wa Kajunason Blog.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Mwanamichezo
kutoka nchini Ufaransa leo anatarajiwa kuonyesha shoo ya bure ambapo
ataonesha umahiri wa kucheza mpira wa mitaani, sarakasi na kucheza
dansi.
Mfaransa
huyo Sean Garnier ambaye yuko nchini kwa ziara maalum ya kimichezo jana
usiku alianza ziara hiyo kwa kuonesha umahiri wake wa kucheza mpira wa
mtaani katika viwanja vya ufukwe wa Coco (Coco Beach) jijini Dar es
Salaam.
Garnier
ambaye anakipaji cha kupiga danadana mpira huku akiweka mapozi
mbalimbali alionekana kuwa kivutio mbele ya mkutano na waandishi wa
habari ambao walikuwepo kwenye mkutano huo huku akionesha umahiri wake
wa kupiga danadana na kucheza na mpira katika barabara ya Alli Hassan
Mwinyi baada ya mkutano huo.
Mwenyeji
wa ziara ya Garnier, Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya Mohan’s Vijay
Joshi alisema kwamba huyu ni mwanamichezo mwenye kushikilia taji la
kipaji cha kucheza ‘Free Style’ duniani.
“Ameletwa
kwa udhamini wa ‘Redbull Street Sytle’ na atakuwa nchini kwa siku tano
ambapo ni kati ya Julai 2 hadi Julai 7 ataondoka.
Aidha
mbali ya kumudu kucheza na mpira pia nacheza sarakasi katika mitindo
mbalimbali huku akiwataka watanzania kuiga baadhi ya michezo ambayo
ataionyesha akiwa atakapokuwa mtaani.
Baadhi ya
mitaa atakayo pita ni Kariakoo, Mlimani City, Posta, Viwanja vua
Sabasaba, Chuo Cha Biashara (CBE) na Sea Clif Jijini Dar es Salaam.
No comments :
Post a Comment