Mgombea Uraisi Tucta Dismas Lyassa akijadiliana jambo na wakili wake Jebra Kambole. Picha na Mpigapicha Wetu.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA WATANZANIA WOTE
Ndugu zangu Watanzania
Asubuhi
ya leo tarehe 28 Julai 2014 nilitoa taarifa maalumu kwa vyombo vya
habari nikiitaka Serikali kutolea ufafanuzi malalamiko yaliyojaa kwenye
mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari. Asante Mungu kwamba
Serikali imetolea majibu jambo hili kwa kusitiza ajira zote.
Rejea
taarifa yangu kwa vyombo vya habari niliyoitaka Serikali kutoa majibu
katika suala hili asubuhi ya leo tarehe 28 Julai na nakala yake kutumwa
katika ofisi mbalimbali za Serikali.
Nachukua
fursa hii kuipongeza Serikali kwa kuwa sikivu katika hili na huenda
katika mengi yajayo, kama Rais Mtarajiwa wa Tucta baada ya uchaguzi
unaotarajiwa kufanyika Agosti 4-5 Dodoma, naahidi kushirikiana na
Serikali hasa kama itakuwa sikivu.
Nahitaji
kupatiwa majibu pia juu ya hatima ya mabaamedi wanaolazwa chumba kimoja
zaidi ya kumi tena siyo katika vitanda, bali zaidi huwa wanalala chini;
wanafanyakazi hadi usiku, wengine wanakoishi ni mbali na baa, hoteli
nk.
Nahitaji
kuona kero za walimu, wafanyakazi wa Serikali za Mitaa, madini, simu,
kilimo, utafiti afya, mawasiliano, reli, bandari nk zinakomeshwa; Ni
aibu hadi leo kuna walimu wanapoanza kazi wanalala kwa walimu wakuu
wakisubiri kupatiwa sehemu za kuishi, ni aibu hadi leo mwalimu
anafanyakazi kazi miezi sita inapita hakuna mshahara anaolipwa…hatuwezi
kwenda hivi, ni lazima majibu yapatikane.
Wafanyakazi
wa Tanzania tunapaswa kuimba nyimbo zingine, siyo za kero zile zile
kila kukicha. Naamini yote yanawezekana, cha msingi ni kwa Serikali na
waajiri kusimamia kwa haki mambo yote juu ya wafanyakazi. Hakuna
lisilowezekana tukipigania haki.
Imetolewa leo Julai 28, 2014
Na Dismas Lyassa
(Mgombea Uraisi TUCTA)
0754 49 8972/0712183282
No comments :
Post a Comment